Agano Jipya

Rev. Kishoka,
Ukiona Mkandara amekaa kimya basi jua napata darasa safi sana. Kusema kweli wewe na Kitila mnanipa mavituz na kama msomaji ni lazima nipime pande zote kwa uzito wa hoja. Nadhani unaelewa fika mimi nimesimama upande gani lakini kuwa kwangu upande huu haina maana sintatazama upande wapili na hoja zake. Binafsi hulichukulia swala la mtazamo wa kisiasa kama vile dini, mathlan leo hii mimi nikiwa mkristu haina maana kabisa kuwa Uislaam ni dini ya Uongo na kukana hata kusikia mawaidha ya dini hiyo. Huo ni ujinga, na Upumbavu huwa pale unaposoma kisha ukataa vilevile kwa sababu tu neno hilo limesemwa na muislaam ama Kuran hata kama lina ukweli na fundisho.
Hivyo basi napokea hoja zote pamoja na kwamba dini yangu bado ni ile ile yaani mimi Mjamaa hadi kufa!...kama wasemavyo wenyewe - kuwa tulikunywa maji ya Uhuru!. Sasa wanapoupachika Ujamaa tafsiri yao huwa sina zaidi ya kuwatazama na kuwaachia imani yao, kwani haikatazwi hata siku moja Mkristu kuishi na Muislaam nchi moja maadam kila mmoja wetu anafuata ibada zake.
Nimefurahi sana kukusikia ukilichambua Azimio la Arusha na hasa Dira ya taifa ambayo marehemu baba wa Taifa alituachia, wakaja wachawi wakaivuruga na kuipachikia tafsiri kama ile imani ya nadharia isemayo Binadamu wote sawa walosema kina Martin Luther King. Mtu yeyote akitaka kuitafsiri anavyopenda basi haiwezi kuwa na mantiki hata kiidogo isipokuwa ni budi sisi waumini tuelewe yule msemaji alikuwa na maana gani na sio hiyo tunayojaribu kuitunga sisi. Hivyo basi napata darasa mkuu wangu mwageni manyanga!
 
Mkandara:


Inafurahisha Kukusoma.

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa Nadhaharia zilizojikita kwenye "Falasafa za Undani Mwanadamu" kama ilivyokuwa Azimio la arusha. Zinahitaji kama Mika 40 na zaidi kabla hazijawiva kwa matumizi ya mwananchi wa kawaida. Mara nyingi unakuta waalimu wake wanakuwa hawapo. Nafikiri Hata Rev atalitambua hili kwenye Mafundisho ya vitabu vyake vitakatifu kuwa "40" inawakilisha ukamilifu wa mizunguko fulani fulani.

Si unajua azimio la arusha lilifikiwa January 1967? Kwahiyo sio kama ni sisi tunapenda kulichambua na kuonyesha thamani na nguvu zake za kijamii zilizofichika. Ndio mambo yalivyo! Ghafla tunaona kinachotakiwa kuonwa.

Itafika wakati huwezi kujiamkia toka huko uankotoka na kutoa "tafsiri zilizofilisika" za azimio la arusha ukabakia unathamani mbele ya ummma. Kwani mazingira yatakuwa yana lidai na yatakusuta. Pale Zanzibar walikorofisha kidogo kwa sababu za ubinafsi tu..ili waweze kujichotea mali za wananchi na za taifa..Kifisadi. Leo hii mzuka unawafuata..Mzuka wa Kiwira, Bank Kuu..Subiri..Utaona mengi...Yaliyowezeshwa na kulikiuka azimio. Leo tunataka Kitu kama hicho kiwe kikatiba maana sio cha mali ya chama chochote!

Lakini Nimalizie kwa kuseme tu kuwa Value na kanuni za Azimio Ni "kiu ya kweli kwa Taifa la Tz kwa sasa". Hatuongelei chama, itikadi wala imani..UTU haujui vyote hivyo. UTU + UBINAADAMU ni status ambayo ni very objective. NI UTANZANIA!!! UTANZANIA=UTU=UBINAADAMU!!! Na hiki ndicho chimbuko na Azimio. Tangulini Utu, Ubinaadamu ukapitwa na wakati? tangulini hivyo vikawa mali ya NGO AU CHAMA etc..."NI MALI YA WATU WENYEWE"

Kuukana utu ni kualika na kukumbatia ufisadi, dhuluma, magonjwa vita, umasikini, unyama..etc. Maana mwanadamu hawezi kuukana utu na maadili yake AKABAKI SALAMA!!!
 
JC,

Nimesoma kiambatanisho cha Mdeme na nitkujibu baadaye. Nimevutiwa sana na utafiti na maoni ya huyu bwana na kwa kweli, inabidi tuangalie upya mambo mengi ili kusonga mbele!
 
