So Ruvuma, Tanga, Morogoro etc kote mwendo RBG, na B/S for Mps??!..dah?! sijui zile za wilaya, Health Center, Dispensary ndio zikoje?!!
Wewe unashangaa Morogoro, sisi hapa Songea hospital ya mkoa ambayo ni rufaa sasa, haina X ray tangu miezi sita iliyopita, haina Ultrasound, kwa sasa wanafanya bs stool na rbg tu, imgeuzwa kuwa dispensary kubwa. Na haya si hapa tu bali ni hospital nyingi nchini. Mfano huku Songea tatizo halionekani coz ya hospital ya Peramiho ambapo huduma nyingi kwa mahitaji ya kitanzania zinapatikana.
Pesa ya kununua risasi za moto,mabomu ya machozi na maji ya kuwasha huwa hazikosekani lakini za kuhudumia wananchi hamna!
Baada ya miaka hamsini ya uhuru ni aibu sana kwa hospitali ya mkoa ya morogoro ambayo imepandishwa kuwa hospitali ya rufaa kukosa huduma ya X-RAY.
Kuna siku nikiwa kwenye daladala nilisikia mtu akilalamika kwa kitendo hicho ila sikuamini. Jana ndiyo niliamini baada ya mmoja wa kijana aliyejeruhiwa jana kushindwa kuhudumiwa kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.....