Agness masogange anywa sumu

Agness masogange anywa sumu

Gumzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2012
Posts
211
Reaction score
8
MUUZA sura anayetamba kwenye video za Kibongo, Agness Jerald ‘Masogange' juzikati alinusurika kuaga dunia baada ya kuchanganya pombe na dawa aina ya Cephalaxin kutokana kuudhiwa na mpenzi, Risasi Jumamosi lina habari kamili.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Masogange aitwaye Janneth asubuhi ya siku ya tukio, Agness alimpigia simu na kumtaka afike nyumbani kwake kwa kuwa tumbo lilikuwa likimsumbua.

Hata hivyo, Janneth alidhani rafiki yake huyo alikuwa akimtania, kwa kufikiria kuwa alikuwa akimtaka tu afike nyumbani kwake na hakuwa na tatizo lolote.

Jananeth alizidi kueleza kuwa baada ya muda alipigiwa tena simu na Agness huku akilia ndipo alipohisi kuwa kulikuwa na kitu, akaamua kukodi teski kwa ajili ya kumuwahi.

"Nilipofika nyumbani kwake nilikuta amejifungia kwa ndani, hivyo ikabidi kuvunja mlango, nilipofanikiwa kuingia nilimkuta akiwa hoi," alisema Janneth.

Janneth alisema kuwa baada ya kuvunja mlango alimkuta Agness akiwa amelala karibu na chooni na pembeni yake kukiwa na chupa ya pombe na pakti ya dawa.

"Nilikwenda dukani na kumnunulia maziwa na kumnywesha kwa kuwa nilihisi atakuwa amechanganya dawa na pombe, kisha nikamkimbiza katika Hospitali ya Mama Ngoma kwa ajili ya matibabu."
 
mtoto nshapiga ukimla 0713 anakupenda akuachi na anjua kupenda na anapenda sana 0713 yawezekana kweli.
 
Alikosea kunywa sumu ya namna hiyo. Si angekunywa ile ya dakika mbili tu!!.
 
alikuwa ana-bip huyo, chezea kufa sio masikhara,

angekuwa siriaz kweli asingempigia simu rafikiye!
 
alikuwa anatisha toto.
kujiua ni mbombo ngafu.

Alitaka kumake headline.nawaambieni global saa ingine wanaumba habari tu,eti kapigiwa simu kakubali alikunywa sumu,,wap! na hilo ni kosa la jinai,polisi wenyewe wanavotafutiza makosa ya hela wangekuwa washamrukia zamani gani
 
Sasa kwa nini aliomba msaada kama alikuwa na nia ya kujiua au alitaka atoke magazetini?

Chezea kifo...
 
Sitaki kuamini kuwa alitaka kujiua kwa sababu ya mwanaume kwa kuwa ameshakuwa sugu wa mapenzi huyo, ila sasa nadhani kuna ile ishu inayosambaa mitaani ndiyo inayomtia hofu....
 
Back
Top Bottom