Aina gani ya maharage yenye bei nzuri sokoni

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,001
Reaction score
1,430
Nina eneo kubwa nataka kulima maharage.

Naomba kujua ni aina gani ya maharage inapendwa sana sokoni na bei yake imechangamka sokoni.

Ukinipa na mbegu inakopatikana itapendeza. Eneo heka 2
 
watu wengi mjini wanakubali sana combat, bei inaweza ikawa sio kubwa sana kama aina nyingine lakini sokoni inafanya vizuri pia ili uwe na bei nzuri inakubidi utoe yenye hali nzuri. (grade)
 
Maharage yenye bei ni soya ya njano hasa kama ukilima ile gololi. Ukilima ngwara ni deal ila hiyo uuze Kenya kibongo hailiwi.

Unaweza kulima pia Rose Koko (Nyayo), Soya Kijivu, Combat au Kichumbaa.
 
Maharage yenye bei ni soya ya njano hasa kama ukilima ile gololi. Ukilima ngwara ni deal ila hiyo uuze Kenya kibongo hailiwi.

Unaweza kulima pia Rose Koko (Nyayo), Soya Kijivu, Combat au Kichumbaa.
Aise umenikumbusha mbali na maharage ya kichumbaa tuliotesha sna na ile inaitwa lovirondo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Natafuta ya kijivu (soya kijivu) wapi naweza pata
 
Ni mkoa na wilaya ipi kwa kilimo cha maharagwe ya njano yanakubali sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…