Mkwere kishasema anategemea misaada hata alipokuwa Iringa alipokea simu kutoka NY kwa balozi kuhuhakikishia kuwa TZ misaada ni bwerere kutoka US. Kwa hiyo Kigoma kuwa Dubai, Viwanja vya ndege 3, Meli 3, Madalaja, laptop kwa kila mwanafunzi, barabara ya lami kuunganisha mikoa na...........................!!! Obama na hao wafadhiri anaowazungukiaga washatuhakikishia.
Kuhusu Slaa, yeye kasema ataongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato, atapunguza gharama za matumizi, no more mashangingi, pesa zinazonufaisha wachache kama za EPA, kujenja mahekaru ya BOT zitawafaidisha wananchi wote, mishahara na marupurupu ya wabunge vitalipwa kutokana na mapato ya taifa, mapato kutoka kwa wawekezaji kwenye migodi yetu ataongezeka kutoka 3% ya sasa mpaka 30+ %, Safari za matanuzi nje ya nchi na kubembea ughaibuni kama ilivyokuwa awamu ya nne hazitakuwepo, Ndege ya Rais haitatumiwa na mkewe, Urais hautakuwa wa familia na marafiki, Party ikulu kwa marafiki, Miss Wilaya, Miss Mkoa, Miss TZ, waburudishaji........................marufuku ikulu. Waimba kwaya na mashiri ni uwanjani siku ya sherehe za kitaifa. Kukutana na akina Drogba, kwenda Real Madrid, England kuangalia mpira hiyo haitakuwa sehemu ya kazi za rais wenu..................................!!!! Nafikiri mpaka hapo ushajua pesa za elimu na afya bure zitapatikanaje.