Nakumbuka Julai mwaka 2021 katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Tokyo, Japan mwanadada Simone Ariane Biles kutoka Marekani alizua gumzo bada ya kuamua kujitoa katika timu yake iliyokua imefikia fainali sita. Biles mshindi mara saba wa olimpiki aliamua kung’atuka kwa kile alichoelezea kuwa ni msongo wa mawazo ulioleta ugonjwa wa akili uliopelekea kuelekea kuathiri uwezo wake pamoja na wa timu katika michuano hiyo.
Salamu za pole na pongezi zilitoka kila upande. Pongezi haswa kwa kua muwazi, kujali afya yake na kutokua mbinafsi kwa kuweka maslahi ya kiushindani ya timu na taifa lake kwa ujumla. Biles aligusa mioyo ya wengi ,alitoa funzo kwa wanamichezo na dunia kuhusu afya ya akili. Biles atakumbukwa kama shujaa wa olimpiki za Tokyo 2020.
Tukio lile lilinionesha ni kiasi gani nchi zilizoendelea hususan Marekani zinavyolitambua na kulichukulia kwa uzito unaostahili jambo hili. Tofauti na huku kwetu Afrika, suala la afya ya akili aidha halitambuliki inavyopasa au halipewi uzito na kuangaliwa kwa jicho pana kama mojawapo kati ya changamoto nyingi zinazotukabili kufikia maendeleo na ustawi wa jamii zetu.
Hii ni kusema kwamba nchi nyingi zinazoendelea hususan za afrika haswa kusini mwa jangwa la Sahara hazijatambua kwa kiasi kikubwa suala hili la afya ya akili kama jambo linalotakiwa kutizamwa kwa umakini. Asilimia kubwa ya waafrika hawaelewi kuhusu magonjwa mengi ya akili, vyanzo, athari za kijamii na kiuchumi, na hata Serikali bado hazijakua tayari kulishughulikia ipasavyo janga hili.
Je afya ya akili ni nini? Kwa kifupi naweza kusema ni usawa au utimamu wa kihisia, kiakili na kitabia unaomuwezesha mtu kuhimili changamoto za maisha. Afya ya akili inachochea na kuchangia binadamu anachofikiri, anachohisi na anachotenda. Afya ya akili ina asilimia kubwa katika kuamua ni jinsi gani tunatatua changamoyo na matatizo yetu, inaathiri mahusiano yetu na wenzetu/watu wengine. Afya hii ni muhimu katika kila hatua ya maisha kutoka utoto mpaka uzeeni.
Jambo hili ni muhimu zaidi kwasababu inagusa sehemu nyingi kama sio kila sehemu ya maisha yetu. Kila kitu kinaanzia na afya ya akili na kinaathiri kila tunachofanya, mienendo yetu, tunachofikiri au kusema. Afya njema ya akili inaleta mahusiano mema, amani, kujithamini na uchapakazi
Ripoti ya shirika la afya (WHO) ya 2014 imeeleza baadhi ya vyanzo vya matatizo ya afya ya akili Africa. Mathalani, kutokua na usawa au uwiano wa kijamii au kiuchumi miongoni mwa wanajamii, umaskini, vita na migongano, udhalilishaji wa utotoni,maradhi ya muda mrefu,kutengwa, madeni, ukosefu wa ajira, uraibu wa madawa na pombe, mlundikano mijini, upweke n,k
Tanzania kama nchi nyingine za Africa bado tuna safari ndefu katika kukuza na kueneza elimu ya afya ya akili. Licha ya kupitishwa kwa sheria mbalimbali na sheria ya afya ya akili (Mental health act) ya mwaka 2008 ambayo lengo ni kuhakikisha haki na tiba bora, pamoja na matunzo na uangalizi vinatolewa na kupatikana kwa wenye magonjwa ya kiakili, bado sharia hiyo haijatosha kuleta uelewa, kuchochea mabadiliko nakuwezesha kiuchumi huduma za kutibu afya ya akili.
