Aibu ya mwaka muce-iringa

logbes

Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
88
Reaction score
20
Wasomi( Walimu na wanafunzi) zaidi ya 70 wapewa 5000 ili wapokee kadi za CCM tarehe 26/1/2013 kwa Philip Mangula. Kama wasomi mnakubali kuhongwa 5000 je tulioko Vijini hatujui vizuri Madudu yanayofanywa na Serikali isiyokuwa makini hii tutapokea sh Ngapi? Kuna watu walikuwa mstari wa mbele kulaumu Wagombea mamluki wa CDM( mfano Mbeya Vijini na Isimani-Iringa) kwa kuhongwa milioni kadhaa kama wasaliti je wanaokubali kupewa 5000 tuwaweke kundi gani? Badala ya kupigania Promotion we unapigania kupata kadi ya Chama Cha Mafisadi. Inasikitisha.
 

Mkuu tupatie vipande vya ushahidi badala ya kuporomosha matusi kwa wasomi wetu.

 
Someni vijana acheni hizi siasa za makelele hazitawasaidia kitu........tengenezeni G.P.A mje tupambane huku mtaani hakuna CDM wala nini kitakupa ugali wee jidanganye
 
International pumba point

Pole saana labda huijui ccm. Kama rais aliwahi kufungua miradi hewa, kama rais aliingizwa mkenge juu ya Ambulance aliyekuja kupokea mkuu wa Wilaya mwingine badala ya yule mtarajiwa, sembuse hii ya kutoa 5000 ili kununua wanachama wafu ili mradi tu Mzee wetu Mangula, aone kweli kuwa watu wanaipenda ccm. Wasipofanya hivi viongozi wa ccm mkoa wa Iringa si hawataonekana kuwajibika mbele ya katibu wao mkuu. Wacha wadanganyane!! Maana wajinga ndo waliwao! Hata mimi ningechukua hii pesa, ningepokea kadi ya Mangula, kesho yake ningeitupilia mbali... CCm Toa pesa, mimi pokea, ila nguvu yangu kazi iko kwingine.
 
Hatufanyii kazi MAJUNGU, toa hoja zenye mashiko pamoja na USHAHIDI mwanana plz!
 
Mkuu ni haki yao, waache wachukue. Siku hizi ni kula CCM; kura kwa chama makini. Wagawaji waache wagawe sana na wapokeaji waache wapokee sana. Nimeongea na mmoja ameniambia watazichoma moto baada ya muda.
 
Someni vijana acheni hizi siasa za makelele hazitawasaidia kitu........tengenezeni G.P.A mje tupambane huku mtaani hakuna CDM wala nini kitakupa ugali wee jidanganye

Mwigulu ukole Mayo, nakukubali mayo tileka shida mbwane we.
 
Someni vijana acheni hizi siasa za makelele hazitawasaidia kitu........tengenezeni G.P.A mje tupambane huku mtaani hakuna CDM wala nini kitakupa ugali wee jidanganye
Watakula hizo G.P.A??
 
Kumbe hako kamtindo bado kanaendelea?.Niliwahi kushuhudia chuo cha RUCO Iringa pia,viongozi wa CCM chuoni wakihimiza watu kuhudhuria mikutano ya Kingunge na viongozi wengine kipindi walipokuja mkoani miaka ya nyuma na kudai kuwa 'mtarejeshewa gharama ya mahudhurio yenu' yaani mtafidiwa mahudhurio yenu(kupewa elfu 5)ikiambatana na kukatiwa kadi za chama ambayo utapaswa ulipie ada ya mwaka mzima-ni sawa na wanajinunulia kadi wenyewe na kuzigawa bure.
Sikatai,hilo ni jambo la kweli kabisa.
 
eti wana wa MUCE ni kweli? Tunaomba ufafanuzi wenu please! Lakin itakuwa kweli mana mwisho wa semster boom linakuwa limekata,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…