Agricom yaikabidhi Serikali Trekta 500, Power Tillers 800 na vifaa vingine vya Kilimo

Agricom yaikabidhi Serikali Trekta 500, Power Tillers 800 na vifaa vingine vya Kilimo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
1723146685966.jpeg

Kampuni ya Kitanzania ya Agricom imekabidhi vifaa na zana mbalimbali za kisasa za kilimo kwa serikali kupitia Wizara ya Kilimo, wakati wa maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika Dodoma leo.
1723146658058.jpeg

Hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan, ambaye alishuhudia makabidhiano hayo.

Vifaa na zana zilizokabidhiwa kwa serikali ni pamoja na Trekta 500, Power tillers 800 pamoja na Vifaa vya maandalizi ya shamba 200.

Makabidhiano haya ni sehemu ya mpango wa serikali wa "Agenda 10/30: Kilimo ni Biashara," unaolenga kuboresha kilimo nchini kwa kuwapatia wakulima zana bora zinazoongeza ufanisi na uzalishaji. Hii inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo, kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa na kuimarisha usalama wa chakula nchini.

Aidha Rais ameweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha kwanza cha uunganishaji wa matrekta katika ukanda wa Afrika Mashariki leo katika maonesho Kimataifa ya Kilimo ya nane nane 2024 Jijini Dodoma.

Kiwanda hiki cha uunganishaji matrekta kinajengwa kwa ushirikiano kati ya kampuni ya Kitanzania ya Agricom Africa Ltd na Mahindra ya Nchini India kampuni kubwa duniani kwa uzalishaji wa Matrekta.

Kiwanda hiki kipya kitatengeneza matrekta maarufu ya Mahindra yenye nguvu na uimara aina ya Swaraj, chapa inayotambulika na kuaminika kwa miongoni mwa wakulima wa Tanzania.

Itakumbukwa wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya Kitaifa nchini India mwezi Oktoba 2023, aliialika kampuni ya Mahindra kuanzisha kiwanda cha uunganishaji matrekta nchini Tanzania.

Kiwanda kipya cha uunganishaji matrekta kinatarajiwa kukamilika mwaka 2025, na kinatarajiwa kuzalisha matrekta 10,000 katika miaka 5 ijayo, mbali na Tanzania kiwanda hiki kipya kitahudumia pia nchi jirani za Afrika, kikiimarisha kujitegemea katika uunganishaji na usambazaji wa matrekta katika ukanda huu.

Kampuni ya Agricom Africa Ilianzishwa mwaka 2009, ikiwa ni msambazaji mkuu wa vifaa vya kilimo nchini Tanzania yenye mtandao mkubwa zaidi wa usambazaji kwenye nchi za Afrika Mashariki.

 
Back
Top Bottom