Afya ya 'mzee small' yazidi kudhohofika...serikali yaombwa kumsaidia haraka..!!

Afya ya 'mzee small' yazidi kudhohofika...serikali yaombwa kumsaidia haraka..!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

ANAFAHAMIKA zaidi kwa jina la Mzee Small, lakini jina lake halisi ni Small Wangamba.

Ana sifa nyingi, lakini iliyo kubwa ni ucheshi, uchangamfu, ukarimu na kila aina ya bashasha. Hata hivyo kwa sasa hali yake ni tofauti, mambo mengi yamebadilika.
Sipati shida kumpata pale nilipokusudia kumfikia na hata ninapofika nyumbani kwake katika banda la vyumba viwili ambavyo vimemalizwa kujengwa hivi karibuni, napokewa na msichana anayenikaribisha katika kiti nje ya kibanda hicho.

Ujumbe unapelekwa ndani kwa Mzee Small kuwa ana mgeni na dakika 20 baadaye mlango unafunguliwa, anachomoza mtu ambaye sipati taabu kumfahamu kuwa ni Mzee Small, mwigizaji nguli ambaye maradhi yamemkalisha kitako.

Anachechemea huku mkono wa kushoto akiwa ameufumbata kwapani, uso umekumbwa na maumivu yanayoshindana na tabasamu hafifu analojaribu kulitoa.

Hali hiyo inaakisi wimbo mmoja wa Shakila Abdallah ‘Bi. Shakila’ wenye mashairi ‘Macho yanacheka moyo unalia’. Kimsingi Mzee Small anaumwa ingawa anajaribu kutabasamu, kinachoonekana katika paji lake la uso ni tofauti na tabasamu hafifu analojaribu kulitoa pale macho yetu yanapogongana na wakati wa mazungumzo anabainisha kinachomsibu.

“Sipo vizuri, naumwa. Kwa sasa inawezekana ikaonekana kama nina nafuu kidogo, lakini naumwa,” anasema baada ya kunikaribisha katika chumba kimoja ambacho anakimiliki na mkewe.

Chanzo cha tatizo


Anasema tatizo lake lilimuanza Mei mwaka jana baada ya kurudi kutoka Mwanza alikokuwa na kazi ya kutumbuiza katika tamasha la kupambana na mauaji ya Albino. Tamasha hilo liliratibiwa na Kituo cha Under The Same Sun .


“Nilitoka Uwanja wa Ndege (Dar es Salaam) na kufika hapa nyumbani, nikaingia chooni moja kwa moja. Lakini wakati natoka, nikadondoka. Nilipojitahidi kunyanyuka haikuwezekana hivyo nikabebwa hadi chumbani,” anasema.


Anasema akiwa chumbani alijaribu kujinyanyua akajikuta anadondoka tena, hivyo akawahishwa hospitali moja jirani na nafuu haikupatikana.

Ikalazimika apelekwe Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam ambako alilazwa siku tatu kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Anasema alikaa Muhimbili mwezi mzima bila matibabu ya maana na baadaye akaruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupewa dawa chache. Lakini akiwa tayari amepooza mkono na mguu, vyote upande wa kushoto.
Mzee Small anasema matibabu katika hospitali hiyo hayakuwa ya kueleweka na pengine kwa kuwa hakuwa na fedha za kutosha basi hakuna aliyemjali.
“Baada ya kurudi nyumbani niliamua kuhangaika na mambo ya ‘Kiswahili’ (waganga wa jadi) kwani niliambiwa kuwa ule ni ushirikina kwani kuna mtu alileta kitu na kukichimbia mlangoni kwangu na kingine nje ya choo, hivyo nikaingia katika tiba mpya,” anasema.

Anabainisha kuwa ‘mafundi’ wengi walimtembelea nyumbani kwake na kila aliyekuja alimweleza kuwa sasa tatizo lake limeisha na kumpa dawa zikiwamo za kuchua. Hata hivyo anasema hakukuwa na jipya zaidi ya kumaliza tatizo la kizunguzungu lililokuwa likimsumbua pia.

“Kweli kizunguzungu kilichokuwa kinanikabili kiliisha, lakini bado mguu na mkono vimebaki vimepooza hadi sasa,” anasema na kuongeza kuwa mbaya zaidi waganga hao kila mmoja kwa wakati wake walihitaji fedha.

Anasema wa mwanzo alimwambia akitoa Sh 300,000 atapona, aliyefuata alihitaji Sh 200,000 fedha ambazo

alijitahidi kuzitoa baada ya kuuza sehemu ya shamba lake eneo la Kiparang’anda, lakini hakupata nafuu.
Anasema kuna ‘Fundi’ mmojawapo alitoka Kigoma na hivyo akalazimika kumpatia hadi chumba cha kulala,

lakini ‘fundi’ huyo alitoweka baada ya mgonjwa wake mwingine aliyekuwa eneo la Segerea, Dar es Salaam kufariki wakati anahudumiwa na ‘fundi’ huyo.

