SoC01 Afya ya akili na mabadiliko ya mitindo ya maisha

SoC01 Afya ya akili na mabadiliko ya mitindo ya maisha

Stories of Change - 2021 Competition

NG1

New Member
Joined
Jul 17, 2021
Posts
1
Reaction score
2
Habari zenu wapendwa.. Ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima wa afya na mapambano yakiendelea kwa kila mtu na nafasi yake.

Leo napenda tuzungumzie umuhimu wa afya ya akili hasa katika mabadiliko haya ya mitindo ya maisha, dunia ikiwa katika mabadiliko makubwa ya kitekinolojia, namna ya kuishi, vyakula, uhusiano, na hata namna ya kufikiri.

Kwanza kabisa ni vyema kujua kuwa kila badiliko lolote linapotekea katika mazingira yako lina adhili ubongo wako moja kwa moja yaweza kuwa athari chanya au hasi, kwasababu binadamu tunafanya kazi au tunatendaa matendo kutokana na mchakato wa taarifa tunazoingiza ubongoni mwetu, mchakato huo unatafsiriwa na kujenga dhana vichwani mwetu, ambayo dhana hiyo ujenga imani kuwa ni kweli au uongo.

Katika saikolojia ya Akili, Ubongo una sehemu mbili ambazo huusika zaidi katika ujengaji wa fikira, utafsiri wa mambo na ujengaji wa imani vichwani mwetu. Aina hizo ni
(i) consciousness (ufahamu awali)
(ii) subconsciousness (ufahamu pili)

Nitazungumzia moja baada ya nyingne kwa namna zinavyofanya kazi

I: Ufahamu awali (consciousness)

Huu ni ufahamu wa kwanza kabisaa wa mwanadamu ambayo ukua pale tu mwanadamu anapozaliwa, utumika kutafsiri mambo yote na kuhukumu kila kitu kama namna kujua majina ya watu, kujua unatakiwa kulala mda huu, bado hujakoga, kujukua hii ni hatari na mambo kama hayo. Ufahamu huu upokea kila kitu na kuchuja na unazima mtu anapolala.

II: Ufahamu pili (subconscious)

Hii ni aina ya pili ya ufahamu ambayo inajiendesha bila sisi kujua, ni ufahamu unaobeba imani leo tulizo nazo, namna yetu ya kufikiri mambo bila sisi kujua. Ufahamu huu unapokea taarifa kutoka ufahamu awali ( consciousness) na hauna chujio upokea kila kitu kutoka kwa ufahamu awali.

Mfano mtoto mdogo anapoambia kila siku kuwa wewe huwezi fanya jambo lolote, taarifa hizo zitapokelewa na ufahamu wali, afu utumwa katika ufahamu pili, huyo mtoto hata akiwa mkubwa akajua kuwa anaweza, daima atashidwa kwasababu ufahamu pili umejenga imani kuwa wewe uwezi jambo lolote.

Sasa kutokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha hasa tekinolojia, umefanya tunapokea taarifa nyingi sana vichwani mwetu kama watu kujionesha maisha yao Mitandaoni ambayo mengi siyo maisha halisi, unapoona kitu hicho Ubongo wako moja moja hautajua kwanza kuwa ni taarifa ya uongo au la, utapokea kwanza hizo taarifa kuwa maisha yako hivii na moja kwa moja utafsiri uhalisia wa maisha uliyoona na yako, baadaye inaletaa mgongano wa mawazo kwako na kuleta odhoofu kwako kuwa wewe ni mtu wa chini. Mwingilianao wa taarifa nyingii kazi hizi na mgongano huu uleta shida ya msongo wa mawazo baadaya muda "depression ".

Sasa kutokana hayo baada ya kujua namna bongo zetu zinavyoweza kujenga dhana ndani mwetu kwa taarifa mbalimbali na kutuletea madhara kama msongo wa mawazo, kushusha utashi wetu na hali ya kujiamini, je tunawezaje kuhifadhi Afya ya akili zetu ili kutunza utashi wetu, hali zetu za kujiiamini na kuhifadhi furaha zetu.?

I: JUA UHALISIA WA MAISHA.

