Afya ya Dr. Ulimboka: Mwenye taarifa tujuze please!

Utotole

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
6,607
Reaction score
4,263
Habari wana JF,

Naamini kila mtu anakubaliana na mimi kuwa habari ya Dr. Ulimboka inaanza kufifia hapa jamvini. Hii ni kawaida kwa kila habari mpya, huvuma, hufifia na kisha hupotea kabisa, hasa zinapokuja taarifa nyingine moto zaidi kwa wakati huo. Pamoja na hayo, suala la afya ya huyu mtanzania halistahili kufifishwa ikizingatiwa kuwa hadi sasa hivi bado yupo kwenye matibabu, na 'tume' ya polisi 'inaendelea kufanya kazi'.

Ombi langu ni kwamba, kama ambavyo wadau, kupitia vyanzo vya uhakika wamekuwa wakitupa 'updates', basi waendelee kufanya hivyo ili tuendelee kuwa na taarifa juu ya mwenzetu huyu.

Nawasilisha.
 
Hakuna Taarifa yoyoe mpya mpaka sasa, tunachoomba kwa Mwenyeezi Mungu amponeshe Daktari wetu Kiongozi Wetu Mpendwa ampe afya na Uzima Mungu ampoeneshe Doctor Ulimboka Ameen.
 
Hali yake inazidi kuimalika kwani kwa sasa anaweza kula chakula mwenyewe, anafanya mazoezi mwenyewe kwa ujumla anaendelea vizuri sana.
Tuzidi Kumwombea zaidi for speedy recovery.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…