“Kuna mgonjwa alienda siku ya kwanza akamchukulia dawa zake, akarudi tena siku ya pili, alipofika siku ya tatu akakuta maturubai na watu wamejaa. Yule mganga akageuza njia na hakurudi tena huko na aliniaga kuwa anarudi kwao,” anasema Mzee Small.

Anasema tiba za mganga huyo zilimtia shaka na ilifika wakati alizikataa kabisa.

“Nilimwambia mimi basi inatosha ila kama kuishi katika mazingira haya wee kaa tu ila kwa tiba zako mimi basi tena, lakini mganga huyo aliendelea kung’ang’aniza hadi tukio hilo la Segerea ambalo lilimkimbiza mjini,” anasema.

Mzee Small anasema amelazimika kuuza shamba ili aendelee na matibabu na kumalizia sehemu ya kibanda chake anachoishi sasa.
Kuhusu tatizo lake, anasema mkono uliopooza sasa unaonyesha kuanza kutengana na bega.

“Sijui hasa ni nini, nina wasiwasi huenda kuna tatizo jipya linajitengeneza. Yaani nimebaki kumwomba Mungu anisaidie kuninusuru na ugonjwa huu,” anasema kwa masikitiko makubwa.
“Nipo njiapanda na sielewi tatizo ni nini. Kibaya zaidi sasa hata ndugu zangu wamenitenga. Hakuna hata mmoja ambaye anashughulika na afya yangu wala kujaribu kunijulia hali

Anasema siku za awali ndugu hao walijitokeza na kumjulia hali, lakini kadiri siku zilivyoenda wakaanza kukacha.

“Ndugu pekee aliyebaki sasa ni mke wangu, vyombo vya habari na baadhi ya mashabiki ambao hufika hapa,” anasema.

Mzee Small ambaye ametamba katika vikundi mbalimbali vya maigizo na vichekesho na kujizolea umaarufu mkubwa ambao ulimwezesha kupata mikataba na kampuni kadhaa mbali ya maonyesho ya jukwaani, anasema mambo yake sasa si shwari kabisa.




AFYA YA 'MZEE SMALL' YAZIDI KUDHOHOFIKA...SERIKALI YAOMBWA KUMSAIDIA HARAKA..!! - GUMZO LA JIJI
 
Pole baba. Sijui lini tutajifunza kuibiwa na 'mafundi'.
Hizo laki alizowapa mafundi wakati akiwa muhimbili si zingemsaidia?

Serikali yetu sikivu, itamsaidia bwana.
 
Mwenyezimungu amfanyie wepesi. Malofa hawawezi saidiwa na serikali. Wavuta unga na bangi wakiji-overdose serikali haraka haraka inawasaidia. Shame!
 
Kwa kufahamu kwangu huyu Mzee Small amepatwa na Ugonjwa wa Kiharusi yaani Stroke.

Kiharusi ni ugonjwa unaoleta kupooza unaosababishwa na matatizo kwenye mishipa ya damu inayolisha ubongo.

Katika tiba kiharusi (stroke) inamaanisha upotevu wa uwezo wa ubongo unaoendelea haraka. Sababu yake ni

tatizo katika mishipa ya damu inayopeleka damu kwenda ubongo. Matatizo haya ni ama kuzibwa au kupasuka

kwa mishipa ya damu. Seli za ubongo hufa haraka zisipopata oksijeni na lishe ya kawaida na yote haya hufika kwa

njia ya damu.


Kiharusi ni hali ya dharura inaweza kutibiwa kama tatizo latambuliwa na kutibiwa haraka. Lisipotibiwa

husababisha viwango mbalimbali vya kipooza mwilini.


Shinikizo la juu la damu, usukari, chakula chenye mafuta mengi au kuvuta kwa sigara huongeza hatari ya kushikwa

na kiharusi.

FAHAMU KINACHOSABABISHA UGONJWA WA KIHARUSI


UKISEMA MTU FILANI ANA UGONJWA WA KIHARUSI MAANA YAKE KITAALAMU VIUNGO

VYAKE VIMEPATA GANZI AU KITAALAMU HUITWA STROKE NA KUSABABISHA MWILI

KUTOJIWEZA AU KWA MANENO MENGINE NI KUWA MTU HUYO HULEMAA KATIKA KILE

KIUNGO KILICHOKUMBWA NA UGONJWA HUO.

DALILI ZA MTU KUUGUA KIHARUSI HUTOKEA GHAFLA NA KUTOWEKA GHAFLA.

