Ahadi ya msaada wa fedha kutoka nchi zilizoendelea kwa nchi zinazoendelea haitoshelezi mahitaji ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Ahadi ya msaada wa fedha kutoka nchi zilizoendelea kwa nchi zinazoendelea haitoshelezi mahitaji ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) umefungwa hivi karibuni huko Baku, mji mkuu wa Azerbaijan, na nchi mbalimbali zimefikia makubaliano kwamba, nchi zilizoendelea zitatoa angalau dola bilioni 300 za Kimarekani kila mwaka hadi mwaka 2035, ili kuzisaidia nchi zinazoendelea katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Dola bilioni 300 za Kimarekani kwa mwaka zinaonekana kuwa nyingi, lakini tafiti zimegundua kuwa nchi maskini zinahitaji dola trilioni moja za Kimarekani kwa mwaka ili kukabiliana na kupanda kwa kina cha bahari na hali mbaya ya hewa kama vile dhoruba, ukame na mafuriko, na fedha hizo zilizoahidiwa na nchi tajiri hazitoshi kabisa.

Aidha, utekelezaji wa makubaliano hayo unakabiliwa na hali ya sintofahamu. Rais mteule wa Marekani Donald Trump anakaribia kurejea Ikulu ya White House. Mara nyingi alidai mabadiliko ya tabianchi ni uwongo, na hata alipokuwa rais wa Marekani, alitangaza kujitoa katika Makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya Kukabiliana na Mabadilio ya Tabianchi. Ikiwa ushiriki wa Marekani utapungua katika siku zijazo, itakuwa vigumu kwa nchi zilizoendelea kutimiza ahadi yao ya kutoa fedha hizo kwa nchi zinazoendelea.

Nchi nyingi zinazoendelea zililegeza msimamo wao, na kupunguza matarajiao yao kupata fedha hadi dola bilioni 500 za Kimarekani, lakini hata hivyo zilishindwa. Wajumbe kutoka nchi hizi wamelaani mkutano huo kwa kufikia “makubaliano dhaifu yasiyo na nia thabiti”. Mwenyekiti wa Muungano wa Nchi za Visiwa Vidogo Cedric Schuster alijiondoa kwa hasira kutoka kwa mkutano huo. Alisema visiwa hivyo vinazama. Inawezekanaje kutarajia wao kurejea nchini mwao na makubaliano dhaifu kama hayo?

Katika hotuba yake wakati wa kufunga mkutano huo, mwakilishi wa China pia alisisitiza kwamba ahadi za fedha za nchi zilizoendelea ziko mbali sana na kukidhi mahitaji ya nchi zinazoendelea. Majukumu ya kifedha ya nchi zilizoendelea katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lazima yatekelezwe vizuri zaidi.

Nchi za Afrika pia zimelaani vikali makubaliano hayo. Ikilinganishwa na kanda nyingine, hasa nchi zilizoendelea, utoaji wa hewa ya kaboni barani Afrika umekuwa katika kiwango cha chini zaidi duniani. Lakini nchi za bara hilo ndizo zimeathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi, ambapo majanga ikiwemo ukame, mafuriko, na mawimbi ya joto hutokea mara kwa mara, na kuleta hasara kubwa kwa watu wa bara hilo.

Mkurugenzi wa Jopo la Washauri Bingwa la Afrika African Powershift anayeshughulikia masuala ya nishati na hali ya hewa Mohamed Addo amesema, mkutano huo ni janga kwa nchi zinazoendelea, na nchi tajiri zimesaliti binadamu na sayari ya dunia.

Mjumbe wa Sierra Leone amesema dola bilioni 300 za Kimarekani ni chini ya robo ya kiasi cha fedha zinazohitajika na hazitoshi kuzuia maafa ya mabadiliko ya tabianchi. Nchi za Afrika zimekatishwa tamaa na makubaliano hayo, ambayo yanaonesha ukosefu wa nia njema ya nchi zilizoendelea kwa nchi zinazoendelea.
 
Kwa waafrika wakipewa hela wanasema tumepandia miti ingawa ni wajibu wetu kulinda misitu yetu
Waache wachapishe tu hayo makaratasi yanayoitwa hela halafu watupe ila wao wabaki kututawala kifikra na kutuuzia kila kitu kwa hela walizozichapisha

Wake up you @%#♧♧
 
Back
Top Bottom