Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,422
Wakati unapoanza biashara, wewe unachojua ni kwamba unahitaji wateja ili biashara yako iweze kufanikiwa. Wafanyabiashara wengi huwa wanafikiri wateja wote ni sawa na hivyo kujiandaa kutoa aina moja ya huduma kwa wateja wa biashara zao.
Lakini ukweli ni kwamba wateja wote wa biashara yako hawako sawa. Kuna aina tofauti za wateja kulingana na tabia zao na hata mitazamo yao. Wewe mfanyabiashara unapojua aina hizi tofauti za wateja unaweza kuwahudumia vizuri na biashara yako ikakua kama unavyotaka.
Karibu ujifunze aina hizi tano za wateja na jinsi unavyoweza kuwahudumia vizuri;
1. Wateja wanajua wanachotaka na wapo tayari kukipata.
Hawa ndio wale wateja ambao huwa tunawafikiria wakati tunaanza biashara. Mteja anakuja na anajua anachotaka ni nini, ukishampa analipa na kuondoka zake. Hakuulizi maswali mengi, haombi punguzo la bei na hasumbui kulipa.
Hawa ni wateja wazuri sana kwenye biashara yako, ila pia ni wachache. Kuhakikisha unaendelea kuwa na wateja hawa, wapatie kile kilicho bora, hakikisha wanapata kile kweli wanachotaka.
2. Wateja walio makini na thamani wanayopata.
Hawa ni wateja ambao wanajua wanachotaka, ila pia wanahakikisha gharama wanayolipia ndio gharama halisi. Wateja hawa watakuuliza maswali mengi sana kuhusiana na kile unachowauzia, watajaribu kulinganisha vitu mbalimbali na kuona kama wanachopata ni bora kwa gharama wanazolipa. Hawa ni wateja ambao unaweza kuwaona ni wasumbufu, ila kama utawapatia uhakika, watanunua kwako.
Kwa wateja hawa hakikisha unawapa taarifa zote wanazohitaji, hakikisha unawapa uhakika kwamba manunuzi wanayofanya ni bora kwao. Na uwe na uhakika kwamba ni manunuzi bora kwao. Na utaendelea kuwa nao kwa muda mrefu.
3. Wateja wanaotaka kupata zaidi ya wanachotoa.
Pia utakutana na wateja ambao wanataka kupata zaidi ya kile wanachotoa. Hawa ni wateja ambao utawaona wakati ambapo umetoa ofa au una promosheni. Hawa wanakuja na watanunua kwa kiwango kikubwa sana kama wana uhakika wa kupata zaidi kwa gharama kidogo. Wateja hawa ni gharama sana kuwa nao hasa kama faida unayotengeneza ni kidogo.
Kunufaika na wateja wa aina hii toa ofa ambazo zina faida ya kukuwezesha wewe kuweza kuendesha biashara yako na kuikuza. Ukitoa ofa bila ya mpango mzuri inaweza kukuumiza wewe mwenyewe.