Aibu,vyoo vya shule karne ya 21

Aibu,vyoo vya shule karne ya 21

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
choo.jpg

Choo cha shule

Huduma za vyoo katika shule mbalimbali nchini inaonekana mbaya kiasi cha kutishia uhai wa wanafunzi na walimu wanaovitumia.
Wataalamu wa masuala ya elimu na saikolojia, wanaibainisha pia kuwa vyoo vinapokuwa duni, vinachangia kudumaza maendeleo sekta ya elimu kwa sababu wanafunzi wenye kuhara, kwa mfano au wa kike hulazimika kutokwenda shule hasa wanapokuwa hedhi kwa vile wanashindwa kujisitiri.

Shule ina wanafunzi 400 haina vyoo
Shule ya Msingi Lugalo iliyopo Kata ya Mazombe, wilayani Kilolo mkoani Iringa yenye zaidi ya wanafunzi 400 ni kati ya shule ambazo kwa miezi mitatu hivi mfululizo imekuwa ikielezwa kutokuwa na vyoo thabiti, achilia mbali uhaba mkubwa wa madawati, kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Joseph Kinyanya.

Shule ina matundu 16 ya vyoo vilivyojengwa kwa miti, ambayo imeoza, mwalimu huyo mkuu ana hofu huenda ikafungwa kwa kuonekana kama eneo lisilo salama kwa watoto, kwani wanaweza kupoteza maisha kwa kutumbukia chooni. Kati ya shule 96 za msingi za wilaya hiyo, Lugalo mara kadhaa imekuwa ikishika nafasi ya tano, hata hivyo Mwalimu Kinyanya, ana hofu huenda maendeleo haya yakawa mabaya ikiwa mazingira hayataboreshwa haraka. chanzo.http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1717038/-/item/0/-/6rq4emz/-/index.html
 
MziziMkavuhapo chacha umejikamatisha mwenyewe ulikuwa unalalamika kuwa majengo yetu ya airport sio nikakuambia tuna mambo mengine ambayo ni muhimu na lazima na yanahitajika kuangaliwa kabla ya majengo ya airports
 
Last edited by a moderator:
choo.jpg

Choo cha shule

Huduma za vyoo katika shule mbalimbali nchini inaonekana mbaya kiasi cha kutishia uhai wa wanafunzi na walimu wanaovitumia.
Wataalamu wa masuala ya elimu na saikolojia, wanaibainisha pia kuwa vyoo vinapokuwa duni, vinachangia kudumaza maendeleo sekta ya elimu kwa sababu wanafunzi wenye kuhara, kwa mfano au wa kike hulazimika kutokwenda shule hasa wanapokuwa hedhi kwa vile wanashindwa kujisitiri.

Shule ina wanafunzi 400 haina vyoo
Shule ya Msingi Lugalo iliyopo Kata ya Mazombe, wilayani Kilolo mkoani Iringa yenye zaidi ya wanafunzi 400 ni kati ya shule ambazo kwa miezi mitatu hivi mfululizo imekuwa ikielezwa kutokuwa na vyoo thabiti, achilia mbali uhaba mkubwa wa madawati, kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Joseph Kinyanya.

Shule ina matundu 16 ya vyoo vilivyojengwa kwa miti, ambayo imeoza, mwalimu huyo mkuu ana hofu huenda ikafungwa kwa kuonekana kama eneo lisilo salama kwa watoto, kwani wanaweza kupoteza maisha kwa kutumbukia chooni. Kati ya shule 96 za msingi za wilaya hiyo, Lugalo mara kadhaa imekuwa ikishika nafasi ya tano, hata hivyo Mwalimu Kinyanya, ana hofu huenda maendeleo haya yakawa mabaya ikiwa mazingira hayataboreshwa haraka. chanzo.http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1717038/-/item/0/-/6rq4emz/-/index.html

Waafrika ndivyo tulivyo. Unashangaa kuona samaki ferry??
 
Back
Top Bottom