Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba

Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mahakama ya wilaya ya Kilombero imemhukumu Yegela Juma Mfula (22) mkulima, mkazi wa Lungongole kifungo cha miaka 30 Jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la 7 (jina limehifadhiwa) wa shule ya msingi Lungongole, kata ya Kibaoni wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya wilaya Kilombero, Regina Mfutakamba amesema kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo Machi 3, 2024 majira ya saa nne asubuhi baada ya kumfuatilia kwa nyuma mtoto huyo aliyekuwa ametumwa dukani kununua maziwa na alipofika eneo lenye uchochoro alimvamia na kumpeleka kwenye migomba kisha kutekeleza azimio lake la kumbaka.

Soma pia: Mbeya: Kijana wa Miaka 17 ahukumiwa kifungo cha nje Miezi miwili kwa kumbaka Mwanafunzi

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amesema kuwa Serikali hususani Jeshi la Polisi linamkono mrefu na asitokee yeyote kujidanganya kuwa atakayefanya vitendo vya ukatili na asikamatwe, huku akibainisha kuwa Polisi watamfikia mhalifu wa aina hiyo hata akitorokea mkoa mwingine.

Aidha, SACP Mkama amewashukuru wananchi kwa kuchukizwa na uhalifu na kuisaidia Polisi kutoa taarifa za wahalifu na ushahidi Mahakamani baada ya kukamatwa kwao.

Screenshot 2024-11-26 165047.png
 
Back
Top Bottom