SoC03 Afya

Stories of Change - 2023 Competition

Madam winny

New Member
Joined
Jun 2, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Afya ni moja ni moja ya kichochezi katika utawala bora na uwajibikaji katika jamii ivyo maswala ya afya yanaitaji mabadiliko makubwa.

Hivyo maswala ya huduma ya afya yanatakiwa yatolewe kwenye jamii ili watu waweze kuajibika vyema na kufanya maendeleo katika sekta nyingine zikiwemo za kilimo, biashara, ufugaji na elimu katika familia na majumbani.

Pia maswala ya afya yanatakiwa kuwekwa kwa gharama nafuu ambayo Kila mtu kwenye jamii anaweza kuipata na kuweka uwezekaji mkubwa kwenye matibabu ya wagonjwa kwa kuboresha vifaa na dawa za wagonjwa kupatikana kwa urahisi na kuweka wataalamu wakutosha katika vituo vya afya ili kuepuka matatizo mengine kwa wagonjwa pindi wamezidiwa nakufika katika vituo ivyo.

Maswala ya miundombinu ya Barabara katika jamii katika sehemu za vijijini imekuwa ni changamoto kubwa kwa wagonjwa na na madereva wakati wa kuwapeleka wagonjwa katika vituo vya afya ili wakapate huduma hii tunaona jinsi watu wengi wanaweza kupoteza maisha kulingana na Barabara na ukosefu wa vyombo vya usafiri kwa uwaraka.

Katika maswala ya afya jamii inatakiwa kuwa na usafiri wa mbadala kwa wagonjwa ilikuepusha vifo ,kwa mfano mtu ana nauli lakini anapesa kwa ajili ya matibabu na kazidiwa hitamlazimu kutembea umbali mrefu ili aweze kwenda kupata huduma za kiafya ivyo technojia ya kisasa ina itajika kwa wagonjwa ili huduma ipatikane kwa urahisi.

Na pia wagonjwa wanapaswa kupatiwa elimu muhimu kuhusiana na afya ili waweze kuchukua taadhari punde wanapo pata dalili ya kuumwa na jinsi ya kujikinga na magojwa mbalimbali katika jamii nakupata chanjo mbalimbali haswa kwa watoto wadogo.

Maswala ya kiafya hasa katika sehemu za vijijini watumie njia nzuri katika kuelimisha wagonjwa pindi wanapofika hospitalini kwakuwapa vipeperushi maalumu vyenye kuonyesha dalili za magojwa mbalimbali yanayo hikumba jamii ya kuambukiza hasa kwa watoto,mazee na wenye uwitaji maalumu katika afya.

Utowaji wa matangazo katika vyombo vya habari juu ya afya ni muhimu sana katika jamii hii itawasaidia wengi katika kutambua dalili za awali punde watakapo jihisi tofauti na hitasaidia wagonjwa kuwahi katika vituo vya afya ili waweze kuchukua matibabu ya haraka.

Pia wataalamu wa afya wanapaswa kupewa mafunzo maalumu ili waweze kuwasaidia wagonjwa pindi wanapofika hospitalini.Hivyo basi kuhamasisha wagonjwa juu ya kuchukua taadhari punde wanapo pata dalili yoyote mbaya.

kwa kumalizia,Afya ni moja ya kichochezi katika utawala bora na uwajibikaji katika jamii afya bora hikikosekana watu hawataweza kufanya maendeleo binafsi katika sekta mbali zinazoizunguka jamii hikiwemo secta ya kilimo, ufugaji, elimu na biashara ivyo basi maswala ya afya yapewe kipaumbele ili elimu ziwekupatikana maendeleo katika ufugaji,kilimo na biashara ivyo afya hikiboreshwa haswa maswala ya miundombinu watu wataweza kuwajibika vyema katika jamii nakupelekea maendeleo makubwa nakupunguza vifo katika jamii zetu.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…