hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,544
Salaam.
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusu afya ya kiongozi mkuu wa nchi Mh. Raisi Jakaya Mrisho Kikwete, kupata matibabu ya tezi dume nchini Marekani.
Binafsi nilishangazwa na taarifa hizi hasa ukizingatia madaktari wa taaluma husika wapo nchini wengi, wenye uzoefu, wenye taaluma kubwa tu.
Miaka miwili hivi iliyopita Serikali ilisema haina kipaumbele cha kusomesha madaktari bingwa, ambao katika dunia ya leo ndiyo wenye kuhitajika zaidi na wengi wao hujisomesha kwa gharama zao lakini najiuliza, Je wanataaluma wetu waliobahatika kusomeshwa na serikali wanapopaswa kutoa mchango wao kwa taifa kisha kutothaminiwa/kudharauliwa n.k inaleta mantiki?
Tafsiri ninayoipata ni kuwa Serikali haina mpango mahsusi wa afya kwa wananachi wake? Kwa mfano huu wa Mh. Raisi JMK kupata matibabu yake yanayoweza kufanyika hapa nyumbani gharama hizi nani mwenye kulipia, jopo zima la watu aliosafiri nao hugharamiwa na nani?
Hapa nisieleweke vibaya, yeye kama binadamu wengine ana utashi wa kuchagua matibabu yake yawe wapi, ikiwa tu anamudu hivyo(na hata hili anamudu), lakini tukumbuke kwa upasuaji mkubwa na mdogo ni vizuri kufanya kliniki ya maendeleo, je bado itamlazimu Raisi kwenda nchini Marekani kwa ajili ya hilo? Gharama hizi ni juu ya nani? Tafsiri gani inaonekana kwa madaktari wetu nchini na nchi jirani pia? Daktari wa Raisi, washauri wake hawakuona hili, au pengine kuna sababu kubwa tusizozijua juu ya afya yake.
Binafsi ni maswali ninayokosa majibu yake.