bampami
JF-Expert Member
- Nov 5, 2011
- 5,699
- 4,117
Jina sahihi la hali hii ni Nocturnal Penile Tumescence (NPT).Ni hali inayotokea karibia kwa kila mwanamme hasa vijana.Watu wengi huamini hutokana na kusisimka au kupanda kwa hisia za kufanya mapenzi jambo ambalo siyo sahihi sana kila muda.
SABABU ZAKE
Kuna sababu nyingi zinazopelekea kutokea kwa hali hii.Baadhi ya nadharia zinazotoa maelezo ya "kwanini" jambo hili hutokea zimeelezewa hapa chini
1.Kusisimka kwa mwili.
Japo macho yanakuwa yamefumba,mwili bado unaelewa na kutambua kila kitu kinachoendelea kwenye mazingira.Ndiyo maana hata ikitokea bahati mbaya (kwa walio oa) mwanamke akagusa au kuziona sehemu hizi za mwanamme uume husimama moja kwa moja.Huitwa upofu unaoona
2.Kubadilika kwa mzunguko wa homoni.
Homoni za kiume au testosterone huwapo nyingi sana wakati wa asubuhi baada ya kuamka kuliko kipindi kingine chochote cha siku.Bila kujali uwepo wa mwanamke,au kusisimuliwa kwa mwili sababu ya chanzo chochote kile,wingi huu wa homoni hutosha kabisa kuileta hali hii
3.Kupumzika kwa akili.
Wakati wa kufanya kazi ubongo huzalisha homoni za kuzuia uume kusimama,lakini wakati wa usingizi uzalishwaji wa homoni hizi hupungua.Ukichukua sababu hii pamoja na sababu zingine (hasa zile mbili za juu) ni dhahiri kuwa uwezekano wa kutokea kwa hali hiyo huwa ni mkubwa sana
HAJA NDOGO HAISABABISHI HALI HII.
Mtu anaweza kudhani kuwa haja ndogo (kukojoa) ya asubuhi ndiyo chanzo kikubwa cha kutokea kwa hali hii.Hiyo siyo kweli na hakuna uhusiano wowote kati yake
NANI HUPATWA NA HALI HII?
Wanaume wa rika zote hupatwa na hali hii.Wavulana wadogo hata (miaka 6-8) nao hupatwa na hali hii.Watu wazima na wazee pia hutokewa na hali hii japo hupungua kadri umri unavyozidi kuongezeka (uzee)
ISIPOTOKEA HUTOA ISHARA GANI?
Hali hii huonesha uimara wa mfumo wa mzunguko wa damu,pamoja na ule wa fahamu hasa unaoelekea kwenye uume.Pia ni ishara kuwa unao uwezo wa kusimamisha hasa nyakati unazokuwa na ufahamu kamili ili utimize haja za mwili wako.Ikiwa ulikuwa unapata kisha hali hii ikaacha,unaweza kuwa na shida hizi:
1.Uzito umeongezeka sana
2.Una shinikizo la damu
3.Una mafuta mengi mwilini
4.Una kisukari
5.Una mkazo&msongo wa mawazo.
NB
Hizi ni baadhi tu ya sababu japo zipo nyingi.
Credit to @afyainfo iG
Sent using Jamii Forums mobile app