Habari wakuu namshukuru Mwenyezi Mungu na natumaini mko salama.
Napenda kujumuika nanyi katika ukurasa huu kwa kugusia suala zima la afya hasa nikilenga kwa zile taasisi binafsi au mtu mmoja mmoja kuna changamoto nyingi katika jamii zetu unakuta mtu anaumwa hata pesa ya kula au mahali pa kuishi na akienda hospitali anatakiwa kutoa pesa ili apate huduma
Inafika hatua familia hata majirani wanamchoka na kumuona mzigo kutokana na maradhi yake mpaka itokee bahati ya taasisi au mtu amuwezeshe kwenda kupata huduma pengine imechukua muda mrefu kupata hizo taarifa na ikitokea hamna msaada kama huo basi mgonjwa anaweza kupoteza maisha au kuwa na ugonjwa sugu na wakudumu.
Mimi binafsi nina mapendekezo au ushauri kwa Serikali yetu
USHAURI:
1) Serikali inawajibu wa kuzitambua hizo taasisi au hao watu wanaojitolea.
2) Serikali inapaswa kutenga bajeti au maeneo ya vituo maalumu kwaajili ya watu(wagonjwa)ili iwe rahisi wao kupata huduma.
3) Kama kutakuwa na mchakato ili hizo taasisi ziweze kuwasaidia watu naomba serikali ipunguze au iweke njia rafiki ili iwe rahisi wao kupata mfano leseni,Vibali n.k maana kuna wengine wanamoyo wa kusaidia watu kupitia mitandao kwa kuchangisha watu wao kutokana na umaarufu n.k
4) Serikali kupitia Wizara ya Afya ijenge mahusiano mazuri na hizo taasisi ikiwa pia kuwapa vipaumbele kwenye mambo muhimu ikiwezekana kutoa tunzo ili kuwapa moyo zaidi.
5) Serikali iwasaidie hawa watu wa namna hiyo(wagonjwa)wapate huduma bure wanapokwenda kwenye huduma za afya.
6) Wananchi wawe wanatoa taarifa inapotokea mgonjwa ambaye ni masikini na anaugua kwa muda mrefu ili aweze kupatiwa msaada
NB: Hapa naongelea taasisi binafsi ambazo watu wanojitolea kusaidia kupitia michango ya watu mitandaoni na kwengine siyo zile taasisi zinazopokea misaada kutoka nje za nchi.Ahsanteni karibuni kutoa maoni

Upvote
1