Aibu bungeni...elimu tanzania ni hohehahe hoja ya mbatia yahitimishwa kienyeji

big f

Member
Joined
Nov 26, 2012
Posts
60
Reaction score
17
Wana jamvi najitokeza kutoa hoja hii juu ya umbumbumbu mkubwa uliooneshwa na ukada na ushabiki wa kizembe uliooneshwa na bunge letu hii leo asubuhi, wakati Mheshimiwa James Mbatia akitakiwa kuhitimisha hoja yake binafsi juu ya Udhaifu mkubwa uliopo katika sekta ya elimu nchini. Mheshimiwa James Mbatia kwa taarifa yake ametumia miaka kumi na nane kufanya utafiti na kuibuka na hoja hii binafsi, lakini cha kusikitisha hoja na utafiti wake vimepuuzwa na naibu spika Ndugai, binafsi nimesikitishwa sana na uamuzi pofu wa Job Ndugai. Hii imethibitisha wazi kwamba nchi hii inaendeshwa bila kuwa na MTAALA RASMI kama alivyosema Mheshimiwa Mbatia kwa miaka yote hii. Taarifa za uhakika ni kwamba Mitaala rasmi ya mwaka 2005 iko katika hatua ya rasimu ambayo ilichapishwa mwaka 2012 yaani mwaka jana kwa maana hiyo kile ambacho waziri wa elimu anakiita mitaala rasmi ni rasimu ya mitaala hiyo na si mitaala yenyewe. Kwa kuanzia sharti tujiulize maswali haya;
Hivi Elimu ya nchi hii tunaipeleka wapi (Waziri wz Elimu na Watendaji wake)? Hoja nzuri na ya msingi kama ya Mheshimiwa James Mbatia ni halali kuhitimishwa kiuzembe namna ile? Kwa nini waziri wa elimu hajalieleza bunge ukweli kuwa kilichopo ni rasimu ya Mitaala rasmi na si mitaala kamili? Hivi ni kweli nchi hii haina mitaala rasmi, kama ipo kwa nini wanaweka siri kubwa juu yake kwani kuna uozo gani huko kwenye hiyo mitaala? Hivi kuna ugumu gani uliomfanya waziri wa elimu kushindwa kuwasilisha mitaala hiyo bungeni kama alivyoahidi katika bunge lililopita? Kwa nini waziri ameshindwa kumkabidhi mtoa hoja japo ile mitaala miwili anayoionesha bungeni au hata kumkabidhi Naibu Spika au alishika vitabu vyake vya hadithi na kuvionesha juu kumbe si mitaala? Kama wanayo hiyo mitaala rasmi kwa nini wamegwaya kuileta bungeni tangu mwaka jana na wanaendelea kutoa ahadi kwamba italetwa kabla ya kabla ya bunge kuahirishwa tarehe 8? Kama waliahidi, hawajatekeleza tuwaamini vipi kwamba wataleta hiyo mitaala kabla ya tarehe 8/2/2013? Je, ahadi zao za Kijuha kama hizi wataendelea nazo mpaka lini kwani hata mheshimiwa rais JK mwenyewe ameingia katika ahadi hewa kwamba walimu wataajiriwa tarehe 13/01/2013 ahadi ambaya haijatekelezwa hadi leo au alimaanisha tarehe hiyo ya mwaka 2014? Uongo na uzembe huu mwisho wake lini? Hii nchi ni bora ya Giningi, Kusadikika na Kufikirika. Haya yanayoendelea ya kukumbatia uozo ni aibu kubwa na bomu lililolipuka tayari kwa matokeo mabovu katika mitihani yooote ya taifa.
 
inashangaza sana inaonekana viongozi hii elimu yetu hawaipi kipaumbere,na ndio maana watoto wa vigogo wanasoma ng,ambo,sijui tumemkosea nini mungu sisi WADANGANYIKA.
 
