Afya njema

Jimaz

Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
35
Reaction score
40
Habari wadau nna machache ya kushare kuhusu afya zetu hasa wamama. Kina mama wengi sikuhizi wameharibika shepu zao kwa sababu ya ulaji mbovu mimi binafsi kwakweli mazoezi siwezi kabisaaa ila kwa kuzingatia kanuni chache za afya na mshukuru Mungu niko na mwili mzuri na ninawatoto watatu lakini bado niko vizuri, unapozingatia haya fanya kwa faida yako binafsi si kwakumfurahisha mtu:

1) kula balance diet, wanga ule kwa kiasi kidogo sana hivyo vingine ndo vizidi
2) Kila muda wa kula ukifika kula usiruke mlo ila kula balanced diet
3) Unapokula chakula kula kwa kiasi usile mpaka mbavu zibane
4) Usile chakula huku unakunywa maji au kinywaji cha baridi hii itanasababisha chakula kisisagwe vizuri na kusababisa vitambi
5) Kunywa maji nusu saa baada ya kula
6) Usiku kula masaa mawili kabla ya kulala ili mpaka unaenda kulala chakula kiwe kimeshasagika tumboni
7) Acha kunywakunywa masoda bila mpangilio, kunywa mara mojamoja sio mbaya
8) Asubuhi kabla ya kufanya chochote kunywa glass moja au mbili za maji ya uvugu uvugu ukiweza weka kijiko kidogo cha asali au limao hii itakusaidia kupata choo ili kutoa uchafu uliokula jana usigande tumboni
9) Acha kula chips mara kwa mara kula tu siku mojamoja kwa hamu
10) Ukiweza fanya mazoezi ya kutembea kwa dk 20
11) Mshukuru Mungu kwa sala

NB: -Tupunguze kula hovyo hovyo jamani, utakuta mtu katoka kunywa chai yake halafu kapitia ofsn kwa mwenzie kakuta anakula mihogo yake kakukaribisha kiutani tayari ushachukua pande la muhogo unakula lanini si ushakunywa chai jamani!
-Au mtu asubuhi mwanamke unakunywa chai na chapati tatu jamani zote hizo ! chapati moja tu inakutosha labda waweza ongeza na yai 1 lakuchemsha au sambusa 1 ili upate na protin,
-Au uko zako barabarani kwenye foleni basi ndo utakuula zikipita koni za azam unayo ikipita mihogo ushanunua yani mpaka ufike umekula vitu ambavyo wala hukupangilia kula.
Nihayo tu kwa leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…