#COVID19 Afya ya akili yako ni muhimu katika kupambana na COVID-19

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Your browser is not able to display this video.

AFYA YA AKILI YAKO NI MUHIMU KATIKA KUPAMBANA NA #COVID19

Shirika la Afya Ulimwenguni linaeleza kuwa afya ya akili ni miongoni mwa jambo la msingi katika kupambana na janga la #coronavirus.

Inaelezwa kuwa athari za janga la Corona linaweza kuzalisha hisia za wasiwasi, woga na msongo wa mawazo miongoni mwa watu katika jamii hivyo kuathiri afya ya akili zao.

Ili kuilinda afya ya akili yako katika wakati huu unashauriwa kufanya mazoezi kila siku, kula vizuri, kuepuka ulevi wa kupindukia, kupata usingizi wa kutosha na kuwaona wataalamu wa afya pale unapohisi kupata na msongo wa mawazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…