Afya ya mwanamke na uke

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
AFYA YA MWANAMKE NA UKE


Utafiti wa shirika la Afya Duniani (WHO) umebaini kwamba matatizo ya afya ya ndani ya mwanamke na maambukizi ya maradhi ya sehemu za siri kwa wanawake (gynocological disease) yanaongezeka kwa kasi kubwa sana duniani.

Takribani asilimia 85% ya wanawake wanasumbuliwa na matatizo hayo, kati ya hao asilimia
75% ni wanawake wa kiafrika na asilimia 60% kati ya hao hawajajitambua, na wengine
wanajitambua lakini wanapuuzia,au wanakosa wapi wapate msaada.
Sasa tuangalie undani wa mwanamke

Mwanamke kwa kawaida ana sura tatu (3). Je! Unazifahamu?

(i) Sura ya nje (Reception)
Wengi husema mwanamke reception; wanawake wengi hujitahidi kwa gharama zote
kuhakikisha reception yao au muonekano wao wa nje upo safi na salama muda wote.

(ii) Sura ya pili ya mwanamke nyumbani kwake
Muda wote mwanamke huwa anahakikisha nyumbani kwake panakuwa safi na wengine hata kuajiri watu, wanalipwa mshahara kazi yao ni kuhakikisha mazingira hayo ya nyumbani yanakuwa safi mara zote.

(iii) Sura ya tatu ya mwanamke ni sura yake ya ndani, uke wa mwanamke na kizazi
Hii ndiyo sehemu nyeti na muhimu sana kwa mwanamke na ndio sehemu imemfanya

mwanamke aitwe mwanamke na apewe heshima na wanaume na sehemu hiyo pia inatakiwa kuwa safi na kutazamwa muda wote. Lakini fikiria eneo hili wanawake wengi hawalithamini wala kulipa kipaumbele, na

ndio sababu imepelekea kusababisha matatizo makubwa ya kiafya katika eneo hilo.
Hebu jiulize swali; kama kweli kila siku unaweza kujicheki kwenye kioo mara kadhaa
kuhakikisha reception yako ya nje iko safi, na kila siku unafanya usafi nyumbani kwako
kuhakikisha mazingira ya nyumbani kwako ni safi na salama.

Je! Ni marangapi au ni lini umeweza kucheki afya yako ya ndani kwa mara ya mwisho au ni mara ngapi kwa mwaka unakwenda hospitali kucheki afya yako ya ndani? Au kucheki afya yako ya kizazi? Fahamu ya

kwamba maradhi yoyote kuanza taratibu na ukua kadri siku zinavyokwenda Utakubaliana na mimi kwamba eneo hilo muhimu na nyeti halijathaminiwa kwa wanawake walio wengi.
Utafiti umebaini baadhi ya vyanzo vikuu vinavyoweza kusababisha maambukizi ya maradhi ya sehemu za siri kwa wanawake wengi ni;

i) Vyoo vya kuchangia (public toilets)
Eneo hili ni hatari sana katika kusababisha maambukizi.kwa hiyo unahitaji kuwa
mwangalifu sana sehemu yoyote yenye mikusanyiko ya watu ambayo itawalazimu
(kuchangia vyoo kama; maofisini, maeneo ya soko, nyumba za ibada , sehemu za starehe,kwenye nyumba zetu tunakoishi nyumba za kupanga,vyuoni,mashuleni, nk...

(ii) Kutotumia maji safi na salama.
Maji mengi tunayotumia sio safi na salama mengi yana bacterias. Wengine eti hujazia maji ndani ya ndoo halafu huwekwa chooni. Maji hayo huhifadhi bacterias ni hatari sana.

(iii) Matumizi ya pads za hedhi ambazo sio salama.
Utafiti pia umebaini wanawake wengi wanapomaliza hedhi huanza kutibu fangasi, wengine hupata michubuko, miunguzo, miwasho na vipele sehemu za siri. Kwasababu tu wametumia pads ambazo sio salama.

