Afya ya mwanangu inateteleka kisa mke wangu maziwa yanatoka kwa shida!

nunua baby formula (maziwa ya watoto) haraka iwezekanavyo
Angalizo: kama mama anamatatizo mengine ya kiafya hususani maambukizi ya VVU basi mkianza kumpa maziwa asinyonye tena, pia mwende mkapate maelezo sahihi zaidi kwa daktari haraka.
 
ahsante sana kiongoz!
 
Kesho jaribu kilo moja ya mbegu za maboga utanambia. Hata lile tatizo la wanaume hii ni tiba pia. Haina masharti. Ijaribu uone. Ukifanikiwa leta hapa mrejesho ili kuwasaidia wengine.
 
ahsante mkuu!
 
Kesho jaribu kilo moja ya mbegu za maboga utanambia. Hata lile tatizo la wanaume hii ni tiba pia. Haina masharti. Ijaribu uone. Ukifanikiwa leta hapa mrejesho ili kuwasaidia wengine.
ahsante kesho mida hii ntaleta mrejesho?
 
Nenda bucher lolote wambie wakupe mifupa ambayo haina nyama kabisa chemsha vizuri anywe hiyo supa utaniambia maziwa yatatoka mpka aone kero
 
Jaman naomben msaada! mwanangu ana wiki mbili ananyonya kwa shida kisa mke wangu mziwa hayatoki inavyotakiwa! ni nini sababu? na tufanyaje ili kutibu tatizo?
Usinunue zile za kwenye pakiti, ni ghali sana. Nenda duka la nafaka, Pima kwa kilo. Kwa Dar hadi morogoro bei ni nafuu, elf 3 kwa kilo, huko kanda ya ziwa zina bei sana, elf 15-20 kwa kilo. Iringa na Mbeya zipo chini pia. Moshi na Arusha sijawahiziona
 
we mwanamke ni mama mzuriii sana! kwa coment yako tu moja nimekuelewa sema umeolewa na mimi nimeoa! abarikiwe sana aliyekuoa!
 
Npo mbeya ntazifuatilia mkuu! nimekukubali kwa ushaur mzuri!
 
Wakati ukitafuta formula kwaajili ya kuokoa jahazi kwa mtoto.. Mpe mama uji mix unga wa maboga,ale nyanya chungu zile za kienyeji.. Pia ale vitu vya moto hasa vimiminika. Japo kuna wanawake wengi wameumbwa hivyo maziwa kutoka kidogo. Pia arelax asiwe na stress au kama chuchu zinauma mtoto akinyonya mwende hospitali
 
Aisee, yaani mwanangu asipate maziwa ya kutosha kisa kuhofia kulala, acha yafike miguuni tu kwakweli[emoji30] [emoji30]
 
Mama atumie uji wenye pilipili manga na mbegu za maboga naskia inasaidia ila pia asicheze mbali na supu supu izi,mitorii
 
Pole ila kwa ushaur uliitolewa na wadau hapa i hope tatizo lako limepata muarobaini
 
comment yako imenifanya nikuone wa pekee sana,hawa wadada form four leavers Sana shida saba,yuko tayar mtoto afya itetereke kwa kutonyonya ipasavyo wakizingatia matiti yasilale,aiseee nilizama kwa CO nikiwa nimechafukwa nikaomba ruhusa nikaeleweka nikapata siku 21,pale home ilibid niwe taahira kidogo kueleweka,mbele ya mama mkwe nilipageuza pale home ni depo,nilipoeleweka kuwa Dogo nataka anyonye maziwa ya mama kwa gharama na hali yoyote nilishangaa maziwa yamekuwa mengi kwa mama bila kutumia dawa yoyote ile,hongera sana rafiki yangu,unajielewa ad nimekupenda asee
 
Kuna maziwa ya kopo mbadala flani hivi yanauzwa 72,000/= kwa kopo yanatoka UK yana nutrients zote mtoto anazohitaji, ni mkataba mtoto afya kama yote [emoji1430]
 
Jaman naomben msaada! mwanangu ana wiki mbili ananyonya kwa shida kisa mke wangu mziwa hayatoki inavyotakiwa! ni nini sababu? na tufanyaje ili kutibu tatizo?
Atumie S26 maziwa ya kopo
 
Ukishindwa vyoooote, kuna kitu inaitwa UWATU, mchanganyie kwenye chai au uji.....ulete mrejesho.
Msalimie sana uncle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…