Safari ya kujenga Utaifa haita kuwa rahisi na tutakumbana na ubabe wa kijinga kama wa waziri wa Sheria Mary Nagu. Hii ni kutoka gazeti la mwananchhi!


 

Rev,
Kwa kweli mimi nakuunga mkono kwa jasho na Damu.Hiki kitu ulichoandika hapo juu kimekuja wakti muafaka kwani ni jana tu kwenye ile posti ya Mwafrika ya kuwa na imani na JF nimechangia jana kuelezea what i feel.

Kwa kweli niko tayari kwa lolote.I hate the way Tanzanians are oppressed by few Tanzanians.

Mungu tupe nguvu!
 
JC,

Nikimsoma Mdeme, nimekumbushwa mengi kuhusu Utaifa na Uzalendo. Nimekumbuka jinsi nilivyokuwa pamoja na taabu zote za kiuchumi, nilijifunza kuwa mvumilivu, mchapa kazi na kuwa na juhudi katika kila kitu na kujifunza kila kitu kuongeza maarifa.

Sisi tuliokulia kwa nyimbo na malezi ya kisiasa, lengo halikuwa kutufanya tuwe wakomunisti au kushindwa kujijenga na kuwa wakomavu. Lengo lilikuwa ni kututayarisha katika ushindani wa dunia hii na majaribu yake bila kukata tamaa au kukimbilia njia fupi eti kusawazisha na kujiondolea matatizo.

Naomba ninukuu hotuba ya Franklin Delano Roosevelt aliyoitoa March 4 1993, siku alipoapishwa kuwa Raisi wa Marekani. Mkumbuke kuwa Marekani ilikuwa imeanza kujinasua kutoka Deep Depression. Pamoja na utajiri ambao Marekani ilikuwa nao, pamoja na matatizo yote yaliyoikabili, ni Utaifa na uimara wa uongozi ndio uliobadilisha sura ya Taifa hili kw amara nyingine na kuleta msukumo wa mapinduzi katika uzalishaji mali kujenga jamii inayojitegemea. Ingawa si kila mtu ni tajiri au anajitegemea, lakini juhudi za kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata tumaini na kujijua kuwa Serikali yake iko nyuma yake kumsaidia ndiko kulikobadilisha sura ya nchi hii na ndio maana hii hotuba, inatambulika kama hotuba kabambe iliyowapa Wamarekani matumaini mapya na ni jinsi Roosevelt alivyofuatilia ahadi na kiapo chake.

Msisitizo ni wa kwangu ambao naufananisha na safari tuliyonayo Watanzania.

 
Rev. Kishoka.

Napitia Kwa karibu Hotuba ya Franklin Delano Roosevelt aliyoitoa March 4 1933. sinayo kwnye library yangu. Nitarejea!!
 
Rev,
It was a fantastic speech! Kwa kweli nikisoma hii hotuba hadi mapigo ya moyo yanaenda kasi.
But,tofauti na hapa kwetu Franklin Roosevelt aliishi na kutenda kulingana na hii speech jambo ambalo kwa viongozi wetu waliopita na wa sasa ni tofauti.Labda Movement zetu tunazoanza na ukombozi ujao ubadilishe hii kasumba.

Alichofanya sasa Roosevelt ni Ku "WALK THE TALK"

Alianza kuwa na Vision na kuona kuna changes zinazotakiwa.


Natamani na nilivutiwa sana kufuatilia historia ya taifa la Marekani mpaka leo hii kuwa super power.Kwa kweli Roosevelt na timu yake ya wanauchumi kama akina Sir Alfred Marshal waliifanyia marekani kazi kubwa sana.

Tanzania yetu inaweza kuwa taifa kubwa sana baadae na sisi kama kweli Tukiamua kujituma kwa Akili,damu na jasho
 
Our foundation for our Marshall plan was Azimio la Arusha.

Tanzania can be an economic superpower in Africa if it will keep its priorities right and create a structure that enables its citizens to be productive and self sufficient.

We have become dependent because of fear of executing the right thing, fear of saying the right thing. We are no longer motivated and do not think of any creative ways to boost morale in production.

We have ended up surrendereing to external grants and loans and imortation of foreign investments.

Our poverty levels are raising and it is due to bad policies and lack of accountability from the Government and rulling party.

If the leaders are lacking vision, are lazy, are looking for easy ways to make money, are corrupt, inneficient, unaccountable and have no morals or ethics, how do you expect to have followers (nation) that is self disciplined?

Charity begins at home, and our home is on our leadership.

Only when we have good governance and accountability, then we will see our dream become reality. Our nation will prosper!

Lakini, kigugumizi kiko kwenye Siasa safi na uongozi bora.

