aibu kwa wanasheria TLS!

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Kwa Ujumla Yaliyomo Kwenye Tovuti Ya Chama Cha Wanasheria Nchini Tanzania (Tanganyika Law Society (TLS) Ni Aibu na yanachefua Kwa Wasomi Wa Sheria Ukilinganisha Na Taaluma Nyingine. Inaonekana Kana Kwamba Hakuna Sekretariate Makini Ya Kukisaidia Chama Hicho Muhimu Kwa Taifa.AU PENGINE CHAMA HAKINA UWEZO WA KIFEDHA KUWEZA KUJIENDESHA na KINAHITAJI MSAADA KAMA FEDHA ZA ADA ZA WANACHAMA HAZITOSHI????

Ukitembelea tovuti ya chama hiki www.tanganyikalawsociety.org.tz" utaona jinsi ilivyoingiliwa kama kwamba hakuna mtaalamu wa IT kwenye ofisi ya TLS au kama yupo halipwi vizruri.

Kwenye ukurasa wa mbele uingiatu tu unakutana na tangazo la zamani la "International Bar Assocaition Meeting YA Madrid, Tarehe 4 OKTOBA 2009".

Kwenye Links zote zilizoorodheshwa Hakuna Lolote Isipokuwa Matangazo Ya Mikutano Iliyopita Ya Wanachama.

Taarifa ambazo Mtukufu Rais wa TLS anataka wadau tuchungulie katika tovuti ya wanasheria hawa wa nchi yetu ni kama hizi:

HIVI WADAU KUNA LOLOTE PALE TLS????
 
Kwanza kabisa mimi naona hicho chama hakipo,mimi nilitegemea chama cha wanasheria kingekuwa mstari wa mbele kutetea masilahi ya nchi pale yanapokuja masuala ya mikataba mibovu,kwani hiyo mikataba huandikwa na wanachama wa chama cha wanasheria,pia nilitegemea hicho chama kuwa msitari wa mbele kuelemisha wananchi juu ya sheria za msingi za wananchi wa taifa hili pale upotoshwaji wa mambo unapotokea kama alivyopotosha waziri Chikawe na pia ningetarajia kuwa waelekezi kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya.Hiki chama kingejifunza kutoka chama cha wanasheria Kenya,ni aibu kwa chama cha wanasheria hapa Tanzania kukaa pembeni wakati mambo yanaenda kombo,wanasheria kwa kutokana na taaluma yao ni watu muhimu sana katika kuleta mabadiliko nchi hii,na si kushugulikia kesi za mahakamani tum
 
nachojua mimi wanayo programm ya legal aid ambapo wananchi wenye shida mbalimbali wasioweza kulipa mawakili wanasaidiwa kwenye kesi zao.
 

Kwa kawaida wanasheria huwa wanatakiwa wasiwe watu wa kutoa sweeping statements. Mimi sitaki kuwatetea hawa watu wa TLS kwa kuwa na website mbaya isiyoridhisha wala kuwa updated.

Sisi kama wadau wa sheria kwenye jukwaa hili tunajukumu la kuwakumbusha wenzetu kuwa wamejisahau.

Tusisahau kuwa kuna msemo wa No research no Right to Speak. Perhaps wana sababu kwa nini website yao iko vile. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na zifuatazo:
1. Pengine hawana mtu wa IT
2. Pengine wana mpango wa kutengeneza website mpya
3. Pengine mtu wao wa kuupdate website ni mzembe na hasimamiwi
4. so many other explanations.

My take is someone should take the lead and let them know.

Kuhusu suala la nini chama kinafanya mimi kama mwanachama wa TLS nikianza kusema nitakuwa biased. Nafikiri wanafanya vizuri sana ingawa bado chama kinaendeshwa kiubabe na watu walewale wa siku zote. Hakuna demokrasia ya kweli na vijana hawapewi nafasi/hawajitokezi kuonyesha uwezo wao.

Mimi ningeona ni vema tukamuomba mtu kutoka katika sekretariat ya TLS aje hapa jukwaani au ahojiwe atueleze ni kwa nini chama chao kimedorora (kama ni kweli).
 
kwi kwi kwi, muiteni bosi wao emilia, kwa jinsi alivo mbabe atawatoa spidi!
 
Ma lawyers are pretending to too busy to bother with little things!. Hawa ni the so called'Learned Brothers and Sisters'
 
Ma lawyers are pretending to too busy to bother with little things!. Hawa ni the so called'Learned Brothers and Sisters'


Pasco,


kama lawyers ni learned brothers basi taaluma imekufa na hicho chama kitakuwa ni "DANGANYIKA LOO SOSA HAYATI". Once upon a time Prof. Issa Shivji aliwahi kuwahasa kuwa "lawyers are Learning Brothers, rather than learned ones"., Mmepotea kwa kushindwa kujua uhalisia wa mambo, mjifunze kutoka kwa taaluma nyingine ili kuweza kujua kama kweli usomi wenu ni zaidi au lah kwa nia ya kusaidia wengine!.

Huu umangimeza kwenye taaluma ya uwasheria ndio unaoua vipaji, kwa kudhain unajiua kumbe unaungua na jua!.

Chama hakina mwelekeo lakini "you're pround to say wewe ni mwanachama wa TLS"...hii ni aibu kubwa mbele ya wenzenu hasa Mashemeji zenu "Wahandisi".

Majigambo ya wanasheria yamepelekea hata kuona Shirikisho la Afrika ya Mashariki ni kikwazo kwa wa Tanzania kwa kuwa hatujajiandaa na siku zote hatupo tayari kwa mabadiliko. Hivi kama haki zenu mnashindwa kuzitetea huko Mahakamani mnatetea nini?.

Nilidhani Dr. Fauzi ana upeo kumbe ndo tatizo kabisa kwa TLS !
 
By the way, do we still boast of having 'Tanganyika'? Inawezekana hata jina wanachelewa kuli-update.
 
wanasheria wote wa tanzania wako bize kuandaa mikataba ya kuuza nchi through mikataba FEKI!!!
 
Nilianzisha thread inayoitwa Tanganyika Law(less) society !It is a big joke hawa wana sheria wetu!
 
acheni taarabu,wanasheria wamefanya mengi.\
 
Lamwai,Mkono,Chenge ,malegesi etc are our lawyers!
Shame to TLS!
 


MZEE advocate!

hili ni tangazo la kazi ya webmaster lililopostiwa na Chaumbea ,mwezi Juni, 2009 kwn hii JF. Sielewi kama TLS wamepata ujumbe wa wanajamii manake nimejaribu kufuatiliwa sijaweza kuiona tena tovuti kongwe www.tanganyikalawsociety.org.tz hewani . Badala yake kuna maelezo. "This website is currently under construction..." na sina uhakika kama wanachama mmejulishwa au mnafahamu haya ya ujenzi wa tovuti mpya.

Kama hamjafahamishwa basi hayo ndio mapungufu ya kiutendaji na kutokuwa makini kwenye taaluma ikiwa ni pamoja na kutofutailia kabisa yanayoendelea kupitia hiyo tovuti labda kwa kuona haina jipya au vinginevyo.




 
By the way, do we still boast of having 'Tanganyika'? Inawezekana hata jina wanachelewa kuli-update.

ver posibo!!! kwani Dr. Faiz ni m-Tanganyika???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…