Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,483
- 2,392
Wadau kama mtakumbuka Waziri Silaa alipoteuliwa tu kuwa Waziri ktk siku zake 100 za kwanza moja ya maagizo yake mazito ni hili la kuzuia ujenzi wa vituo vya mafuta nchi nzima na kuwataka makamishna wasaidizi wa mikoa kumpelekea orodha ya vituo vya mafuta vikionesha umbali toka kituo hadi kituo, kiwanja kilivyopata matumizi ya petrol station, kiwanja kama kipo kwenye makazi namna utaratibu wa kubadili matumizi ulivyofuata n.K.
Toka agizo hilo amelitoa wananchi tulitarajia kupata taarifa ya utekelezaji wa agizo lake na hatua zilizochukuliwa kwa wahusika lakini mpaka sasa ni miezi kadhaa waziri yupo kimya na ujenzi wa vituo vya mafuta unaendelea kama vile hakukuwa na katazo lolote.
Hii ndio Tanzania taifa la maagizo bila utekelezaji.
Pia soma:

- Waziri Jerry Silaa apiga marufuku ujenzi holela wa Vituo vya Mafuta
- Pongezi Waziri Silaa kumsimamisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi vituo vya Mafuta vinajengwa katikati ya Makazi
- Suala la petrol stations aliloagiza Waziri wa Ardhi limeishia wapi?
- Kuongezeka kwa Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kwenye makazi ya watu Serikali inasubiri ya Morogoro yatokee ndio ichukue hatua?