SoC02 Aibu yenye kuleta heshima (binti jikubali)

SoC02 Aibu yenye kuleta heshima (binti jikubali)

Stories of Change - 2022 Competition

Angshine

Member
Joined
Aug 26, 2022
Posts
11
Reaction score
23
Kwenye maisha kila mtu Mungu alimleta kwa makusudi yake na wakati wake pia. Lakini wengi husahau kuwa kupitia kusudi aliloitiwa duniani, yampasa akubali pia njia atakayopitia kufikia kusudi hilo, haijalishi njia itakuwa na miiba kiasi gani, lakini yakupasa uikubali ili kufika kule uendako.

Ni ukweli usiopingika kuwa, kabla ya kupata kitu fulani, kitu kingine hutangulia.
Mfano:- Kabla ya kupata heshima, huanza aibu.
- Kabla ya kufaulu, huanza kufeli.
- Pia kabla ya kushiba, huanza njaa.

Dhumuni la kuandika chapisho hili ni kuhitaji kujifunza na kujikubali hasa mabinti wa kike, nikiwa na Imani kuwa ni vijana tunaopitia changamoto nyingi mno katika kufikia ndoto zetu tulizonazo.

Kwenye maisha Kuna wakati yatupasa kufanya maamuzi magumu ili kuleta utukufu kwa Mungu na matokeo chanya kwa yale tunayoyahitaji. Japo ni wachache Sana hukubali kulipia gharama ya maamuzi wayachukuayo, wengi hawapo tayari kubeba hualisia, hivyo hutafuta njia mbali mbali kwa ajili ya kuuficha ukweli na kuweka bayana yale ambayo wanahisi yataweza kupendezesha macho ya watu, hata kama yatakuwa kinyume na Mwenyezi Mungu.


HISTORIA YA BINTI SARA KWA UFUPI, YENYE FUNZO NDANI YAKE.

Sara ni binti wa kwanza katika familia ya watoto 4, ni mtoto pekee anayeangaliwa kwa jicho la tofauti sana, kwani ni yeye tu ndiye aliefanikiwa kufika elimu ngazi ya chuo katika ukoo wao.

Binti huyu ametokea katika familia ya kawaida kabisa, hivyo alikuwa akitamani sana kuikwamua familia yake kupitia yeye.

Alipofika chuoni aliamua kujihusisha zaidi na maswala ya kikanisa, kwani chuoni hapo kulikuwa na taratibu za ibada kama ilivyo kawaida ya kwamba MUNGU KWANZA. Sara aliona ya kuwa, ili kuepuka vishawishi na changamoto mbali mbali ambazo aliwahi kuzisikia huko mitaani kuhusiana na vyuo ikiwemo (kupata ukimwi kwa kujiuza mwili) akaona kujihusisha na ibada na kanisa kwa ujumla itakuwa ndio salama yake.

Basi siku zikasonga Sara akawa mdada mzuri mwenye hofu ya Mungu, tena akapata hata uongozi wa chuo na ibadani kutokana na bidii aliyokuwa nayo binti huyu.

Lakini Sara alikutana na Kijana mmoja ambaye alimwelezea kumueleza hisia zake na kumkubali Kati ya wengi waliokataliwa kutokana na uoga wa kukiuka maadili ya kidini ikiwemo kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa.

Sara aliamini kuwa Kijana huyu atakuwa msaada mkubwa kwake na familia kutokana alikuwa ametokea kwenye familia yenye uwezo kidogo wa kifedha.

Siku zilikwenda, Sara akapata ujauzito wa Kijana huyo, lakini cha kushangaza alikuja kugundua ukiwa na miezi mitano(5) kutokana na kwamba haukuwa anapata zile dalili za kumuonyesha moja kwa moja ya kuwa ni mjamzito, zikiwemo
- Kutapika
- Kuchagua vyakula
- Kuongezeka tumbo na nyinginezo.

Sara alikuwa hana dalili kama izo,yeye haswa hakuwa anapata siku zake ikiwa ni dalili kuu ya kuwa mjamzito.
Lakini kila alipokwenda hospitali alikuwa akielezea tatizo hilo na kuambiwa kuwa ana maambukizi makali sana ya mkojo yaani (UTI) na kupewa dawa na sindano Kisha kuendelea na mambo yake ya kawaida.