Ukimsoma Roosevelt, hata Marekani walisitisha kujenga interest za foreign investment, wakaweka mkazo kwenye kuinua uchumi kwa mikono yao kutumia maarifa na juhudi na si kutegema "saidia maskini"

Tumeridhika na umasikini kiasi kwamba tumekuwa vipofu. Suluhisho lake ni kuwa na AGANO JIPYA la Utaifa. Tuiangalie Katiba yetu na Azimio la Arusha na kuoanisha malengo na yale yanayotupa nguvu kama Taifa.

Tulipoimba "sisi tunataka kuuwasha mwenge", haukuwa mwenge wa kuwaka mafuta tuu, bali ilikuwa ndiyo tamko rasmi la kujijenga kama Taifa huru!
 
.. only thing we have to fear is fear itself

Tamko hilo la Roosevelt la “ogopa woga kwa moyo wako wote” Leo hii katika sanyansi na dhana mpya kabisa (1998/2000) ya kutathmini Ustawi wa jamii Emotional Intelligence (EI) au Ukomavu wa utu linachambuliwa hivi;

WOGA unatizamwa katika njia tofauti kabisa na ile inayofahamika kwenye Psychology na psychiatry. Woga, wasiwasi na Mashaka, (negative emotions/hisiahasi) vinaweza kutumiwa kama nguvu maalum ya kusaliti ustawi wa jamii iliyopevuka na kujitawala kiuchumi na kibinadamu. Mnapokuwa kwenye kundi na mkashituliwa na "Mbwa makali…" yule atakaye zalisha au kusambaza woga zaidi ya wenzake ndiye atakaye kuwa wa kwanza kuwa kitoweo cha mnyama huyo mkali. fuatilia. http://www.duniahai.com/Uharibifu wa Hisia Hasi.html
Atakaye zalisha woga zaidi atashambiliwa, atakuwa mnyonge na atakaye fedheheshwa na mnyama huyo. Atajulikana kama “With low EI”. Yaani aliye duni katika kuerevuka kihisia. Ili kuelewa vizuri dhana hii , Kwenye neno mbwa liondoe na weka neno FISADI, ndipo utelewa vema Roosevelt anasema nini. Yaani fisadi akutishe kwa kukumwagia tindikali usoni na wewe utishike, fisadi akutishe na wewe uogope pale anaponyofoa vipengele muhimu kwenye maagano, maazimio na nyaraka muhimu za kitaifa. Fisadi atoe tafsiri za kifisadi za kitu kama azimo la Arusha na wewe ukae kimya unatetemeka kwa woga! Hakika Fisadi atakufanya kitoweo muafaka. Atatafuna jamii nzima kupitia kodi za walalahoi zilizoko bank kuu, mikataba hovyo ya uchumi wa taifa, miradi muhimu ya kitaifa, kuyumbisha makusudi dira ya taifa kwa faida yake etc. Lakini yote haya ni kwa kuwa mwananchi kajitakia mwenyewe ;kawa mkarimu wa woga tu kwa fisadi. Kimsingi Kama wewe ni Mtanzania wa kweli: Kamwe Usimuogope fisadi. Hasa unapopigania na kutetea haki ya wanyonge waliowengi. “Milele usimwezeshe Fisadi” kwa Hisia hasi! Erevuka kuhusu hisa zako sasa!Na uziwajibikie.

Woga na hisia hasi anasema Roosvelt havituwezeshe kamwe kusonga mbele na kujitokeza kutetea taifa kwa kusema Ukweli kama Ulivyo mioyoni mwetu au kama tunavyoujua na kuuamini.”This is preeminently the time to speak the truth, the whole truth, frankly and boldly. Nor need we shrink from honestly facing conditions in our country today. This great Nation will endure as it has endured, will revive and will prosper. So, first of all, let me assert my firm belief that the only thing we have to fear is fear itself”

Shime tumnyime Fisadi kile anachotaka kutoka kwetu “ngvu ya hisia hasi”. Bila sisi kumpa woga, wasiwasi, unyonge na kunywea hovyo mbele yake, fisadi hana Nguvu peke yake ya kutunyonya nakutufanyia michezo inayoendelea sasahivi ndani ya taifa letu!

Bila kumpa Mbwa woga , anauweka mkia sehemu inayostahili .. katikati ya miguu yake na kurudi alipotoka kwa unyonge mkubwa. Huo unakuwa ni ujembe tosha kwa Fisadi wa aina yeyote toka kwa wale anaowafisadi. Maana anajua Nguvu ya fikra toka kwa Mtanzania asiye ujua woga wa kijinga. Fikra Pevu zilizojikita kwenye kiwango cha juu cha EI sio IT; Ni silaha tosha ambayo inaweza kumtingisha fisadi hatakama yuko JF na kufuatiwa na hatua ACTION NOW!!!Ambazo lazima lazima Zitakuwa Productive!!
 

