Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
"Kikosi kwa sasa kinaendelea na programu ya mazoezi kikijiandaa na mchezo dhidi ya Pamba. Leo usiku tutaondoka kwenda Mwanza na wachezaji wanne waliokuwa Taifa Stars na Camara aliyekuwa timu ya taifa ya Guinea wameshajiunga na kambi. Steven Mukwala atawasili Dar kesho alfajiri na kuunganisha kwenda Mwanza."
"Kesho tukiwa Mwanza tutatembelea Kituo cha Kutunza Watoto Yatima cha Ilemela kurudisha kwa jamii. Wanahabari tutaondokea benki ya NBC kesho saa 4 asubuhi baada ya mkutano wa wanahabari ambao kocha na mchezaji watazungumza."
"Mchezo dhidi ya Pamba ni muhimu mno kushinda sababu utatupa ujasiri kuelekea mchezo dhidi ya Bravos. Nichukue nafasi hii kuwambia mashabiki wetu wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwamba waangalie Pamba kama mpinzani wetu mgumu kwa maana hiyo wafanye maandalizi makubwa ya kwenda kumuangamiza Pamba. Tunahitaji ushindi huo."
"Hakuna uzalendo kwa watu wa Mwanza kwenye mchezo huo, tusiposishinda itakuwa faida kwa watu wengine. Tusimame kwanza na Simba na uzalendo utarudi baada ya kushinda. Hata uwe nani simama na Simba yako, hii vita sio ya Pamba wao wametumwa tu."
"Baada ya mchezo dhidi ya Pamba usiku huo huo wa Ijumaa tutarudi Dar. Tarehe 23 tutakwenda Kituo cha Kutunza Watoto Yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni, Dar es Salaam. Wanasimba siku hiyo mjitokeze kwa wingi kwenda kutao msaada. Ukifanya mema na Mungu anakulipa mema na mema yetu ni kuwafunga Pamba na Bravos."