Daniel Adam Kidingija
New Member
- Jan 20, 2015
- 2
- 1
Watu wengi mtu anapokosea kufanya jambo, tunalaumu. Wachache hujiuliza amekutwa na nini. Jambo tusilofahamu ni kwamba, kila moja achukuliwe kwa upekee alionao. Haina maana tumpongeze mtu anaevunja taratibu nzuri katika jamii zetu.
Upekee hujengwa na sababu za kimazingira, na za kibaiolojia.
Ndugu msomaji, mtazame kijana Y:
Y alikuwa ni kijana mpole, mcha Mungu, asievunja sheria , na mchapa kazi haswa. Alipendwa na watu wengi sana. Ikiwa ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu, mwaka jana, Y aliwapoteza wazazi wake. Jamii iliomzunguka alimuambia akomae kwani mtoto wa kiume hapaswi kulia. Kwakua hakuwa na mtu ambae aliweza kuzungumza nae juu ya amani na furaha iliopotea na moyoni, basi alibeba jambo lile peke yake.
Siku zilivyozidi kwenda, utendaji kazi wake ofisini ulishuka na kupelekea kutoelewana na boss wake kila siku. Mahusiano yake yalivunjika kutokana na mabadiliko ya kitabia alionesha. Y aliamua kugeukia pombe na madawa akiamini itamsaidia kukwepa ukweli wa maumivu na kile kinachoendelea kwa wakati ule.
Watu wanaomzunguka walimyoshea vidole na kumuita mhuni, na mlevi.
Matumizi endelevu ya vilevi yalipelekea Y kufukuzwa kazi. Kiasi kidogo cha pesa alichokuwanacho alikitawanya katika kununua pombe na madawa kwani kila akiitazama jana yake na kesho yake haoni mwangaza wowote wa tumaini, mwili pia umeshajenga uraibu wa madawa na hakuna mtu ambae yupo tayari kumsaidia zaidi ya kumnyoshe kidole. Ata pale alipoishiwa pesa alijikuta amejiingiza katika utapeli na uporaji.
Mabadiliko haya ya tabia kwa Y ni muendelezo ya matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza ata kwa watu wengine. Kufeli kwetu kuchangua njia sahihi ya kupambana na mambo yanayotusibu huzalisha changamoto kubwa zaidi na kubadili tabia zetu. Vizazi na vizazi katika jamii zetu tumebebeshwa imani zinazozidi kandamiza afya zetu za akili. Pia, hakuna mtu anaekuwa mtu bora zaidi kwa kunyoshewa vidole. Ni wajibu wa kila moja wetu kuhakikisha anasimamia afya yake ya akili na ya watu wanaomzunguka.
Mwanasaikolojia;
Daniel Adam Kidingija
kidingijadaniel@gmail.com
0710161374