Afya ya Akili na Ujasiriamali

Afya ya Akili na Ujasiriamali

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu;

Leo nataka nizungumzie jambo tata sana ambalo wengi hukutana nalo ingawa hawajui kama ni tatizo.Jambo hili linahusu uhusiano uliopo kati ya afya yako ya akili na mafanikio yako ya kibiashara.

Kwanza nianze kwa kueleza kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati afya ya akili ya mtu na uwezo wake wa kufanikiwa katika maisha,na katika biashara.

Matatizo kama msongo, wasiwasi, hofu, mashaka, kutokujiamini, woga na mengineyo yana uhusiano mkubwa sana na uwezekano wa wewe kufanikiwa kibiashara.

Ni muhimu sana kuitazama afya yako ya akili kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha kwamba unaweza kufanikiwa katika biashara yako.

Tujadili kwa pamoja namna ambavyo matatizo yanayoathiri afya yetu ya akili yanavyoweza kuathiri uwezo wetu wa kibiashara na namna tunaweza kukabilina na matatizo hayo

Karibuni Tujadiliane
 
Back
Top Bottom