mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 901
- 1,742
1. Watch Videos and Get Paid (Angalia Video Youtube na Ulipwe)
Hakuna pesa inakuja kwa kutizama wananzengo tufanyeni kazi jamani.
•Mara nyingi, wanakutaka uweke hela kwanza kabla wao hawajakulipa
•Wanakupa points ambazo huwezi kuzitoa, points zinazo onekana kama pesa
•Mwisho wa siku, umepoteza muda na pesa na hujapata kitu
2. Cryptocurrency- wanakuambia Bitcoin mining kwa kutumia Simu
•Huwezi ku Mine Bitcoin na simu yako
•Hizo Apps zinaiba data zako au zinakuomba hela ya “upgrade.”
•Mining halisi inahitaji vifaa vya gharama kubwa na vyenye uwezo mkubwa sana, sio simu yako , simu yako ina uwezo mdogo wa ku mine bitcoin
3. Betting Odds za Uhakika "sure bet"
•Wanasema wanajua matokeo ya mechi kabla ya kuchezwa
•Unatuma hela kununua odds za “sure bet” lakini unakula hasara.
•Hakuna mtu anayeweza kutabiri matokeo kwa uhakika wa 100%. Fanya kazi hakuna utajiri wa haraka na raisi hivyo.
4. Forex Trading unauziwa Binary Trading Bots
•Unaambiwa kuna bot inafanya Trading kwa niaba yako na inakuletea faida bila hasara wewe ni kuliwasha na kulizima tu.... huogopi ??
•Ukiweka pesa zako, hazirudi.
•Wanakuvutia na screenshot za faida feki, magari makali waliokodisha na airbnb apartments wanazokaa kwa kupangisha na kulipa kwa siku....Forex trading ni kazi kama kazi zingine na husomewa kuanzia miaka 3 na kuendelea.... acheni mihemuko !!!
5. Tuma Pesa kwa Radio Ushinde Zawadi
•Unaambiwa utashinda zawadi kwa kutuma pesa mf:500
•Ni lazima utume pesa ili kushiriki
•Mwisho zawadi hiyo itakuwa ndoto – pesa zako zitaenda.... hii inatumika sana na vituo vya redio na television sasa hivi !! Wacha huu ujinga hakuna mtu anashinda milioni 10 kwa kuweka 500 kua na akili hebu....
6. Mzigo Wako Umefika, Tuma Pesa Nairobi ili usipotee airport
•Unaambiwa mzigo wako umefika na unahitaji kulipa custom
•Basi ukilipa, pesa zako zimeenda – mzigo haupati kabisa
•Hii wengi wamepigwa na wanaija & Wakenya. Mnao agiza mizigo tumieni legit Company ambazo una track mzigo wako tangu mwanzo mpaka unapokea.
7. Ponzi Scheme "Fake Online Investment Platforms" Jiunge na watu wajiunge chini yako
•Unaambiwa unaweza kuwekeza pesa yako na kupata returns kubwa haraka
•Niponzi scheme
•Ukiweka pesa zako, kuna siku itazimwa utaloose
Au unaambiwa wekeza kwenye mradi wa nguruwe, au kilipo cha Vanilla ebwana weee kama pesa yako haina kazi peleka kwa Lugumi isaidie kulea watoto Yatima achana na huu ujinga !!
8. Mikopo ya Mtandaoni kuna Apps za kukopesha Zinazodai Fees Kabla ya Mkopo
•Unaambiwa utapata mkopo haraka, lakini kwanza unalazimika kulipa ada ya usajili
•Pesa zako zimeingia kwao na mkopo haupo – kwisha habari yako kenge wewe
9. Nafasi za kazi Feki Online "Fake Job Offers & Visa Scams"
•Unaambiwa kuna kazi za nje ya nchi lakini kwanza lazima uweke pesa ya processing fees. Jifunze kufuatilia kwa undani kila taarifa unayoipokea kwenye Medula Oblangata yako.
10. SMS ZA KUSHINDA - Umeshinda Simu Mpya au Gari,
•Unapokea simu au SMS ukijulishwa kuwa umeshinda simu au gari ama umepata ajira
•Ili upokee, unatakiwa kutuma gharama za usafirishaji au kodi, aisee tumieni akili basi .... ntarudi na zingine lakini kwa sasa hizi ndio zinazo ongoza kwa kula pesa za wabongo !!