Aina kadhaa za rushwa,hata wanaojifanya kupinga rushwa,wanatoa rushwa

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Kuna Aina nyingi Sana za rushwa.
  • Fedha
  • Mapenzi
  • Vyeo
  • Ahadi.
Tanzania tuna Rais anaepinga rushwa kwa vitendo.

Je, Rais huyu ameweza kuzuia rushwa ya fedha kwa baadhi ya VIONGOZi wa kisiasa kutoka vyama vya Upinzani?

Je, Rais wetu huyu kipenzi ameweza kuzuia rushwa ya vyeo kwa VIONGOZi wa vyama vya Upinzani?

Je Rais wetu huyu mchukia rushwa ameweza kuzuia rushwa za ahadi mbalimbali za vitu vinono kwa VIONGOZi wa vyama vya Upinzani?

Rushwa ni rushwa tu, iwe ya fedha, mapenzi, ahadi zote ni rushwa tu.Takukuru na mahakama zetu zinatakiwa zimuunge mkono raisi wetu kipenzi kutokomeza rushwa.

Rais wetu kipenzi anajenga Taifa la wastaarabu. Miaka 15 Ijayo Tanzania itakua Taifa la kistaarabu kabisa lisilokua na rushwa. Kama vile Rais wetu alivuoanza kupambana na vyeti feki nadhani hata kura feki pia hazipendi na atapambana nazo
 
Hizi nyingine kejeli sasa.
 
hahahaa ukitaka vichekesho kama hivi tuma neno cheka kwenda 1373
magu anapinga rushwa tangu lini
 
Nani alikwambia wale wa TACAIDS hawanaga UKimwi?
 
Ungeelekeza swali kwake kwanza
 
Kejeli ni aina mpya ya rushwa,fafanua tafadhali.
Nasema hivi.

Kusema mtu aliyesema trafiki wakipewa hela ya rushwa si rushwa ni hela ya kupigua brashi tu anapinga rushwa, hiyo ni kejeli.

Kusema mtu anayekataa manunuzi ya serikali kufuata open tender process ni mtu anayepinga rushwa, hiyo ni kejeli.

Kusema mtu anayesema atawapiga mpaka shangazi za waziri mkuu wake ni mstaarabu, hiyo ni kejeli.

Kuna maneno mengine unayasikia halafu unajiuliza huyu mtu anaweza kuwa mjinga hivi?

Au anafanya kejeli tu?

Maana hapa JF kuna wanafasihi wengi.

Wana ndimikuwili zinazoweza kukumwagia sifa, zinazokutusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…