Aina mbili za mataifa maskini

Aina mbili za mataifa maskini

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Kuna aina mbili za mataifa maskini; Kuna taifa ambalo ni maskini lisilo kuwa na matumaini na kuna taifa ambalo ni maskini lakini lenye jitihada.

Taifa lolote maskini na lenye jitihada ni lazima liongozwe na maono na matumaini ya kufanikisha hayo maono. Kwakuwa wanaamini umaskini sio kitu cha kudumu ni cha kupita. Wanajua utajiri ni zao la akili, busara, jitihada na maarifa.


Kuwa maskini na kukosa matumaini hupelekea kuwa na ufukara. Kwahiyo taifa fukara ni lile maskini na watu wake wamekosa matumaini na baadae yao. Hili kamwe halitoendelea. Mataifa mengi ya Afrika yapo hapa.
Na huku ni kukosa jitihada tu.

Kwetu sisi kama watanzania kuna matumaini kama tutabadili mwelekeo wa fikra zetu wa sasa. Kwakuwa kuwa maskini na kutofanya jitihada za dhati za kuondokana na umaskini huo ni uvivu na uvivu ni ufukara.

Kuna aina mbili za uvivu.

1. Uvivu wa kimwili

2. uvivu wa kiakili.

Ni muhimu sisi kama taifa kuondokana na uvivu wa aina zote mbili kama tuinataka kuendelea. Na ni muhimu kuwa watu wenye malengo na dhamira moja.

Ni vigumu kuamini kwa taifa kama Tanzania lenye maliasili kibao kuendelea kuishi katika ufukara. Ni muhimu kutambua ugonjwa wetu ili tuupatie tiba mbadala. Kwakuwa bila kugundua chanzo cha ugonjwa hatutaweza kuutibu.
 
Back
Top Bottom