Ahmed Ally: Simba hatuna cha kujivunia sana maana hatujapata tulichokihitaji

Ahmed Ally: Simba hatuna cha kujivunia sana maana hatujapata tulichokihitaji

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Screenshot 2023-06-13 at 12-02-37 Ahmed Ally on Twitter.png

Tuzo zilizotolewa jana zimehitimisha rasmi msimu wa 2022/2023 Tuwapongeze waliotwaa Ubingwa na waliopata Tuzo, Na kwa kipekee kabisa tuwapongeze wasimamizi wa ligi pamoja na waaandaji wa Tuzo.

Kwetu Simba tuwapongeze nyota wetu waliotwaa tuzo hakika wametuheshimisha Kiujumla kama timu hatuna cha kujivunia sana maana hatujapata tulichokihitaji msimu huu Hii inatupa nafasi ya kujipanga zaidi kwa msimu ujao Ubingwa unahitaji wachezaji bora na timu imaraNi jukumu letu viongozi kutafuta wachezaji sahihi na kutengeneza timu madhubuti.

Na hilo limeshaanza kufanyika kwa umaridadi wa hali ya juu sana Kiu na shauku kubwa ya Wana Simba ni kuona mataji yanarejea kwenye timu yao kwani wamechoka kelele za jiraniTimu kubwa kama Simba haipaswi kukaa muda mrefu bila mataji, miaka miwili inatosha ni muda sasa wa kurudisha ufalme na wetu

Simba sc.jpeg
 
Kwa hiyo anapingana na mwenyekiti wake Murtaza Mangungu aliyethibitisha kujivunia mafanikio ya kuifunga Yanga kwenye ile mechi ya mzunguko wa pili wa ligi!
 
Huyu jamaa kipindi kigumu anapambana peke yake, wengine wamenyuti.
 
Back
Top Bottom