Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,814
- 8,118
Hakuna ubishi kwamba fursa za kilimo Tanzania ni kubwa na soko la bidhaa za kilimo duniani ni kubwa na la uhakika na pia halina dalili za kufifia kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu.
Hata hivyo soko la bidhaa za kilimo duniani linahitaji vitu vitatu.
1. Bidhaa zenye ubora na (Quality products).
2. Uzalishaji wa kutosha wa bidhaa hizo;
3. Upatikanaji wa uhakika na kwa wakati kwa bidhaa hizo kwa kipindi chote cha mwaka, bila kujali mvua au jua. Huwezi kuwapelekea mchele Marekani mwezi wa 8 na wa 9 halafu wasubir tena miezi kama hiyo mwakani. Walmart hatakubali kuwa na supplier wa hivyo.
Mahitaji ya uwekezaji katika kilimo yanayoweza kukidhi vigezo hapo juu ni makubwa na ya muda mrefu kiasi ni ndoto za alinacha kama Serikali haitatia mkono wake tena kwa dhati. Hapo tunazungumzia uwekezaji wa miundombinu ya barabara, umwagiliaji, uhifadhi, usindikaji na masoko. Katika Dunia ya leo, private sector may not invest unless government invest, and invest wisely. Tanzania haijatumia kabisa fursa za Ardhi na rasilimali zake katika kuendeleza kilimo.
Nikiangalia trend ya graduates, vijana wetu, ukuaji wa idadi ya watu, maendeleo ya viwanda nk, nachelea kusema Serikali isipochukua hatua za haraka, za kijasiri na madhubuti kuwekeza katika kilimo, huenda hatutakuwa na Tanzania tunayoiona. Kwa bahati mbaya, kwa kipindi hiki sehemu kubwa ya maeneo yako wazi tu, hayana mpango wowote watu wanaota jua na kusubiri mvua ati wapande. Unfortunately, Serikali iko busy na yenyewe kusubiri mvua!!! This is a big joke katika mfumo wa maendeleo wa kileo ambao hauhitaji rocket science kubadilisha hali hiyo, kwani kila kitu kipo. Serikali iweke mkakati wa kuhakikisha kuwa hakuna kipande cha Ardhi Tanzania ambacho hakichangii katika ukuaji wa uchumi. Au hakuna rasilimali yoyote Tanzania ambayo haichangii katika ukuaji wa uchumi.
Majaribio kuwaza, kwa mfano, kiasi cha pesa kinachotumika kujenga SGR au mradi wa umeme, Serikali ikijipanga kiasi cha pesa kama hicho kuwa injected kwenye miradi ya kilimo, hii nchi itakuwa na uwezo wa kushindana na mataifa makubwa na kupiga maendeleo kwa haraka. Hali ilivyo kwa sasa ni kama hakuna maana ya kuwa na ardhi tuliyonayo wala rasilimali tulizonazo. Ni sawa kama Rwanda tu au Burundi! Why do we have all these resources but cannot be utilized to solve our problems?
Ushauri.
Serikali ianzishe WAKALA wa maendeleo ya kilimo (Agriculture Development Agency, ADA). Wakala huu pamoja na mambo mengine uwe na majukumu yafuatayo:
1. Kutafuta na kubainisha maeneo ya kilimo na mazao pendekezwa kwa kila eneo nchi nzima; ili kuwezesha hili kuna maeneo lazima yatwaliwe kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kuwajumuisha kama wanufaika kwa maana kuna maeneo watu Wana vijishamba vidogo. Hawa waunganishwa ama wafidiwe na eneo husika kuwekwe block ya mashamba yaliyoendelezwa;
2. Kuendeleza maeneo tengefu ya kilimo kwa kujenga miundombinu ya kilimo kuanzia barabara za kutoka mashambani, mifumo ya umwagiliaji, maghala ya kuhifadhia, maabara za kilimo na vituo vidogo vya usindikaji wa mazao husika;
3. Kutangaza/kuhamasisha fursa kwa wananchi kwenda kukodisha katika maeneo ya kilimo yaliyoendelezwa ( yaani kuwa na mfumo wa kielectroniki wa kuomba kukodi maeneo ya kilimo yaliyoendelezwa kama wanafunzi wanavyoomba loan board);
4. Kuwa wakala/ kiunganishi kikuku baina ya wakulima na Taasisi za kifedha ili wakulima wanaokodi mashamba yaliyo katika miundombinu yao waweze kukopeshwa fedha za kumeneji mashamba yao.
5. Kusajili na kusaidia uendelezaji wa mashamba binafsi kwa njia ya mkopo au ruzuku wa kuwajengea miundombinu. Mathalan, wakala wanaweza kuchimba visima vya umwagiliaji, kumjengea ghala na kufunga mashine za kuchakata mazao kwa kuzingatia takwa la ukubwa wa eneo alilonalo na mkulima kurudisha gharama kidogokidogo;
6. Kusimamia na kujenga mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji tu.
7. Kusaidia katika udhibiti wa ubora wa mazao na idadi kwa kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa zinakidhi mahitaji ya soko (quality and quantity).
8. Kuunganisha wakulima kutoka katika maeneo hayo yaliyoendelezwa na masoko ya uhakika ya nje na ndani.
9, 10, .... Majukumu mengineyo.
With time, wakala huu ataweza kujiendesha mwenyewe na hatategemea pesa kutoka Serikali Kuu kwani naamini watapa pesa nyingi kutoka kwa watakaowakodisha au kutumia huduma zao. Pia naamini Serikali ikifanya hivi, kwa ukubwa wa ardhi ya Tanzania ambapo mazao karibia yoooote duniani yanaweza kuzalishwa, hadithi za njaa zitabaki historia na tutaweza kutengeneza ajira nyingi kwa vijana wetu.
Anyway, mambo ni mengi na muda hautoshi. Wacha nilale kesho nimtumikie beberu huku. Alamsiki