Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Meneja wa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amewasilisha ujumbe wa pole kwa mashabiki wa klabu hiyo kufuatia kuahirishwa kwa mechi yao leo.
Kupitia taarifa yake, Ahmed Ally ameomba radhi kwa mashabiki wote wa Simba, hususan wale waliotoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo. Ameeleza kuwa uamuzi uliofanywa na viongozi wa klabu ni kwa maslahi ya timu na mpira wa miguu kwa ujumla, hivyo mashabiki wanapaswa kuupokea kwa utulivu.
Soma: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
Aidha, amewasihi mashabiki waliokuwa tayari wamefika uwanjani kurejea nyumbani kwa utulivu ili kuwahi futari, huku akiwatakia safari njema wale wanaorejea mikoani.
Ahmed Ally amesisitiza kuwa licha ya kuahirishwa kwa mechi hiyo, mashabiki wa Simba wasikate tamaa kwani, kwa mujibu wa ujumbe wake, "haki imeshinda."