KINACHASABABISHA KIHARUSI;-

WATU WENGI WANGEPENDA KUJUA KINACHOSABABISHA MTU KUPATA KIHARUSI.

KINACHOSABABISHA NI PALE ENEO FULANI LA UBONGO LINAPOKOSA DAMU KWA SAA24 AMA

ZAIDI NA NDIO MAANA WAZUNGU WAKAITA UGONJWA HUU BRAIN ATTACK AU STROKE.

MTU PIA ANAWEZA KUPATWA NA KIHARUSI KAMA ITATOKEA KUNA KIZUIZI KATIKA

MWILI WAKE KINACHOFANYA DAMU ISISAFIRI KATIKA MISHIPA YAKE HIVYO KUSABABISHA

KUPASUKA BAADHI YA NYAMA MUHIMU KWENYE UBONGO AMBAZO KITAALAMU HUITWA

VITAL BRAIN TISSUE.

HALI HII IKITOKEA INAKUWA HAINA TAFAUTI SANA NA INAPOTOKEA MISHIPA YA ARTERI

KATIKA MWILI INAPOPASUKA NA MTU HUYO KUKUMBWA GHAFLA NA UGONJWA WA MOYO

AMBAO KITAALAMU HUITWA HEART ATTACK.

AINA MBILI ZA KIHARUSI:


HALI HIYO INAWEZA KUTOKEA KWA KUSABABISHWA NA KITU KINACHOITWA

THROMBOSIS AMBAPO DAMU HUGANDA KWENYE MSHIPA MKUBWA WA ARTERI, MSHIPA

HUU NI MUHIMU SANA KATIKA MWILI WA BINADAMU KWA KUWA NDIO UNAOSAFIRISHA

DAMU KUPELEKA KATIKA UBONGO.

HALI HIYO INAWEZA PIA KUSABABISHA VIMIRIJA VIDOGODOGO VINAVYOPELEKA DAMU

KATIKA UBONGO KUZIBA NA KITENDO HICHO WATAALAMU WA AFYA AU TIBA HUWA

WANAKIITA LACUNAR STROKE.

HATA HIVYO, AINA HII YA KIHARUSI (LACUNAR STROKE) WATAALAMU WAMEGUNDUA

KUWA HAINA MADHARA MAKUBWA SANA KWA MTU AMBAYE AMEKUMBWA NAYO.

KIHARUSI CHA HAEMORRHAGE

MTU HUKUMBWA NA KIHARUSI HIKI KIITWACHO KITAALAMU HAEMORRHAGE BAADA

YA KUPASUKA MSHIPA KWENYE UBONGO NA KUSABABISHA DAMU KUVUJA YAANI

HAEMORRHAGE.

HALI HII INAPOTOKEA NI KWAMBA DAMU ILIYOVUJA HUKANDAMIZA UBONGO HALI

INAYOSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA KWENYE UBONGO KWA KUWA UBONGO NI KIUNGO

LAINI KATIKA MWILI.

KITENDO CHA DAMU HIYO KUGANDA KATIKA UBONGO LICHA YA KUHARIBU ENEO HILO

KATIKA FUVU LA KICHWA, KIASABABISHA HUARIBIFU WA CHEMBE HAI KWENYE UBONGO

HIVYO KUHATARISHA MAISHA YA MGONJWA NA HALI HIYO UITWA KITAALAMU

CEREBRAL/HAEMORRHAGE AMBAPO UVUJAJI WA DAMU UNAFANYIKA NDANI YA UBONGO.

MTU PIA ANAWEZA KUKUMBWA NA KIHARUSI BAADA YA KUPASUKA MSHIPA WA

DAMU AMBAO UNAZUNGUKA UBONGO NA HALI HIYO INAPOTOKEA KITAALAMU KUWA NI

SABARACHINDID.

USHAURI NA TIBA

MWENYE KIHARUSI AWAHISHWE HOSPITALI NA HAKIKISHA KICHWA CHAKE

KINAINULIWA KIDOGO ILI MATE YASIWEZE KUMPALIA

KIHARUSI CHA ISCHAEMIA

KIHARUSI KIITWACHO ISCHAEMIA. AINA HII YA KIHARUSI HUTOKEA KUTOKANA NA

MSHIPA UITWAO KITAALAMU ARTERI UNAPOGANDA DAMU.

HALI HIYO IKITOKEA DAMU INASHINDWA KUSAFIRI HADI KWENYE UBONGO, HIVYO

MTU KUKUMBWA NA KIHARUSI KIITWACHO ISCHAEMIA NENO AMBALO KWA KIGIRIKI MAANA

AYAKE NI KUZUIA DAMU.
 
serikali siyo ya kusaidia wasanii tu bali watanzania wote. pesa za sanaa alipeleka wap adi achangiwe sasa.
 
Back
Top Bottom