Chikawe Jr
Member
- Jun 6, 2017
- 23
- 85
Anaandika: Juma George
Nimejaribu kufanya utafiti juu ya hoja ya KATIBA iliyozungumzwa na baadhi ya watanzania (Wanasiasa na Wasio-wanasiasa), kwa muda wa wiki tatu na kugundua kuwa lina maslahi ya kisiasa kwa sehemu kubwa. Nimepitia makala na nukuu mbalimbali za watanzania juu ya kwa nini tuwe na katiba mpya kwa sehemu kubwa zinamsukumo wa kisiasa ndani yake.
Licha ya kuwa na umuhimu wa kipekee, Hivi kalibuni suala la katiba mpya limewapatia watu wengi umaarufu nchini na wengine kuitumia hiyo kama agenda ya kuungwa mkono na makundi mbalimbali ya kijamii. Ni ukweli usiopingika kuwa SUALA LA KATIBA MPYA NI NYETI NA MUHIMU SANA lakini linaweza kupoteza unyeti na umuhimu wake kama watu wachache wenye dhamira ovu juu ya jambo hili wakiwa mstari wa mbele kutuhamasisha kulidai. Kuna umuhimu wa kila mtanzania kuona kipi muhimu kuliko kipi na kwanini bila kusahau wakati.
Agenda hii ya katiba Mpya sio ngeni na tayari watanzania tulishaingia katika mchakato wake ambao haujamalizika mpaka sasa. Licha ya umuhimu wake, agenda hii ilizungukwa na mizengwe mingi na kufanya mchakato kutokamilika kwa wakati. Mizengwe hii kwa sehemu kubwa ilihasisiwa na kikundi cha watu wachache wenye "Maslahi Binafsi" ambayo ni vigumu kuyaona kwa macho. Kuna makundi mengi lakini leo nitaeleza kwa uchache tu baadhi ya watu walioshiriki kudhoofisha agenda hiyo na kuibaka KATIBA MPAYA mchana kweupe.
LOWASA NA URAIS.
Ikumbukwe agenda hii ilikuwa katika kipindi ambacho kama Taifa tunaelekea katika uchuguzi mkuu, na EDWARD NGOYAI LOWASA akiwa na dhamira ya kugembea nafasi ya URAIS kupitia CCM kabla hajaingia CHADEMA, alikuwa makini sana kuhakikisha hakuna jambo au utaratibu wowote unaoweza kumzuia kufikia malengo yake hayo ikiwomo na katiba mpya.
Katika katiba ya Tume ya JAJI WARIOBA, yapo mambo tofauti tofauti ambayo yaliwakwaza watu fulani kwa maslahi yao na Makundi yao. Kila kundi lilisimama kidete kuhakikisha maslahi yao yanaingia katika katiba kwa gharama yoyote ile. Na hapa ndio unapokuja umuhimu wa jambo hili kufanyika wakati una watu wazalendo kwelikweli.
Lowasa akiwa katika harakati zake za kusaka Urais kati ya mambo ambayo hakutaka yawepo kabisa katika katiba Mpya ni kuhusiana na maadili ya viongozi. Akiwa kama msaka Urais suala la Maadili ya Viongozi lilikuwa mwiba mkubwa kwake na hasa kipengele cha Kuzuia Viongozi wa Serikali kuwa na "Akaunti binafsi" nje ya Nchi. Hili lilikuwa jambo gumu kwa viongozi wengi sio LOWASA PEKEE bali wapo wengi hasa wale wanaonufaika moja kwa moja na MFUMO WA UFISADI NCHINI. Kuweka suala la Maadili ya viongozi katika katiba iliyopendekezwa na Tume ya JAJI WARIOBA ulikuwa mwiba juu ya tabia za baadhi ya viongozi hao KUFICHA FEDHA huko ughaibuni wanazozipata kwa njia za UFISADI.
SIO LOWASA PEKEE ALIEIKATAA RASIMU YA WARIOBA.
Wapo viongozi wengi walioingia kuharibu mchakato huu wa katiba kwa kuwa katiba iliyopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba ilikuwa mwarobaini wa matatizo mengi ijapokuwa *ilikuwa na mapungufu machache ambayo yangeweza kuangaliwa vizuri kwa mapana yake mfano suala la serikali 3 mimi siliungi Mkono na siwezi kushauri liwepo*.Viongozi wengine waliopinga suala la MAADILI YA VIONGOZI hasa kipengele cha KUZUIA VIONGOZI WA UMMA kuwa na Akaunti nje ya nchi alikuwepo KINGUNGE NGOMBALE MWIRU, FREEMAN MBOWE, SUMAYE, n.k.
KWA NINI MAFISADI WANAOGOPA KUTOKUWA NA AKAUNTI NJE YA NCHI.
Kumiliki akaunti nje ya nchi kwa viongozi wa UMMA ni mpango mahususi kabisa ulioasisiwa na kundi la wanamtandao wa UFISADI ili kuhakikisha FEDHA zote wanazopata kwa kuliibia taifa hili hazionekani hasa katika mifumo halali ya fedha iliyopo ndani ya nchi. Hii inawawezesha kuendesha Mipango Ovu ikiwemo na matumizi makubwa ya RUSHWA wakati wa chaguzi au kutafuta nafasi fulani ya maamuzi makubwa ya Rasilimali za Taifa.
Kutokana na kumiliki fedha nyingi nje ya nchi ambazo hazijulikani, wanaweza kuendesha uchumi wanavyotaka na kuendelea kutawala kwa kuweka watu wa MFUMO WAO au wale wanaowaunga mkono. Kwa uwezo wa pesa wamejizolea wafuasi ambao siku zote wanawatukuza na kuwasifu ili kuomba hisani mbalimbali zikiwemo nafasi za kazi au kukumbukwa wanaposhika madaraka.
MADAI YA KATIBA MPYA YANACHOCHEWA NA WATU WASIO NA NIA NJEMA.
Kumekuwa na ongezeko la baadhi ya watu hususani wanadiasa UCHWARA kushawishi Watanzania kuwa katiba ndio suluhisho la kila kitu jambo ambalo sio kweli. Kwa sehemu kubwa jambo hili linachochewa na wanasiasa ambao lengo lao kuu ni kushika Dola ndio maana msingi wa madai yao katika katiba mpya ni TUME HURU TU hawana lingine. Usifikiri LOWASA angependa kushitakiwa kama angekuwa Rais kwa sababu mpaka hapa tu kwa nafasi alizoshika anastahili kufikishwa mahakamani sembuse angekuwa RAIS?. Tusijidanganye watanzania wasiasa hawana la zaidi isipokuwa ni tamaa zao za kushika Dola ili waendeleze UFISADI na maombi yao Makubwa ni TUME HURU TU na sio kitu kingine.
Katika hili la madai ya katiba mpya yanaloendeshwa na WANASIASA iwe ndani ya CCM au kutoka Nje ya CCM, halina tija kwa tiafa hasa wakati huu wa Vita vya kiuchumi na Ufisadi nchini, isipokuwa lina tija kwa maslahi yao ya kisiasa, hivyo basi tusiyumbishwe wanapokuja na hoja kama hizi ili kujificha tuwaambie AGENDA yetu ni kuhakikisha kwanza MAFISADI YOTE yanashughulikiwa ipasavyo iwe kimya kimya au waziwazi na wajibu wetu sisi ni kumuunga Mkono Rais Magufuli katika kupambana vita hii kubwa yenye kuhitaji uthubutu.
MKAKATI WAO WANAOUTUMIA
Baada ya Mafisadi kugundua kuwa RAIS Magufuli yuko imara katika kuwashughulikia, wameandaa mpango mahususi kuitumia agenda ya katiba mpya kama njia pekee ya kunyamazisha hoja ya UFISADI kwa kuwa wameshikwa pabaya. Katika mpango huo wanatumia baadhi ya watu wenye ushawishi katika jamii ili wawashawishi watu wao wanaowaamini na kuwafuta waunge mkono agenda ya katiba mpya na kutupotezea Malengo yetu katika hii vita kubwa ya UFISADI NA UHUJUMU UCHUMI. Watu wanaotumika hasa ni VIONGOZI WA DINI, WANASIASA MBALIMBALI WANAOKUBALIKA, WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU, NGO's, n.k.
Watu hawa wanatumiwa kutoa matamshi au maandiko mahala pao pa kazi kuwaaminisha wananchi wao kuwa KATIBA ni muhimu sana kuliko hii vita ya kitaifa tuliyonayo. Na kwa hili tumeona hivi karibuni viongozi wa kidini na watu mbalimbali kutoa matamko ya kuonyesha tunahitaji sana katiba muda huu ila ni mkakati madhubuti UNAOFADHILIWA NA MTANDAO WA UFISADI NCHINI.
USHAURI WANGU KATIBA ISUBIRI MPAKA TUTAKAPOKUWA NA UHAKIKA WA WATU SAFI WA KUSIMAMIA MCHAKATO HUO.
Mchakato wa katiba mpya ni kama chakato wa kula chakula. Ni ustaharabu wa kawaida kuanza kunawa mikono kabla ya kula chakula, vivyo hivyo kuanzisha mchakato wa Katiba kabla hujasafisha makundi dhalimu ambayo yananguvu ya kununua chochote isipokuwa uhai tu tutakakuwa tunafanya makosa makubwa sana. MAFISADI na washurika wao wamejipanga kuhakikisha KATIBA ambayo ndio Msingi mkubwa wa taifa inatoa nafasi ya wao kuishi maisha yao bila kubanwa.
Haya tumeyaona katika Mikataba ya Hovyo ambayo baadhi ya Wenzetu walisign huku wakijua wanaliangamiza taifa lakini walijali maslahi yao binafsi na si ya watanzania wote. Kwa hiyo Watanzania wenzangu suala la katiba sio la kisiasa pekee ni jambo nyeti na linalohitaji uangalifu mkubwa sana ili lisije likanajisiwa na watu wachache wenye nguvu na mabavu ili kulinda maslahi yao.
Kwa sasa mimi binafsi naona ni muhimu sana kurekebisha maadili ya watumishi wa UMMA kabla ya kuingia katika mchakato mkubwa kabisa wa KATIBA MPYA. Katika kurekebisha maadili haya NAMSHAURI Rais wetu Mpendwa JOHN JOSEPH MAGUFULI tunaweza kufanya marekebisho ya Sheria yetu ya UTUMISHI WA UMMA NA MAADILI kwa kuongeza udhibiti kwa watumishi wa serikali. Katika Sheria hiyo napendekeza kuongezeka kwa zuio la Viongozi wa Serikali kuwa na Akaunti nje ya Nchi kuanzia sasa ili kuongeza jitihada za kupambana na UFISADI NA UHUJUMU UCHUMI.
Hii iambatane na kuwataka wagombea wote wa nafasi za UBUNGE na URAIS kurudisha fedha zao zote ndani ya nchi wakati wa kuomba ridhaa ya uongozi huo ili kuzuia matumizi ya pesa chafu katika uchaguzi. Tukiweza kudhibiti hili basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa na suala KATIBA MPYA likasubiri mpaka wakati muafaka.
Suala la marekebisho ya sheria ya maadili ya viongozi na utumishi wa Umma kwa kuongeza kipengele cha kuzuia viongozi kuwa na Akaunti Nje ya Nchi ni muhimu sana na unaweza kuwa mwarobaini tosha wa kupambana na kuzuia UFISADI nchini kama litapewa kipaombele.
TANZANIA KWANZA...........
....................... UZALENDO WA KWELI
Chikawe Jr.