Aina tano za pesa zenye nguvu duniani...WHY

Aina tano za pesa zenye nguvu duniani...WHY

Attachments

  • Screenshot_2017-01-26-16-11-13.png
    Screenshot_2017-01-26-16-11-13.png
    147 KB · Views: 96
Malyenge umeelewa vizuri nilichokuwa nasema..watu wengi wanadhani dola ndio yenye thamani kubwa kwa kuwa inaonekana kila sehemu sivyo..katika currency kumi zenye thamani duniani us dola haipo..kuna vinchi vidogo visivyojulikana lakini pesa zao zipo juu sana..kuwaiti dinar ukiwa nazo 2000 ata waarabu wenyewe watakushangaa is so poweful..ni mara tatu ya dola..chasa anasema hajawai kuziona kwenye exchange zipo...au tumia tu simu yako google currency conveter itakupa jibu..nashukuru sana kunielewa malyenge
Kitu gani kinafanya pesa iwe na thamani? Hili swali nimejiuliza, mf; Zambia iliongeza thanani ya pesa yake sina uhakika na figure but ni kama elf moja wakaifanya iwe tsh moja. Je ukifanya hivyo hata kwa shilongi utasema pesa yetu inathamani kwa ulinganisho uliofanya?
 
Aliyeanzisha mada halewi sana nini maana ya fedha kuwa na nguvu

Ili fedha iwe na nguvu lazima uangalie je inakubalika kwa matumizi kiasi gani worldwide?

Au kwa lugha rahisi je mzunguko wa fedha ni mkubwa kiasi gani duniani?

Kwa maana hii US dollar ndiyo fedha yenye nguvu zaidi.
 
Kitu gani kinafanya pesa iwe na thamani? Hili swali nimejiuliza, mf; Zambia iliongeza thanani ya pesa yake sina uhakika na figure but ni kama elf moja wakaifanya iwe tsh moja. Je ukifanya hivyo hata kwa shilongi utasema pesa yetu inathamani kwa ulinganisho uliofanya?
Serikali kupitia central bank wakiamua kupandisha au kushusha thamani ya fedha wanafanya hivyo purposefully.

Kwa mfano central bank inashusha thamani ya fedha ili kusaidia kuuza zaidi bidhaa nje. Hapa wanunuzi toka nje wanashawishika kwasababu wananunua bei nafuu

Kadhalika central bank ikiongeza thamani ya fedha inasaidia nchi husika kununua bidhaa nje kwa unafuu

Lakini yote hayo kupandisha/kushusha thamani ya fedha kama nilivyosema yanafanyika purposefully na ni kwamuda tu

Ili fedha iwe na thamani isiyoyumba inabidi nchi iwe inauza bidhaa nyingi nje ili ipate fedha za kigeni nyingi zaidi. Na hii ndiyo inaipa nguvu sarafu/fedha ya nchi.

Uarabuni fedha yao inathamani kwasababu wao wanapata fedha za kigeni nyingi kwa kuuza mafuta
 
Back
Top Bottom