Pre GE2025 Ahadi za Watiania nafasi ya Ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Ahadi za Watiania nafasi ya Ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakati tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu ambako pia wananchi watapata nafasi ya kuchagua wabunge watakaowawakilisha kwa miaka mingine 5, tunashashuhudia viongozi wakianza kutangaza nia na kuahidi mabadiliko wakipata nafasi.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Uzi huu utakuwa maalum kwaajili ya ahadi zanazotolewa na watiania kwenye nafasi ya ubunge, wakati wa utekelezaji (endapo watachaguliwa na wananchi) itakuwa rahisi kuona kama ametekeleza aliyoahidi au lah.
 
Mgombea ubunge hapaswi kutoa ahadi yoyote kwa wananchi. Kwasbb mbunge hana fungu la fedha analotengewa na bunge (vote). Hivyo ni ulaghai kwa mgombea ubunge kuahidi kuwa atajenga barabara, daraja, ama kuleta maji ktk Jimbo
 
Kwa hiyo nini yatakuwa maono ya mbunge kwa miaka 5 ijayo
 
Wakiwa wanaomba kura ahadi kibao ILA wakushapata hugeuka na kusema Mbunge hana hela
 
Kwa hiyo nini yatakuwa maono ya mbunge kwa miaka 5 ijayo
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi, yeye ni mpokeaji wa malalamko na maoni ya wananchi na kuyawasilisha serikalini ama kuyasemea bungeni. Mbunge hapaswi kubeba mawazo ama maono yake binafi, kwani kufanya hivyo itakuwa ni kujimwambafai na kukiuka misingi ya uwakilishi
 
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi, yeye ni mpokeaji wa malalamko na maoni ya wananchi na kuyawakilisha serikalini ama kuyasemea bungeni. Mbunge hapaswi kubeba mawazo ama maono yake binafi, kwani kufanya hivyo itakuwa ni kujimwambafai na kukiuka misingi ya uwakilishi
Kwa hiyo waliwakilisha maoni au matarajio ya wananchi pamoja na Raisi
 
Back
Top Bottom