Sheria hii pamoja na sheria ya magonjwa ya akili (Mental disease act) licha ya kua ni za muda mrefu na zinahitaji mabadiliko ila pia kama walivyo watanzania wengi wakiwemo viongozi imeshindwa kuelezea aina tofauti za matatizo ya afya ya akili na kujumuisha aina moja, yaani ‘wazimu’.
Imeshindwa pia kuleta mazingira ya kuwepo mfumo bora wa elimu na uwezeshaji wa huduma ya tiba ya afya ya akili na si tu kanuni na uangalizi kwa waathirika wa magonjwa ya akili.
Ukiachilia ya kuwa elimu na uelewa mdogo lakini tafiti zinaonesha kua mifumo ya maisha na kupuuzia au kukataa uwepo wa tatizo ni changamoto kubwa kwa Tanzania. Huduma hafifu, kutokua na unafuu (gharama) pamoja na ugumu katika upatikanaji wa madawa ya afya ya akili. Imani potofu na miiko kwenye jamii zetu pia ni baadhi ya changamoto za huduma ya afya ya akili.
Dr Sylvia Kaaya mhadhiri kutoka chuo cha afya Muhimbili katika chapisho lake la mwaka 2014 aliloliita ‘Mental Health Service Systems in Tanzania’ yaani mifumo ya huduma ya afya ya jamii Tanzania pia ameelezea kua waathirika wa afya ya akili ni wengi kuliko hata inavyoripotiwa. Anaelezea kukubaliana na ripoti ile ya WHO ya mwaka 2014 iliyoonelea kujengwa kwa vituo zaidi vya afya ya akili.
Zaidi, WHO pia katika ripoti hiyo imetaja mambo muhimu ya kufanya ili kuboresha huduma za afya ya akili ikiwemo kuielimisha (educate) na kuihusisha jamii (involve), zikiwemo familia na wadau. Nyinginezo ni kuunganika kwa sekta mbalimbali za utoaji huduma ya afya katika kuelimisha na kutoa huduma pamoja na kuunga mkono tafiti nyingine zinazohusiana. Jambo jingine muhimu ni kutoa huduma na elimu za afya ya jamii katika vituo vya afya vya mwanzoni (primary) kama zahanati na hospitali ndogo.
Mambo mengine ambayo yanatakiwa kufanywa ili kuboresha huduma ya afya ya akili ni kutengeneza sera ya kitaifa ya afya ya akili, kutengeneza miradi, kutunga sheria mpya zilizoboreshwa. Sera na sheria hizo zilenge zaidi kuboresha programu na sheria kama zifuatazo.
Licha ya mambo hayo,ila hatua nyingine zinazotakiwa kuchukuliwa ni kuongeza rasilimali watu.
Rasilimali watu kama vile madaktari wabobezi wa afya ya akili (phychiatrists and phychologists)
kwa njia ya kutoa kipaumbele kwa kozi hizo vyuoni na kuboresha maslahi kwa wabobezi.

(1) Mradi wa afya ya akili wa 1980 ( National mental health programme ),
(2) 1999- 2009: Programu ya sera ya afya ya akili IoP and MoSWH ,
(3) Mental heath; a key component of the National health policy 2003 ( Afya ya akili; chachu ya sera ya afya ya Taifa 2003).
Pia, (4) 2004: Party to Framework convention for Tobacco Control (Tobacco WHO/AFRO) (Azimio la udhibiti wa tumbaku 2004) – iliyopitishwa 2007,
(5) 2006: Policy guidelines for mental health
care in Tanzania released ( Muongozo wa sera kwa afya ya akili Tanzania) ,
(6) 2008: Mental health act amendment to emphasize access to quality services and the rights of the mentality ill (Maboresho ya sheria ya afya ya jamii kusisitiza upatikanaji wa huduma bora na haki kwa
waathirika wa magonjwa ya akili).

Upvote
0