SoC02 Afya ya ubongo

Stories of Change - 2022 Competition

Makisetu

New Member
Joined
Sep 4, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Nawaza vidonge hamsini vitatosha? Ama nichukue kamba nijining’inize ama ninunue sumu ya panya na vidonge vya usingizi nipotelee usingizini? Nimechoshwa na msongo wa mawazo na moyo wangu kupapatika. Natafakari mambo mengi sana ya dunia hii yanayo tetemesha nafsi yangu.

Baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari wazazi wangu walishindwa kunilipia ada ya elimu ya juu zaidi na kwa bahati mbaya sikufanikiwa kupata mkopo unaotolewa na Serikali. Ghafula ndoto zangu za mafanikio ziliyoyoma na nuru ya kuiokoa familia yangu na umsikini ikaondoka. Ili nibidi nirudi kijijini kwetu Miburani wilaya ya Mafia ambapo niliendelea kuishi na wazazi wangu nikijishughulisha na shughuli za uvuvi ambazo ndo kazi ambayo hata babu yangu alikuwa anaifanya.

Kutokana na kwamba nilikuwa na elimu japo ni ya sekondari nilitamani kufanya uvuvi wa kisasa zaidi na kutumia vifaa vya kisasa nikiamini kwamba tukiweza kuvua samaki wengi zaidi tutaweza kuuza zaidi na kuongeza kipato. Nilijaribu kufanya utafiti wa namna ya kupata vifaa vya kisasa ila bei zilikuwa ghali sana na pesa ambayo ningeweza kuitafuta mimi pamoja na Baba yangu isingetosha kabisa kununua vifaa hivyo.

Basi hali ya maisha ilizidi kuwa duni nakumbuka kuna Msichana nilimpenda sana tulisoma wote kidato cha tano na sita ni msichana ambaye alikuwa mzuri sana kama ua la waridi lililotiwa mbolea ya samadi na nilitegemea ningemuoa na kufanya maisha pamoja hapo mbeleni, kila nikimkumbuka moyo wangu unazizima nawaza hata nikimtafuta atakubali kuwa na mimi na maisha yangu haya duni? Yale mambo yote ambayo nilimwambia nitayafanya nitakapo maliza elimu ya juu na kupata kazi nzuri siwezi kuyafanya tena. Nabaki na masikitiko makubwa kila nikitafakari haya.

Miaka mingi ikasonga na umri wangu ukazidi kuwa mkubwa, Baba akaanza kuniuliza Atlasi ni lini utaoa ni lini utaniletea wajukuu!? sikutamani kuoa kulingana na maisha duni tuliyonayo na nikijaribu kumueleza Baba sababu zangu za kuchelewa kuoa aliniambia Yeye na Mama walioana akiwa anafanyakazi hii hii ya uvuvi na ameweza kutulea hivyo hivyo mpaka leo hii tu watu wazima kwanini mimi nakuwa mbishi kuoa?Baadae Baba aliamua kuniozesha binti wa rafiki yake kwa kuwa hakuwa chaguo la moyo wangu sikuwa na mapenzi nae niliishi nae tu kwa sababu ni wajibu na utaratibu wa maisha lakini akilini mwangu siku zote nilimuwaza na kumkumbuka yule wa zamani niliyempenda kwa dhati.

Kwa kuwa mke wangu alikuwa binti alieishia darasa la saba alikuwa hana elimu yoyote ambayo ingeweza kumsaidia kufuata uzazi wa mpango na mimi nilikuwa nimeshakata tamaa ninaishi tu ilimradi siku zipite za hapa duniani, tukawa na watoto wengi ambao wamepishana mwaka mmoja kwa mwaka na nusu. Hali ya maisha ilizidi kuwa ngumu, samaki mmoja au wawili hawatoshi kwenye familia yangu. Nashindwa kuwalisha vizuri watoto wangu na kuwavesha vyema, nikageukia kwenye pombe za kienyeji, pesa kidogo ninayoipata nakimbilia kwenye pombe.

Daaah!! kwa kweli Nimechoka najiona kama sifai, sifai kuishi hapa duniani. Mini ni Baba wa aina gani ninaeshindwa majukumu yangu, nashindwa kuitunza familia yangu, sina pesa na kidogo ninayoipata nimeshajiingiza kwenye unywaji pombe!! Nawaza labda nijipumzishe tu ya nini kuteseka hivi. Nikiwa kwenye dimbwi zito la mawazo natafakari dhiki zote zilizonikumba kwa miaka mingi sasa, na labda nichague vidonge,sumu ya panya ama kamba ili nipumzike na dhiki hizi nimekosa tumaini kabisa nasitushwa na sauti ya mtoto wangu, “Baba mbona unalia?” napatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuwaona watoto wangu wote wananishangaa kwa macho ya mshangao uliombatana na huzuni hawaelewi kwanini Baba yao anatokwa na machozi naanguka chini na kuzimia.

Nakuja kuzinduka niko hospitalini nimetundikiwa dripu ya maji na Mke wangu amekaa pembeni yangu kimya namuuliza “imekuwaje” ananijibu “umezimia kwa masaa matatu sasa” kimya kinatawala katikati yetu kila mtu anatafakari la kwake ndipo dokta anakuja kuniona na kuniuliza kama nakumbuka ilikuwaje mpaka nikazimia, nilipomueleza akaniambia niendelee tu kupumzika kesho yake nitaonana na daktari wa afya ya Ubongo.
Kesho yake Daktari wa afya ya Ubongo aliagiza nipelekwe ofisini kwake, nilipofika daktari alinikaribisha vizuri sana;

Daktari: “Pole sana, unajisikiaje?”
Atlasi: “ Napata shida ya kupumua,mpapatiko wa moyo,natokwa na jasho jingi,nahisi kukabwa kuna mda Napata maumivu ya tumbo,chevuchevu, pia kuzirai na nimekata tama kabisa ya maisha”

Daktari: “ Pole sana, hizi ni dalili za Ugonjwa wa Wasi wasi. Kuna aina tano za ugonjwa wa Wasiwasi ambazo ni 1) Wasi wasi wa kijumla (Generalised anxety disorder) 2) Woga maalumu ( specific phobia) 3) Wasiwasi wa Baadaye(Post traumatic stress disorder) 4) Ugonjwa wa kujilazimisha(Obsessive-compulsive disorder) 5) Woga wa watu(Social phobia).Sasa hiii hali umeanza kuisikia lini?”

Atlasi: “ Nina muda mrefu sasa ila mara nyingi hunitokea nikiwa kwenye mawazo mengi?”
Daktari: “ Unawaza nini Atlasi kiasi hicho mpaka kufikia kuzimia?”
Atlasi: “ Maisha tu Daktari”. Nikajibu kinyonge
Daktari: “ Basi wewe utakuwa umepata ugonjwa wa Wasi wasi wa Kijumla( Generalised anxiety disorder) Ugonjwa huu huwa na dalili za kubabaika na jambo lolote maishani kama afya, jamii,marafiki,hela ama kazi. Watu walioathiriwa hujibabaisha kuhusu hatari inayoweza kuwajia wao au wapendwa waona kubabaika huja na huzuni na pia hali ya kushtuka.

Atlasi: “Ugonjwa huu unasababishwa na nini Dokta?”
Daktari: “ kuna sababu za kurithiana, sababu za kikemikali na sababu za tabia”. “ Na nitakutibu kwa njia zifuatazo kwanza kabisa ninakuandikia dawa zinazopunguza huzuni, dawa ya wasi wasi inayolenga matibabu ya akili na Matibabu ya kisaikolojia ya kurekebisha tabia (Cognitive Behavioural Therapy CBT) hizi zinalenga kubadilisha mawazo, tabia na imani zinzoleta wasiwasi.Pia fanya mazoezi, kunywa maji ya kutosha na chakula bora. Afya ya Akili na Mwili vyote ni vya muhimu.”

Baada ya miezi sita ya kumeza Dawa,Therapy na mazoezi ya mwili na kula chakula bora; nilirudi katika hali yangu ya kawaida. Pia Daktari aliweza kunikutanisha na rafiki yake alienipakazi kwenye shamba lake lenye mabwawa ya samaki nisimamie mradi wake. Kwa sasa matumaini yamerudi na Bosi wangu ameniahidi mambo mengi mazuri kwa sababu ya juhudi kubwa ya kazi anayoiona ninaifanya katika shamba lake, nayafurahia maisha na najitahidi kuijali familia yangu.

MWISHO
UKIONA MTU ANADALILI ZA UGONJWA WA WASI WASI MSHAURI AENDE KWENYE KITUO CHA AFYA YA UBONGO KWA MATIBABU ZAIDI. VIFO VYA KUJITAKIA VINAZUILIKA.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…