Ahsante Mungu, wife amejifungua salama

Kwani kupata mtoto ni big deal, mi kila siku navikataa hivyo vi-kid. Sasa naona kuna umuhimu wa kuanzisha Jukwaa la UJAUZITO NA KUJIFUNGUA. Siyo kila kitu lazima kije hapa, mwisho mtaanza kupost mpaka chakula mnachokula sasa.

mibaba mingine hata haistahili kuitwa baba. sasa we kuvikataa hivo vitoto unaond deal eeh. afu vikitupwa majalalani mnasema wanawake wakatili kumbe nie ndo chanzo.

wengine wanashinda kutwa kucha wakililia baraka hizi za watoto afu we unasema nini agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr

hongera kaka jojipoji kwa kupata kababy bana. hebu mbarikiwe sana.
 
Hongera Mkuu
Habari za zenj? Waifu akishapona ni pm nije nikupe hongera.
 
Salam wadau,
Ijumaa ya leo imekuwa ya furaha sana baada ya wife kujifungua salama mtoto wa kiume

hongera Mkuu, Umepata wa kumkabidhi mikoba

Hongera Sana Mkuu!!

Hongera kwa kuleta dume la mbegu, Mungu akukuzie.

hongera sana mkuu kwa kuijaza dunia.

Kwani kupata mtoto ni big deal, mi kila siku navikataa hivyo vi-kid. Sasa naona kuna umuhimu wa kuanzisha Jukwaa la UJAUZITO NA KUJIFUNGUA. Siyo kila kitu lazima kije hapa, mwisho mtaanza kupost mpaka chakula mnachokula sasa.

hongera mkuu!

Mungu awape afya njema mama na mtoto... Mungu awajalie pia hekima na busara mumlee vema!

Siku hizi ukiwa mjamzito na ukajifungua salama ni bahati ndugu yangu, Joji amefurahia hiyo bahati so akaona si vibaya kushea furaha yake na memba wenzie... Wanawake wanakufa sana wakat wa kujifungua...

Jojipoli
Hongera sana mkuu na
samahani hapo juu

Mambo swahiba?
Hivi kumbe hata wewe wakasirikaga hv?... Msamehe bure huyu manake hajui alinenalo... Kuna siku atavikumbuka hvyo vi kid bt itakuwa too late...

hongereni.

Hongera sana na mungu azidi kuwabariki mkapate kumlea vyema kijana akapate kukua na kuwa raia mwema na mpiganaji.

Matusi uliyotukana mi namwachia Mungu tu, maandiko yananiambia nisamehe saba mara sabini. Malaika wa Mungu wata-deal na wewe tu, we subiri adhabu tu!

Mshukuru Mungu kwa kila jambo.
Hongera

Hongera sana kaka..
naomba nipendekeze jina la mtoto: Eben-ezer/Ebeneza/Ebenezer/Ebenezeri...spelling yoyote utakayopenda.
Soma: 1Samuel 7:12

Ahsante ndugu nitalifanyia kazi

wazo tu
kumbuka muwe mnajitahdi kusali sana sana usiku ,,utaona usiku mambo makubwa watoto wanayaona we huoni soln ni maombi ya kufululiza
mpaka kanalala na sio kulia

Unafiki mtupu.. Eti Malaika wa Mungu wata -deal na mimi..Na hao malaika ambao we unawakata ..Wata deal na nani...Usijifanye mtakatifu naomba..

Hongera sana mkuu.. Mwenyezi Mungu amjalie mama na mtoto afya njema!

hongera sana mkuu , 01/07/2011 tarehe nzuri sana ya siku ya kuzaliwa

nawatakia afya njema mama na mtoto

Hongera sana Mungu awajalie afya njema.

Hongera saaaaana kwenu wote,mleeni mtoto katika njia impasayo yaani amjue Mungu wa kweli

Hongera Kwako, Mpe Pole na Hongera my wife wako.

hongeara zenu sana! Namtakia mtoto afya njema na makuzi bora!

mpe jina langu Edson....