Mkuu Jc,
Kwa kweli kati ya vitu vinavyonitia huzuni ni woga ambao watanzania walio wengi tumekua nao.Nikiangalia case mbalimbali za kifisadi kama za Ballali watu walipiga kelele hadi Jk alipoona hali inakua mbaya akamtoa,sasa kuna hawa wakubwa zake ambao kwa nafasi zao moja kwa moja wanatakiwa wawajibike kama akina Mramba na Mgonja.Sasa kwa sababu ya woga wa watanzania wengi tunashindwa kushikilia na kuanzisha kampeni za kuwawajibisha au kumlazimisha rais awawajibishe.


Unajua Taifa kama la Marekani,wananchi wake walianza kuwa na ujasiri wa kutaka mabadiliko na hasa ya kiuchumi,kwa hiyo ilikua ngumu kwa Mmmarekani kuvumilia utovu wowote wa nidhamu uliokua na kila dalili ya kuhujumu uchumi wanchi yao ilihali wao wanataka kupiga hatua mbele.


Sasa inabidi tuanzie hapa tulipo leo hii
 

Mkandara:

Kwanza naanza na Matamshi haya:

Mark Twain said, "In the beginning of a change, the patriot is a scarce man, and brave, and hated and scorned. When his cause succeeds, the timid join him, for then it costs nothing to be a patriot"
Alafu nitoe angalizo hili:
Nakumbuka vizuri tulijaribu kuchangia mengi mazuri kisha kuna wakati niliomba mchango wa wengi nikiwa na haja kubwa ya kuorodhesha maoni ya watu na kutunga Azimio jipya (Agano jipya

Nimepitia kila post kwenye hii thread kwa undani wake. Nimekuja kukuta kuwa ningefurahi sana kama ungenipa some or all findings za kile mlichokipata that time ref the quote"....Nafkiri mimi sikuwahi kuziona. Pls Nafikiri kwa faida ya wengi haitakuwa vibaya kma ungetupa hata muhutaari. Thanx alot!
 
Azimio,

Leo nimeshinda nikibarizi katika mtandao (internet) kutafuta vitendea kazi kuhusiana na Suala la Katiba na muungano. Chungulia PM yako halafu tuwasiliane.

Wakati huo huo, tumsubiri Mkandara aje na busara zake za upande wa pili wa shilingi! Wikiendi njema.
 
One of the things we need to do as society is to rescue Watanzania from fear. CCM has been ruling using threats and fear as a way and means to justify its existance and credibility.

What took place in Monduli and so is Bariadi, tells me that CCM is buying souls using threats and planting fears and capitalizing on poverty to justify that CCM is the only party that can lead Watanzania from poverty.

When I wrote CCM Pambalama, I was advocating for CCM to split so that "upinzani makini" should have emerged. However I think it was wrong for me to assume that if CCM will split into two factions, Tanzania will be better.

No we do not need CCM at all. I will send my apologies to wazee wangu wa Chama, kina Warioba, Salim, Malecela and others by stating that CCM ni Mzizi wa Umasikini na Unyonge wa Tanzania na Mtanzania!

Hili agano jipya nalo liongeze mipaka na si kupiga ufisadi pekee, bali ni kumkomboa Mtanzania kutoka makucha na uanaharamu unaofanywa na CCM.

Ugonjwa wa kutumia vitisho si lazima uwe umetoka Chimwaga, Lumumba au Kisiwandui, bali ni tabia iliyojijenga kwa nguvu sana vijijini na katika Mitaa kwa wale viongozi wa ngazi za chini wa CCM kutumia ubabe na vitisho kushurtisha wananchi wakubaliane na CCM hata pale inapoonekana wazi kuwa CCM imekosea.

Naomba nijinikuu kwa majibu yangu kwa Mkandara kuonyesha ni jinsi gani huko kwenye ngazi za chini vitisho na rushwa vimetumika kujenga woga na hata kununua kura ili mradi CCM iendelee kushika hatamu!

 
Azimio jipya,
Duh, sikumbuki vizuri kichwa cha mada ile lakini nadhani ilisema kitu kama:- ILI TUENDELEE. TUNAHITAJI blaa blaaa ilianza mwaka juzi winter (between Nov au Jan) hadi mwaka jana nadhani kwa mara ya mwisho nimeandika mchango wangu mara tu baada ya kurudi huku mwishoni mwezi April.
Sidhani kama bado ipo inabidi tumwombe Invisible afanye mavitu..
 
Rev sikuiona hii, hopeful mipango bado inaendelea ingawa safari ni ndefu lakini nadhani mapambano bado yanaendelea, sijasoma watu wengine wanasemaje ila nitasoma kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…