Afya ya gari

Kitukula

Member
Joined
Jul 2, 2022
Posts
6
Reaction score
5
Hivi mtu unapotaka kusafiri na gari yako (private car ) kipi unatakakiwa ukizingatie (service gani ni ya muhimu kwa safari ndefu )
 
Matairi, Ball Joints, Tie rod ends ziwe zipo vizuri bila kusahau kufanya service ya engine oil, oil filter, cabin filter etc..kama chuma ina zaidi ya 100,000 km badili timing belt, tensioner, bearing za mbele...etc...

Shukrani kaka
 
Hivi mtu unapotaka kusafiri na gari yako (private car ) kipi unatakakiwa ukizingatie (service gani ni ya muhimu kwa safari ndefu )View attachment 2284656
Kwa uzoefu wangu

Change oil. Weka oil quality nzuri ambayo viscosity haipotei hata wakati wa extreme engine temperature over extended time ie any full synthetic oil.

Angalia tairi za gari zisiwe zimezidi miaka minne tangu date of manufacturing, zisiwe zimeisha kashata yake na ziwe na temperature rating "A"

Hapa kwenye tairi pia zingatia uwingi wa upepo unaijaza usizidi PSI 35 na check pressure ya tairi regularly after every 400km hasa kama waendesha gari jua kali non stop. ( Jua during daytime molecules ndani ya tairi u expand na kuongeza pressure ya tairi kwasababu ya joto, so ni kucheki upepo mara kwa mara, au jaza hewa ya .... Ili kuzui unpredictable tire pressure increase)

Kwenye tairi pia hizi matari tambua yanatofautiana uwezo wa kuhimili speed..hizi tairi zina speed rating..sio tairi imeandika ina hilimi maximum speed 120kmh wewe unataka tembea 180kmh..so zingatia speed limit ya tairi yako.

Pia kwenye hizi tairi je umefunga rim za kichina au za juma au ni alloy lakini ni zakuja na Gari? Rim za udongo zina changamoto ya kupasuka hasa ukipika shimo la kueleweka..na issue huwa mbaya zaidi kama una low profile tyre.. so umakini wako barabarani hasa kwenye kufukia mashimo wa bumba kubwa uzingatie aina ya rim ulizo nazo, lakini pia profile ya tairi lako

Hakiksha cooling system ya engine yako ipo njema (yaan feni zipo poa, thermostat inafanya kazi vizuri, radiator ipo poa na haipotezi maji, pia hakikisha kifuniko cha radiator kipo vizuri(wengi huwa haangalii mfuniko wa radiator upo kwenye hali gani ila unaweza kukununulisha engine na hakikisha kama unabadili mfuniko wa radiator basi weka kama ulio toa-yaan kama una psi 1.1 weka huo huo.) Pia kwenye cooling system hakikisha temperature sensor yako nzima ili ikusaidie ku monitor temperature ya engine yako na tembea na maji hata lita tatu for emergency..

Hakikisha wheel alignment ipo sawa

Brake zako zote za mbele na nyuma zipo sawa (wengi husahau kuangalia brake za nyuma matokeo yake unakuta emergency brake zako hazifanyi kazi(jua gari inakuja na two brake system so system inayotumja hydraulic ikifeli unabaki na mechanical brake system ambayo ufanya kazi kwa matairi ya nyuma so akikisha brake shoes zako za nyuma zipo njema na parking brake/handbrake/footparking brake zipo vizuri.

Check brake rotors na brake drum pia kama zipo njema for heavy braking during any emergency or kama zimaweka kuhandle temperature ya extended braking application.

Check suspension kiujumla kama shock absorber zipo njema(shock absorber ndo huakikisha tairi za gari zina maintain ground contact for proper handling hiivni muhimu kwa usalama), check tie-rod, rack ends, ball joints,

Hakikisha headlights zako na tail lights zipo zafanya kazi hasa kusafiri kipindi hiki chenye ukungu (na kama gari ina fog lights na unasafiri kipindi chenye ukungu, basi weka fog light bulbs zenye mwanga kama wa halogen bulb-kama mwanga wa njano like for visibility.

Kua na tairi ya spea hakikisha ina upepo wa kutosha.

Pia hakikisha una vitu vya kukufanya uweze kusaidika wakati wa emergency, vitu kama jeki, spana ya kufungulia tairi, jumper cable, chain ya kuvutia Gari (inauzwa elfu kumi kama upo DSM).

Zingatia alama za barabarani na kua dereva mzuri wa defensive driving maana hizi highway zina so many reckless drivers. Pia kama ukiwa unahisi usingizi wakati wa driving don't force kwenda.

Maandalizi mema ya safari na safari njema.
 
I think kwenye safari ndefu vitu vinavyokula msoto zaidi kwenye gari ni matairi, bearing, suspension (shocks / joints / ends), brakes na oil.

Wadau wameelezea hapo juu kwa kina.

Kama gari haichemshi kwenye foleni za Dar ukiwa unatumia AC haitochemsha kwenye trip za highway kwasababu ile hewa inayopita kwenye radiator inaipooza zaidi engine kuliko ukiwa umesimama kwenye foleni.

Factor kubwa zaidi ni dereva. Uchovu utakuua. Usingizi utakuua. Ubishi utakuua. Ubabe utakuua. Uono hafifu utakuua. Kufosi kutakuua. Kubeti kutakuua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…