Ahmed Ally: Simba imepungua ubora

Ahmed Ally: Simba imepungua ubora

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
“Simba imepungua ubora kidogo, lazima tuwe wakweli. Kwanza kuna nyota wetu ambao ubora wao umepungua kidogo kwa sababu ya kuchoka, wamefanya kazi kubwa kwa miaka 5, wamecheza sana kwa miaka yote hiyo michuano ya kimataifa, Ligi kuu na michuano mingine”

Ahmed Ally
Ahmed-Ally-Jukwaani.png
 
Mimi sikubaliani na hilo sema wachezaji wengi umri umekwenda sanaaaaa, timu za ulaya zinacheza kila kukicha mbona hawatoi sababu za kitoto hivyo? Tatizo la simba mnang'ang'ania wachezaji wale wale kila siku. Mnawaita wenye simba yao hawaguswi. Bocco kachoka, mkude, mzamiru, shabalala, tibazonkiza,onyango yaani karibu wachezaji wote umri umeenda, wenzenu wanawekeza kwa vijana nyinyi mnawekeza kwa wazee hii ndo shida yake.
 
Wachezaji ulaya wanacheza kwa kupenda
 
Kama wamechoka sasa, si wapumzike/wastaafu kucheza mpira wa ushindani! Imagine mtu kama Erasto Nyoni mpaka leo bado anacheza tu mpira!

Wenzake akina Aggrey Morris, Shaaban Nditi, Mussa Hassan Mgosi, Awadh Juma, na wengineo wengi wamehamia kwenye ukocha! Yeye bado ana mkataba na simba! Halafu wakati huo huo watu wanataka maajabu! Yatoke wapi?

Angalia kikosi cha Yanga! Kimesheni vijana wengi! Hivi hata sikumbuki kama kuna mchezaji mwenye umri mkubwa, baada ya Saido Ntibazonkiza kuondoka.
 
Na msimu kesho tusubiri visingizio? Au vitaishia msimu huu.
 
Simba ipo kwenye recession, ila wanaweza kurejea kwenye ubora wakijipanga vyema.
 
Hayo ni maneno ya hizi mechi tatu tu. Akishinda kwa Vipers, atakuja kuongea shombo na vile vicheko vyake vya kinafiki…!!!
 
Sasa hata kama akiishinda Vipers ataenda wapi wakati kashadondosha point 6 o'clock!
 
Mimi sikubaliani na hilo sema wachezaji wengi umri umekwenda sanaaaaa, timu za ulaya zinacheza kila kukicha mbona hawatoi sababu za kitoto hivyo? Tatizo la simba mnang'ang'ania wachezaji wale wale kila siku. Mnawaita wenye simba yao hawaguswi. Bocco kachoka, mkude, mzamiru, shabalala, tibazonkiza,onyango yaani karibu wachezaji wote umri umeenda, wenzenu wanawekeza kwa vijana nyinyi mnawekeza kwa wazee hii ndo shida yake.
Una umri gani?
Huoni kuwa ameongea koutu uzima kwamba simba ina wazee wamechoka?
 
Back
Top Bottom