Afya yako ni kitu muhimu kuliko chochote

Afya yako ni kitu muhimu kuliko chochote

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
1,595
Reaction score
451
Unaweza kuwa na kila kitu hapa duniani lakini kama afya yako ni mgogoro basi ujue una tatizo... mfano huu unaweza ukaufanyia kazi au ukaachana nao sijakulazimisha......... nilijikuta nina uzito wa kilo 100, nilijihoji kilo mia nimezipataje nikagundua kwamba ni kwa sababu ya kula kula yangu .... nikajiuliza nakula nini nikagundua kwamba asubuhi napata breakfast yenye mikate silesi 4 za blue band na jam sosaji 2 kikombe kikubwa cha chai ya maziwa ya unga ya cowbell na maji lita moja.... mchana ninakwenda kula kwa hawa mama ntilie ambao kuna wanaojitahidi kuandaa misosi ya nguvu misosi yao inanifanya niwe nakula ugali wa dona na mboga zao zipatazo 5 au zaidi yaani dagaa, nyama, kipande cha samaki, mboga za majani, mlenda na maharage ....(menu hii inaweza kwenda na chapati tatu kwa mboga hizo pia) lazia nipate maji chupa ya lita moja ya masafi ... baada ya hapo jioni kama kawaida nikifika mtaani kwenye mabaa nachoma nyama ya mbuzi ya book 4 au kongoro lenye ndizi au nusu kuku, au kiti mo.. nusu kg... hapo lazima nipate na cha kushushia vibia kama vitatu au vinne ..... baada ya hapo naelekea home na kukutana na nahotpoti ya wife na hapo pia najipinda na kisha kuoga na kwenda kulala.... hayo ni maisha ya kula kula ambayo nimekuwa nayo bila kujitambua kuwa natafuta majanga.... ghafla nilijikuta napumua kwa shida, nahitaji hewa safi kila wakati .... nikitembea mwendo mrefu sijisikii vizuri lakini moyo hauendi mbio .... nilikimbilia hospitali na kufanyiwa vipimo vyote lakini Mungu ni mwema nilionekana sina tatizo la sukari ukimwi na presha lakini nikashauriwa nipunguze uzito na kuambiwa kwamba niache kula vitu vyenye mafuta na chumvi ile ya kuongeza na kupunguza chumvi kabisa .... nilichofanya niliamua kushinda kutwa kwa matunda na maji mengi .... niliambiwa kufanya utafiti wa chapati tunazo kula yaani kuchukua chapati moja na kuiweka kwenye microwave kwa sekunde 40 nilipofanya hivyo nilishangaa mafuta yaliyojichuja kutoka chapati za mama ntilie yule ni mengi na kama nilivyokuwa nakula chapati 3 au 4 ni hatari sana.... nimeacha kula chapati za mafuta na nakula zile ambazo zinaandaliwa bila mafuta na chumvi kwambali ..... halafu kwa miezi 3 sasa nimeacha kula baadhi ya vitu kama nyama na chakula chochote chenye mafuta ... hali yangu imekuwa nzuri na nimepungua kwa kilo 14 na zoezi la kuacha mafuta bado linaendelea kumbe kitambi ni noma....
 
Back
Top Bottom