Hata mimi ningempuuza Mbatia, kazi ya mbunge ni kuwawakilishi wananchi wake. Yeye si mbuge wa wananchi, zaidi zaidi ni Mbunge anayetumikia tumbo lake..!
 
Elimu ni msingi wa maendeleo katika kila jamii, ni kama msingi na muelekeo wa taifa husika. siasa mbovu ktk nchi yetu ipo katika kila nyanja si elimu tu. Swala la msingi ni wananchi kuchukua hatua katika kulitetea na kutafuta ufumbuzi wa kina. ni vema sasa kuacha kulalamika kwenye mitandao bali ni kuchukua hatua madhubuti kwa kauli na msimamo mmoja chini ya imani ya kutaka kuleta mabadiliko.
 
Hata mimi ningempuuza Mbatia, kazi ya mbunge ni kuwawakilishi wananchi wake. Yeye si mbuge wa wananchi, zaidi zaidi ni Mbunge anayetumikia tumbo lake..!

Mungu akusamehe maana hujui unenalo!! Je, mwananchi yeyote yule hana haki ya kuhoji na kuchangia mambo anayohisi hayaendi vizuri katika nchi yake? Mbatia ni mheshimiwa mbunge, mwenyekiti wa nccr mageuzi na mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na hii ni kwa mujibu wa katiba.
 
Khaaaaaa hivi wewe ni member wa JF, Mungu wangu saidia hii mutu. Hoja ya elimu inagusa kila mtu hata kama wewe una uwezo wa kupeleka watoto shule za saint, vipi watoto wa ndungu, kizazi cha mlala hoi hata huwafikilii.
 
Ni hasira tu mkuu wangu juu ya madaraka ya rais yalivyopitiliza, sasa wale aliowateua kiana hata wakiongea point inakuwa ngumu kumesa.
 
Khaaaaaa hivi wewe ni member wa JF, Mungu wangu saidia hii mutu. Hoja ya elimu inagusa kila mtu hata kama wewe una uwezo wa kupeleka watoto shule za saint, vipi watoto wa ndungu, kizazi cha mlala hoi hata huwafikilii.
Ni hasira tu mkuu wangu juu ya madaraka ya rais kupiliza, inafikia point hata mtu akiongea point hatukubali kisa aliteuliwa kiaina na rais..!
 
Bunge zima hawana akili walisusia kikao cha asubuh jioni wakarudi cjui wanafikiria nini (kambi ya upinzani)?
 
Hawakususia kkao walitoka nje kujadliana juu ya utendaj wa spka na naib wke jins wanavyozika hoja za upnzan
 
Hata mimi ningempuuza Mbatia, kazi ya mbunge ni kuwawakilishi wananchi wake. Yeye si mbuge wa wananchi, zaidi zaidi ni Mbunge anayetumikia tumbo lake..!

Hapana unakosea alkua na hoja mcng pitia
www.mwananchi.co.tz(mpy)
 
Aiseeeeee babayangu ngoja nikazane kulima na kuuza ndizi nimpeleke mwanangu nairobi akasome elimu ya uhakika kama wizara ya mwakyembe
 