Kubeba mimba na kujifungua salama ni jambo jema na la kumshukuru Mungu!..Hongereni sana wazazi wapya! Malezi mema na welcome to the parenthood!!

Majina mengine bana...hivi hilo lina maana gani!?? ama ni just for purposes of classification!??lol

...na baba! (malizia mkuu)

Hongera sana baba. Mtunze vyema jojipoji jnr...

Sweetlady umenena ukweli mtupu! Jojipoji ana kila sababu ya kuonyesha furaha yake hapa.Maana siku hizi ukiwa mjamzito ni kama unatembea na kifo.Hongera sana Joji!!!!!!!!!

Hongera mkuu,
mi mwenyewe Mungu akipenda soon! Endelea na maombi

Hongera sana!

Trh 1 July duh? Mzee ulicheza vyema na trh za mwanzo, mwanao atakua mfanyabiashara!

Hongera sana..

Kaonane na daktari wa magonjwa ya akili asap!

hongereni na Mwenyezi Mungu awaajalie kwa hali na mali mkalee vizuri....kabinti kangu keko eti!

Ndugu zangu ahsanteni sana, kwa kweli nimefarijika sana
 
Hongera zenu na kila la heri katika malezi.
 
Hongora sana Jojipoji hii ni habari njema kwa familia yako na kwetu pia
 
Siku hizi ukiwa mjamzito na ukajifungua salama ni bahati ndugu yangu, Joji amefurahia hiyo bahati so akaona si vibaya kushea furaha yake na memba wenzie... Wanawake wanakufa sana wakat wa kujifungua...
kweli ni jambo la kumshukuru mungu.
 
Ndugu zangu ahsanteni sana, kwa kweli nimefarijika sana

Hakikisha unampunguzia kazi wife wako kazi kama kufua, kupika, kuosha vyombo kwa kufanya wewe mwenyewe kwa miezi 3
 
Hongera sana
Mungu amlinde na kumjalia afya njema pamoja na familia yako
 
Ha ha ha ha ha ha leo umeniwahi nilitaka kutapika haya haya
 
Matusi uliyotukana mi namwachia Mungu tu, maandiko yananiambia nisamehe saba mara sabini. Malaika wa Mungu wata-deal na wewe tu, we subiri adhabu tu!
Acha unafiki eti Malaika? Na hao unaowakataa ni nani? Kuwa na adabu kijana
 
Hakikisha unampunguzia kazi wife wako kazi kama kufua, kupika, kuosha vyombo kwa kufanya wewe mwenyewe kwa miezi 3

Siku hizi wote wanapewa leave ya siku tatu nasikia...so kwa SIKU TATU TU ndo anaruhuiwa kufanya uyasemayo!
Ila vijana wengi wa siku hizi hizi kazi hawazijui..i doubt kama zitafanyika kweli!!!
 
Siku hizi wote wanapewa leave ya siku tatu nasikia...so kwa SIKU TATU TU ndo anaruhuiwa kufanya uyasemayo!
Ila vijana wengi wa siku hizi hizi kazi hawazijui..i doubt kama zitafanyika kweli!!!

Inabidi amsaidie sana kwa kweli ili atoe maziwa mengi
 
lakin mkuu hii habari ya heri mkuu. mtu amevuka kifo hapo.kulikuwa na mawili..kifo au uhai. kwa wote au kwa mmojawapo sio vibaya kuwashikirikisha JF members. Ndio maana ikapewa jina la Jamii.

Kwani kupata mtoto ni big deal, mi kila siku navikataa hivyo vi-kid. Sasa naona kuna umuhimu wa kuanzisha Jukwaa la UJAUZITO NA KUJIFUNGUA. Siyo kila kitu lazima kije hapa, mwisho mtaanza kupost mpaka chakula mnachokula sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…