AIBU:Simba wafanya ushirikina mechi ya leo Taifa.

AIBU:Simba wafanya ushirikina mechi ya leo Taifa.

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Leo kwenye mechi kati ya simba sc na Lipuli fc kumetokea vitendo vya kishirikina.Ilipofika muda wa mapumziko mchezaji wa simba Dilunga alikataa kutoka kwenye pitch ya uwanja mpaka pale wachezaji wote wa lipuli watoke lakini lipuli fc wakastuka na mchezaji wao mmoja akawa anagoma kabaki uwanjani hivyo mchezaji Dilunga wa simba na mchezaji mmoja wa lipuli wakabaji uwanjani kila mmoja akimsubiri mwenzake atoke mwanzo.

Uwanja ulifurika kwa shangwe kutoka kwa mashabiki lkn wachezaji hao bado wakawa wanategeana kila mmoja akimsubiri mwenzie atoke.Muda ukawa unayoyoma ndipo Dilunga akamfuata mchezaji huyo wa lipuli na kumsihi watoke lkn kituko walipofika kwenye mstari wa kutoka uwanjani wakategeana ndipo dilunga akamsukumiza mchezaji huyo wa lipuli na yeye akafuatia.



Hata hivyo mganga na komandoo maarufu wa simba aitwaye somo alionekana akitoa maelekezo kwenye benchi la ufundi la simba wkt hali ikiwa tete uwanjani.



Video tizameni mpate mwanga vizuri
 
Safi sana,kila mtu na imani yake anayoamini
 
Mbona wachezaji wengi wakubwa duniani wanaweka alama ya msalaba au utatu mtakatifu wakiwa uwanjani? Au wanapiga dua kabla ya mechi kama Salah? Hayo ni mambo ya kawaida, binadamu ana spiritual life, wengine wanaipuuza na wengine hawaipuuzi.

Ila, huyo mzee Somo sijui ndiyo nani? Hapo ndipo soka la Tanzania linapokwama. Hao ndiyo watu wa kufyekelewa mbali na ikiwezekana aadhibiwe kwa ku-approach benchi na kuvunja heshima.
 
Back
Top Bottom