SoC02 Afya

SoC02 Afya

Stories of Change - 2022 Competition

LucyPound

New Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
2
Reaction score
0
AFYA
Afya ni Hali ya kuhisi vizuri kimwili na kiakili, afya ni chachu ya maendeleo katika Kila sekta.

Tukianzia na madawa, ningependq kuona serikali inatoa kipaumbele Cha kwanza kwenye uagizaji wa dawa kutoka inje, iweke mipango madhubiti ya kukagua ubora wa madawa hayo, kabla hayajaingia nchini na baada ya kuingia yakaguliwe pia kabla ya kusambazwa kwenye jamii.

Kwa wanaopewa dhamana ya hii ya ukaguzi ni vema wakatanguliza utu mbele kuliko kujali maslahi Yao binafsi.

Kwa wazalishaji wetu wa dawa wa ndani ya nchi, nao hivo hivo WAJALI zaidi UTU kuliko maslahi binafsi, wazalishe dawa zinazo ponya jamii na sio kuangamiza jamii.

Wataalam wa afya nawaomba WAJALI utu na sio maslahi, mgonjwa anapokuja kutibiwa nawewe, hapo anakuwa amekupa maisha yake, Ivo inabidi utumie taaluma Yako vizuri katika kumpatia Tiba mgonjwa, na tiba endeane na anachoumwa. Hii itapunguza magonjwa yatokanayo na mlundikano wa sumu ndani ya miili yetu, mfano Magonjwa ya FIGO, KISUKARI na KANSA.

Chakula, Vyakula vinaoagizwa nje ya nchi vikaguliwe vizur na Kwa uaminifu mkubwa kabla ya kumfikia mlaji, Waliopewa dhamana ya ukaguzi wafanya kazi hiyo Kwa Moyo na Utu mwema, bila kujali maslahi binafsi.

Hivi Sasa Kuna vyakula vipo masokoni vimejaa lakin havina ubora Kwa matumizi ya binadamu, magonjwa ya viriba tumbo yameenea kwenye jamii kutokana na vyakula ivi visivo na ubora.

Wazalishaji wetu wa vyakula wa ndani, wahifadhi mazoa Yao ya Chakula Kwa vihifadhio salama visivo na viambata sumu, wanapozalisha vyakula WAJALI zaidi ustawi wa taifa katika kuwa na afya Bora, na sio kujali pesa tu.

Na kwetu walaji napenda kuona tunakula vyakula vya asili zaidi, Ili miili yetu ipate virutubisho muhimu, tufundishe watoto wetu kuwa UTAJIRI sio kula vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta mengi, UTAJIRI ni kula vyakula vyenye uwiano sawa wa virutubisho mwilini mwetu.

Uzazi wa mpango, Napenda kuona serikali inatoa elimu kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango, iwe wazi zaidi kwenye jamii, Ili iokoe jamii ya wanaoteketea Kwa magonjwa ya NJIA ZA UZAZI NA KUISHIA KUWA WAGUMBA, wanapo hamasisha watu watumie njia hizi Kwa kusema mazuri yake au faida zake, basi waseme na hasara zake.

Asilimia kubwa ya wanatumia njia hizi huishia kupata madhara zaidi wengine hupata ugumba na wengine huishia kifo.

Hivi Sasa Kuna ongezeko la magonjwa ya NJIA ZA UZAZI, KAMA SARATANI, KANDIDA, UVIMBE n.k.

Tunaomba wataalam wa afya wawe wazi sana na hizi njia, Ili kama MTU ataamua kuzitumia atumie huku anajua madhara yake, atakuwa na umakini mkubwa anapoamua kuzitumia njia hizo.

Matumiz ya Dawa, Jamii iache matumizi holela ya Dawa, jamii yangu ya Tanzania imezoea matumiz holela ya hizi dawa, MTU anatumia dawa bila kujua ugomjwa unaomsumbua, hii ni hatari sana Kwa afya zetu.

Serikali iweke mkazo Kwa wataalam wa afya wanapouza hizi dawa, wasimuuzie MTU dawa pasipo repoti ya daktari, maana pamoja na SERIKALI kukataza watu kutumia dawa kiholela lakini hili tatizo bado lipo Tena kubwa mnoo, Serikali iunde Sheria nzito Kwa atakaekutwa anamuuzia MTU dawa bila cheti Cha daktari. Hii itapunguza athari zaidi kwenye jamii na watu watakuwa na afya Bora, Kwa tiba sahihi inayoendana na ugonjwa husika.

Vipodozi, Wataalam wa vipodozi wavipitie vizuri vipodozi Ili kujua ubora wake Kwa matumizi ya mwili wa mwanadamu, Wataalam waifundishe jamii kupenda, kutunza na kulinda ngozi zao asili, wataalam wa ngozi wajitolee kuiokoa jamii Kwa kuielewesha namna ya kuifanya ngozi ipendeze Kwa kula vyakula vya aina Fulani, mfano Mboga Majani, matunda na kunywa maji safi Kwa wingi, ukiongeazea na mazoezi ya viungo.

Wataalam wa vipodozi watoe elimu ya urembo Kwa kuielewesha jamii kuwa urembo wa ngozi unaanzia ndani ya mwili na sio nje ya mwili, ukila chakula Bora ngozi itapendeza tu, haihitaji vipodozi vyenye viambata sumu kujichubua Ili ipendeze.

Jamii ya kiafrika Ikubali, ipende na ilinde asili ya ngozi Yao, rangi ya mwafrika ni nzuri sana ikitunzwa kiasili Kwa chakula, Mboga Mboga, matunda, maji mazoezi na kupumzika muda wa kutosha.

Vipodozi vitengenezwe utaalamu wa Hali ya juu, Kwa Mali ghafi za asili kutoka ndani ya nchi, pasipo kuweka viambata sumu, tufundishe watoto wetu kujivunia rangi zao za asili, tufundishe jamii yetu madhara makubwa wanayo weza kupata Kwa kutumia vipodozi vyenye viambata sumu.

Napenda kuona jamii inatambua kuwa thamani ya MTU SIO RANGI YAKE TU, Bali thamani ya MTU ni utu wake, tusiharibu ngozi zetu Ili tuonekane bora kwenye jamii inayo tuzunguka, tukiwa watu waadilifu tutakuwa na thamani pia.

Jamii ihamasishwe kuzalisha vyakula asilia, isi ishie kuzalisha TU! Bali izalishe na itumie vyakula hivo Kwa ustawi wa fya ya jamii.

Jamii ihamasishwe umuhimu wa kufanya mazoezi Kwa afya.

Jamii ipewe elimu sahihi ya matumizi ya maliwato, na usafi wa maliwato Ili kupunguza magonjwa ya NJIA ya mkojo mabayo yamekuwa ni JANGA KUBWA sana Kwa Sasa.

Hospitali za serikali ziajiri wataamu wa afya WENYE ujuzi mkubwa, Kwa kuwa hospitali hizi ndio kimbolio la watu wengi WENYE kipato Cha chini na Cha kati, na jamii kubwa ni watu wa kipato Cha chini na Cha kati, Jamii hii isikose huduma Bora za afya Kwa kukosa uwezo, Serikali iitazama Kwa ukubwa sana JAMII HII.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom