Agizo kwa wanaume wa Dar toka kwa wanaume wa mikoani

Ushajiuliza kwanini? Hao ndio wawezeshaji wa pesa mpaka shughuli ikakamilika. Hamziki mpka pesa zitoke Daslam unategemea nini
 
Ila nanyi wa kijijini kwanini msiwe mnazika mpaka mtusubirie sisi huku mjini,Mpo radhi msizike mpaka kauli ya mwisho itoke dsm,Kumbuka Dar ndo kila kitu mkuu,
 
Ila wanaume wa mikoani akili zao mbovu sanaaa
Maana unakuta mtu mzima anamaswali ya kipumbavuu.
Eg utaskia eti Dar Kuna mwendokasi..???
Mwengine utasikia eti Dar Kuna lami kila sehem..??
Mwengine eti Dar Kuna madem wengi.
Eti Tigo ndio ninii..???
Yaani mbwa kwelii nyie wa naume wa mikoani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hotuba ya kuaga ya Mtume Muhammad (SAW)

Khutba hi)i ilitolewa na Mtume Muhammad (SAW) tarehe 09 Dhul
Hijja mwaka wa 10 Hijriya kwenye Mlima Arafah.
1 Enyi watu! Nisikilizeni maneno yangu vizuri , kwani sidhani kama baada ya mwaka huu nitakuwa pamoja nanyi. Hivyo sikilizeni
kwa makini nitakayoyasema na (maneno haya ) mfikishieni kila
asiekuwepo hapa leo.

2."Enyi watu! Hakika damu zenu na mali zenu ni takatifu kwenu kama mlivyoufanya mwezi huu kuwa mtakatifu na mji huu kuwa
mtukufu? rudisheni amana mlizokabidhiwa kwa wenyewe wanaostahiki.
Msimdhuru yeyote ili nanyi msije msije mkadhuriwa. Kumbukeni mtakuja
kukutana na mola wenu naye atahesabu amali zenu. Allah (SWT) amekukatazeni kula riba . Hivyo riba zote zimeondoshwa na mna haki ya kubaki na rasilmali (mitaji) yenu. Hamna haki ya kudhulumu wala kudhulumiwa . Allah(SWT) ameharamisha riba na kila haki ya kisasi iliyekuwepo enzi za Ujahiliya imefutwa!

3 "Enyi watu! washirikina wanajaribu kuakhirisha (kuchelewesha)
kalenda ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyo
itukuza Allah na kulifanya halali jambo ambalo Allah(SWT) ameliharamisha
na kulikataza jambo ambalo Allah(SWT) ameliruhusu Miezi kwa Allah(SWT) ni
kumi na miwili. Minne kati yao ni mitakatifu, mitatu ikiambatana (Dhul Qaadah, Dhul Hijjah na Muharram) na mmoja (Rajab) uko kati ya Jumada (ya mwanzo na ya mwisho) na Shaaban.

4 "Jiepusheni na shetani kwa ajili ya kuilinda dini yenu . Tayari (shetani) amekata tamaa kwamba hataweza kuabudiwa katika ardhi hii milele lakini bado ana mikakati ya kukupotezeni hivyo
tahadharini nae katika mambo mengine."

5 "Enyi watu! ni kweli mna haki juu ya wanawake na wao pia wana haki juu yenu . Kumbukeni mmewachukua kuwafanya wake zenu kwa amana ya Allah(SWT) na mmehalalishiwa (kustarehe) nao.

6 "Nnakuusieni kuwatendea wema wanawake na kuwa na huruma kwao
kwani ni wake zenu ni wasaidizi wenu.

7 " Enyi watu, nisikilizeni kwa utulivu , mcheni Allah(SWT), msali sala tano kila siku, fungeni katika mfungo wa Ramadhan na toeni Zakah. Tekelezeni ibada ya Hijjah ikiwa mna uwezo."

8. Binadamu wote wametokana na Adam na Hawaa, hakuna mbora kati
ya mwarabu na asiyekuwa mwarabu , wala asiekuwa mwarabu kwa
mwarabu, wala mweupe kwa mweusi au mweusi kwa mweupe
isipokuwa kwa Taqwa( kumcha Allah).*

9"Enyi watu Eleweni * kila muislamu ni ndugu kwa muislamu na waislamu wote
ni ndugu. Hatohalalishiwa muislamu kitu chochote isipokuwa kile alichopewa kwa ridhaa na ndugu yake. Wala msidhulumu nafsi zenu. Na msisahau kwamba kuna siku mtakutana na mola wenu na
mtahesabiwa amali zenu. Hivyo tahadharini msije mkapotea baada
yangu"

10 "Enyi watu! Hakuna tena Mtume baada yangu na hakuna dini nyengine itakayokuja. Ninakuachieni vitu viwili ambavyo
mkishikamana navyo hamtopotea milele navyo ni QURAAN na SUNNA.

11 "Wale wote walionisikiliza waufikishe ujumbe huu kwa wengine
na wengine waufikishe kwa watakaofuatia na inawezekana hawa wa mwisho wakayafahamu vyema maneno yangu kuliko hawa walionisikiliza moja kwa moja."

"Ewe mola shuhudia kwamba nimefikisha ujumbe kwa watu wako"
******
*Inshaallah * atakaepata ujumbe huu ahakikishe anamfikishia mwengine
kama tulivyoagizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Sasa huyu mtume tumuweke kundi gani Kati ya wanaume wa Dar au wa mikoani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila nanyi wa kijijini kwanini msiwe mnazika mpaka mtusubirie sisi huku mjini,Mpo radhi msizike mpaka kauli ya mwisho itoke dsm,Kumbuka Dar ndo kila kitu mkuu,
Kila kitu hadi kwa maiti?
 
Mkuu huyu ni wa dar au mkoani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…