Kadri miezi ilivyokuwa inakata, Sara hakuwa anaona siku zake...... ndipo alipochukua maamuzi ya kuamua kupiga ultra saundi na kugundulika kuwa mjamzito tena wa miezi mitano(5).

Hapo ndipo Sara alipochanganyikiwa na kuamua kumjuza mpenzi wake.

Lakini mpenzi akamwambia kuwa itakuaje kwa sababu hawezi kulea kwa wakati huo kwani hajajipanga bado, hivyo yampasa atoe ujauzito huo.

Ndipo Sara alipoumia sana na kubaki njia panda hajui lipi la kufanya,ukizingatia amekuwa akiaminiwa na Familia yake na ndugu kwa ujumla kuwa ndio tegemeo kwao.

Basi alichoamua Sara alisema....... Ni kweli nimemkosea Mungu wangu, Familia yangu, ndugu zangu na jamii kwa ujumla lakini siwezi kufanya tena kosa lingine la kutoa ujauzito huu kwa kuficha kosa la kuonekana mzinifu wakati nimeokoka na wengi wanajua hivyo.

Nipo tayari kulipia gharama ya makosa niliyoyafanya kwa kubeba aibu na fedheha...... Lakini baada ya kujifungua mtoto huyu nitaendelea na masomo yangu.

Ikumbukwe kuwa alikuwa akiwa mwaka wa kwanza wa Diploma akiwa na miaka (19) kwani hakupitia kidato cha sita(6).

Basi akafanya maamuzi ya kurudi nyumbani kwao na kuwaeleza wazazi wake kila kitu kilichotokea... Wazazi wake walilia Sana na kuumia mno kwani ni binti wa pekee walikuwa wakimtegemea afanikiwe ili asomeshe wadogo zake.

Basi, Sara akamwambia mama yake kuwa ataenda chuoni kumalizia mitihani yake, pamoja na fieldi kwani mimba ilikuwa bado ina miezi 5.

Akafanya mitihani yake, akamaliza na fieldi lakini Mungu alivyo wa ajabu...... Baada ya kumaliza fieldi yake, Sara akajifungua mtoto wa kiume akiwa na miezi 7 yaani njiti.

Akampiatia Jina la USHINDI kwani hakutegemea Yale Mungu amemfanyia, huku chuo kikimuhitaji mwezi wa 11 yaani miezi 3 baada ya kumaliza mitihani na fieldi kuingia mwaka wa pili wa Diploma yake.

Sara alijifungua salama, japo maneno yalikuwa mengi mno kwamba alikuwa akitumia mgongo wa kanisa kufanya maovu yake, wengine walisema ni mlokole wa mchongo, kiongozi asiye na sifa ya kuongoza wengine, akatengwa na kanisa, marafiki, ndugu lakini Mungu hakumwacha Sara.

Baada ya muda kidogo Familia ilimpokea na kumkubali tena,ilimsamehe, na kugundua kuwa alikosa na amejifunza kupitia makosa hayo, Baba wa mtoto aliomba msamaha na kujitambulisha kuwa baba halali wa mtoto yule. Lakini cha kufurahia zaidi ni kwamba.

Sara alimaliza chuo akiwa na GPA nzuri sana, ya kuwaziba midomo wale wote waliomzungumzia vibaya hapo awali.

Alifanya mahafali vizuri na mtoto wake akiwa na mwaka mmoja(1) wenye afya njema tena huwezi kujua kama alizaliwa njiti.


FUNZO.
Mabinti wengi hasa wanachuo wamekuwa wakifanya dhambi ya kuuwa yaani kutoa mimba kwa kuhofia
- Kusemwa vibaya na watu
- Kuonekana wasiofaa mbele ya jamii,

Na wengine kuogopa kukosa soko pia, Lakini nina Imani kipo kitu cha kujifunza kupitia dada Sara.

Alionyesha ujasiri na msimamo wake, alikubali kulipia gharama na kudharaulika na kuitwa mlokole wa mchongo, lakini mwisho wa siku Mungu alimuheshimisha kwa kuonyesha maamuzi aliyochukua ya kulea ujauzito yalikuwa ni maamuzi sahihi Sana.

Atukuzwe Mungu kwa kumfanya Sara kuwa ushuhuda kwa mabinti wengine

Imeandikwa na Angshine
 
Upvote 2
Ni story halisi ya mtanzania fulani.... japo siwezi kukuaminisha kitu ambacho umeshakataa kuamini
 
Back
Top Bottom