Wana jamvi najitokeza kutoa hoja hii juu ya umbumbumbu mkubwa uliooneshwa na ukada na ushabiki wa kizembe uliooneshwa na bunge letu hii leo asubuhi, wakati Mheshimiwa James Mbatia akitakiwa kuhitimisha hoja yake binafsi juu ya Udhaifu mkubwa uliopo katika sekta ya elimu nchini. Mheshimiwa James Mbatia kwa taarifa yake ametumia miaka kumi na nane kufanya utafiti na kuibuka na hoja hii binafsi, lakini cha kusikitisha hoja na utafiti wake vimepuuzwa na naibu spika Ndugai, binafsi nimesikitishwa sana na uamuzi pofu wa Job Ndugai. Hii imethibitisha wazi kwamba nchi hii inaendeshwa bila kuwa na MTAALA RASMI kama alivyosema Mheshimiwa Mbatia kwa miaka yote hii. Taarifa za uhakika ni kwamba Mitaala rasmi ya mwaka 2005 iko katika hatua ya rasimu ambayo ilichapishwa mwaka 2012 yaani mwaka jana kwa maana hiyo kile ambacho waziri wa elimu anakiita mitaala rasmi ni rasimu ya mitaala hiyo na si mitaala yenyewe. Kwa kuanzia sharti tujiulize maswali haya;
Hivi Elimu ya nchi hii tunaipeleka wapi (Waziri wz Elimu na Watendaji wake)? Hoja nzuri na ya msingi kama ya Mheshimiwa James Mbatia ni halali kuhitimishwa kiuzembe namna ile? Kwa nini waziri wa elimu hajalieleza bunge ukweli kuwa kilichopo ni rasimu ya Mitaala rasmi na si mitaala kamili? Hivi ni kweli nchi hii haina mitaala rasmi, kama ipo kwa nini wanaweka siri kubwa juu yake kwani kuna uozo gani huko kwenye hiyo mitaala? Hivi kuna ugumu gani uliomfanya waziri wa elimu kushindwa kuwasilisha mitaala hiyo bungeni kama alivyoahidi katika bunge lililopita? Kwa nini waziri ameshindwa kumkabidhi mtoa hoja japo ile mitaala miwili anayoionesha bungeni au hata kumkabidhi Naibu Spika au alishika vitabu vyake vya hadithi na kuvionesha juu kumbe si mitaala? Kama wanayo hiyo mitaala rasmi kwa nini wamegwaya kuileta bungeni tangu mwaka jana na wanaendelea kutoa ahadi kwamba italetwa kabla ya kabla ya bunge kuahirishwa tarehe 8? Kama waliahidi, hawajatekeleza tuwaamini vipi kwamba wataleta hiyo mitaala kabla ya tarehe 8/2/2013? Je, ahadi zao za Kijuha kama hizi wataendelea nazo mpaka lini kwani hata mheshimiwa rais JK mwenyewe ameingia katika ahadi hewa kwamba walimu wataajiriwa tarehe 13/01/2013 ahadi ambaya haijatekelezwa hadi leo au alimaanisha tarehe hiyo ya mwaka 2014? Uongo na uzembe huu mwisho wake lini? Hii nchi ni bora ya Giningi, Kusadikika na Kufikirika. Haya yanayoendelea ya kukumbatia uozo ni aibu kubwa na bomu lililolipuka tayari kwa matokeo mabovu katika mitihani yooote ya taifa.

Big F, unajua hile mitaala iliyokuwepo wameichakachua kila kukicha.. unakumbuka yule waziri sijui nani Mkenya aliondoa somo la Kilimo... hivi hata michezo siku hizi hipo..UMISHUMITA NK.
 
Hata mimi ningempuuza Mbatia, kazi ya mbunge ni kuwawakilishi wananchi wake. Yeye si mbuge wa wananchi, zaidi zaidi ni Mbunge anayetumikia tumbo lake..!

Hakika kama akili ingekua ni kiungo basi wewe ungekua kilema
 
Hata mimi ningempuuza Mbatia, kazi ya mbunge ni kuwawakilishi wananchi wake. Yeye si mbuge wa wananchi, zaidi zaidi ni Mbunge anayetumikia tumbo lake..!

uwii wewe ni hanisi wa akili tena mbulula, yani hoja ya mbatia n utumbo sishangai hata kidogo coz akili za ndugai+makinda+kawambwa+mzee wa pemba mozambique(mlugo)+lukuvi.=na za kwako, so hata cshangai

nenda kawaambie magamba wenzako mwisho wenu n 2015.
 
Katika nchi hii wafuasi wa Cameroon hamnaga nafasi ya kuchangia mambo nyeti
 
Back
Top Bottom