Sadick Kilasi
New Member
- Apr 9, 2018
- 1
- 0
Stori ya pesa na mafanikio ni stori ambazo zimekuwa zikizungumzwa kila siku katika maisha yetu.
Stori hizi hazihitaji hata watu wawili kwani hata mtu mmoja mmoja peke yake anaweza kujipia mwenyewe ndani kwa ndani. Pesa na mafanikio kimekuwa kitu ambacho wengi sana wanazungumzia katika maisha.
Kutokana na njaa ya watu wengi kuhusu pesa, basi wengi wamekuwa wakitumia njia hiyo hiyo kutapeli wengine. Ama kweli waweza kutawala mtu kupitia tamaa yake mwenyewe.
Watu wamekuwa wakitafuta pesa kwa njia mbalimbali kwa kutaka kufikia mafanikio. Pesa imefanya maisha ya watu kuwa magumu zaidi badala ya kuwasaidia. Wengi wamekuwa wakiwaona wengine wakiwa wamefanikiwa katika maisha yao, wenye majumba yao, magari yao na starehe zao.
Vijana wengi husema haya si ndiyo maisha sasa. Ukweli ni mitazamo hii imekuwa inawafanya watu kutafuta pesa kwa nguvu hata kufikia wakati mwingine wanaharibu maisha ya wengine kwasababu ya pesa. Ama kweli pesa mwanaharamu.
Mtazamo juu ya pesa na utajiri umekuwa ukiwasumbua vijana wengi sana. Huu ndio mtazamo wa kwanza ambao umekuwa ukiwasumbua wengi sana katika kutafuta mafanikio na mwisho kwa bahati mbaya wamejikuta wanaishia katika maumivu makubwa hata baada ya kupata kile ambacho walikuwa wanakita ama la wameshindwa kupata kabisa.
Mpendwa msomaji, kuna aina ya pili ya mtazamo wa pesa na maisha kwa ujumla ukiachana na mtazamo huo wa kwanza ambao umekuwa ukiangamiza maisha ya wengi bila ya kujali anajua ama hajui. Mtazamo huo wa kwanza umekuwa ukifanya maisha ya watu kama vile maisha ni kupanda mlima mkubwa na mrefu, ukifika kwenye mafanikio au kilele huna hamu tena na mafanikio kwa jinsi ulivyochoka.
Mpendwa msomaji, unafikiri huu mtazamo wa pili umebeba siri gani ambayo mhusika huwa anapata mafanikio makubwa na yenye furaha katika kilele chake cha mafanikio?
Wako Sadick Kilasi,
mwandishi wa blogu ya jikolaushauri.blogspot.com,
Mawasiliano ni sadikila65@gmail.com au 0687000768,
Tuma ujumbe nitakujibu.