Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Nimekuwa nikikufuatilia kama Refa unayeheshimika nchini Kwa vile umevaa beji ya heshima.
Lakini tofauti na matarajio yangu Mechi zote unazochezesha umekuwa huitendei haki BEJI kubwa uliyovaa.
Siongelei ushabiki lakini Kwa mwenye kumbukumbu, Kila unapolaumiwa huwa nakomenti kutokuwa na imani na wewe.
Nichukilie mfano wa Mechi ya jana Yanga Vs Namungo. Ni Mechi ambayo wengi tulitegemea ufute makosa na Lawama Kwa sababu ulipangwa kutokana na umaarufu wako ikitegemewa ungeweza kudhibiti pressure ya mchezo.
Lakini Kwa masikitiko ya wengi ukabebwa na pressure ya mchezo na kushindwa kutoa maamuzi sitahiki Katika matukio mengi.
Hebu tueleze Sisi marefa wenzio ni sababu ipi ilipelekea utoe Onyo la mdomo Kwa beki Magingi wa Namungo Kwa mchezo wa hatari Kwa shambulio la kutokea nyuma (attacking from behind) alilofanya dhidi ya Mayele wa Yanga?
Ni vema baada ya Mechi uwe unaangalia marudio ya Mechi ili uone unavyoboronga kwenye michezo mingi ili ujirekebishe. Najua ni kazi kumtrain mwamuzi mpaka kufikia hadhi yako, lakini ulipofikia unatakiwa kupatendea haki.
Kila mwaka baada ya ligi kumalizika hutolewa tuzo Kwa waliofanya vizuri kwenye ligi wakiwemo Waamuzi Bora.
Mwaka Jana nilifurahia kuona tuzo ya "Couple Bora ya Waamuzi". Nadhani mwaka huu wataongeza kipengele cha "Couple Mbovu ya Waamuzi" na nitafurahi Waamuzi wa Mechi ya jana Yanga Vs Namungo wakibeba tuzo hiyo.