(iv) Bacterias
Bacteria hupatikana sehemu mbalimbali na katika mazingira mbalimbali, unahitaji umakini katika matumizi ya vitu ktk sehemu za ndani.

Pia unapofua nguo yako ya ndani unashauriwa kupiga pasi kabla ya kuvaa. Swali, ni wanawake wangapi wanapiga pasi nguo zao za ndani kabla ya kuvaa?
Vyanzo ni vingi sana, suluhisho ni nini? "Kinga ni bora kuliko tiba " ni vyema ukafahamu
namna ya kumdhibiti muhalifu kabla hajaingia ndani kwako kuliko kupambana nae akiwa
tayari ndani ni ngumu. Ndo maana tumejitoa kuelimisha na kukushauri, jinsi ya kupambana na adui kabla na hata kama atakuwa ameingia kujua jinsi ya kumshinda.
 

Attachments

  • Fathima Kulsum Zohar Godabari.jpg
    30.7 KB · Views: 817
  • beautiful-women-india-actress-charm-woman-supermodel-best-90327.jpg
    83.3 KB · Views: 815
Asante MziziMkavu mimi huogopa sana ndoo zenye maji chooni kwa ajili ya kuchambia mh kweli ni hatari
 
Last edited by a moderator:
Somo zuri sana,ahsante
pia niongezee choice ya mavazi yetu wanawake nayo inachangia...
Unakuta mtu anaswampa siku nzima na skin jeans imembanaa na ni kipindi cha joto,unategemea nini:..
Skirts na magauni ni nzuri zaidi cz upepo unapita and u feel dry and comfortable..
Pia unaweza tumia pantliner au kubadilisha chupi during the day na usiku ulale bila pichuu..
 
Ngoja niprint hii itawafaa sana watu wangu wa karibu. Asante sana Dr MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
#mzizimkavu mbona umeweka picha yangu hapo bila ruksa yangu
Tatizo wengi wetu kwenda kucheki maswala ya afya ya uzazi hatujazoea mpaka tuanze kuumwaa hatuna mazoea ya kufanya check up mim mwenyewe sijawah tatizo hayo masaratan yanatisha mpaka tunaogopa kwenda hospitalin tunaona tufe kimya kimya tu

Swala usafii bado sana wanawake wengi wanavaa chupi mbichi hazijakauka vizurii!!!!


Kuhusu pad ni ipi iliyo salama kutumiaaa???kuna hizi HQ mi nazipenda zina kafriji pale kati kanapunga upepo sasa sijui ni salama! !!
 

hahha shoga kumbe hzi human cherish umezistukia eeeh,..pantliners zile yani ukivaa tu unasikia km kuna AC vile...mi nahs km ni chemicals ,natumiaga ila naogopa hadi basi
 
duh haya Dinazarde...so speechless! ukipata jibu nijuze ili siku nikifadhiliwa nami nirudishe fadhila angalau kwa kitu chenye friji kama hicho!
 
hahha shoga kumbe hzi human cherish umezistukia eeeh,..pantliners zile yani ukivaa tu unasikia km kuna AC vile...mi nahs km ni chemicals ,natumiaga ila naogopa hadi basi

Mi basi huaga nasikia raha kale kaubaridi ndio aje MziziMkavu atupashe kuhusu HQ pad
 
Last edited by a moderator:
Nimekupenda ndio maana nimeweka picha yako bibie.
 
Darsa zuri,shukran MziziMkavu.
Tatizo ni maumbile yetu nayo yalivyokaa,na hapo kwenye pads ndio dah! kila siku kuna toleo jipya ipi inafaa na ipi haifai mpaka ikutende ndio utaiepuka! Sijui turudi tu enzi za vitambaa??
Check up nayoo dah! yaani routine ya kwenda kumchanulia mtu akague cervix inafananaje uwiii! uso umeumbwa na haya bwana,nitaenda kama sijielewi elewi mengine Mungu atatunusuru.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…