Hii ni kwamaana kwamba, kufanikiwa maishani ni mchakato wa utumilifu wa malengo makubwa au madogo madogo yaliwekwa na mtu husika, unapotafakari hvyo na kukubali kubwa kila mtu atafanikiwa ikiwa tu atajenga malengo yake, unajengaa taarifa katika ubongo wako ambazo zinakujengea imani kwako mwenyewe, uleta utulivu wa akili na ubongo utakusaidia kutafakari malengo hayo.

2: JUA HAMNA CHENYE UKWELI KAMA WEWE HUJAKIRUHUSU KUWA KWELI

Kama nilivyoelezea huko juu, ufahamu wetu wa pili unahifadhi taarifa ambazo baadaye ujengeka kuwa sisi au imani zetu katika vitu mbalimbali. Kwahiyo kwa mfano kama tukipokea taarifa mbalimbali katika mitandao na kuona watu ambao kiumri tuko sawa wakionyesha maisha ya furaha, wakiwa sehemu nzuri au hata kuonyesha fedha hadhalani

Unaweza jengaa taarifa ya kuwa mimi ni mzembe, au sina bahati hiyo, kwahiyo kama utakubali taarifa hiyo kuwa kweli basi itakuwa kweli ila kama utakataa basi haita Kuwa kweli, kwaihiyo usibali taarifa hasi ikajenga dhana ya ukweli katika ubongo wako, utakusaidia kutuliza akili na kuupa ubongo nafasi ya kufikiri namna ya kwenda mbele badala ya kufikiri zile taarifa na kuzipanua.

3: ACHA KULINGANISHA UWEZO WAKO

Dhana hii imekuwa sumu kubwa sana kwa bongo zetu sisi vijana, kwa kulinganisha viwango vya mafanikio yao na yetu katika nyanja mbalimbali za maisha. Jambo hilii linajenga taarifa ya kutokuamini uwezo wako, na kuupa ubongo nguvu ya kufikiri uwezo wa mwenzako na kusahau kuwa Mungu aliumba kikamilivu " INDEPENDENTLY MIND" , kwahiyo unanyima ubongo wako kutenda mambo yake yale yanayoweza kukufaidisha wewe.
Kwahiyo kubali kwanza daima hatuwezi kuwa sawa mpka ulimwengu utakapo potea, chukua yale mema kuwa chachu, na kujengaa matamanio yako wewe mwenyew na kuwa imani kuwa unaweza yafikiaa., taarifa hizii zinaipa ubongo kufanya kile inachotakiwa kuafanya, yaani kukusaidia wewe kutimiza malengo yako.

5: TAWALA UNAYOWEZA USIYOWEZA ACHA.

Ubongo wetu utatua matatizo yale tu yaliyochini yake, kwamfano leo uambiwe tunakupa mwaka mmoja, tunahitaji ufikie utajiri wa billgate au MO kiuhalisia ni jambo gumi au haliwezekani kabisa kwa njia ya kawaida mbali na njia hasi. Kwahiyo unapopokea taarifa kutokana na dunia yetu ya sasa, chakata na ujue taarifa hiyo iko ndani uwezo wa ubongo wangu kwa sasa? Au itakuwa ndani uwezo wangu baadaye? Unapochakata kuchukua unayoweza kutawala na kuacha yale ambayo yako juu ya tawala za ubongo wako, unaupa ubongo wigo wa kutatua matatizo yako kwa weledi mkubwa sana.

Hivyo basi ndugu zangu, hizo ni njia chache zinazoweza kutusaidia kubadiliana na Utulivu wa akili zetu kwenye dunia yetu ya sasa yenye mambo mengi, ulio na kila mtu amefanikiwa mitandaoni, kila mtu ana familia bora, kila mtu anamahusiano yenye furaha mitandaoni.

Ndugu, Afya ya akili ndiyo tafasiri ya kwanza ya namna ya uendeshaji wa maisha yetu, ndiyo siraha yetu ya kwanza Mungu aliiyotupa ya kutatua matatizo yetu, kwahiyo linda sana afya yako ya akili katika ulimwenguu huu wa mabadiliko makubwa ya maisha.

ASANTENI SANA.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom