Swali zuri na linaeleweka halina haja ya kulibabaisha wala kujibabaisha.
Kwa kuwa umeuliza as if u are "layman" in the field, na mimi naekujibu pia najifanya kama "layman" katika majibu yangu. Ukisoma kwa pamoja na majibu ya sijui nini, mtaalam aliyetolea ufafanuzi wa "Thamani ya pesa na nguvu ya pesa" mi naongeza yafuatayo:-
Ukiitoa Marekani ambayo stability and strength ya fedha yake inategemea zaidi na kukubalika kwake duniani kote(hili somo refu kidogo tuliache), na UK ambayo thamani yake inatokanana mfumo mzuri kabisa wa fedha ulioko UK (London na miji mingine ya UK ndiyo kitovu cha soko la fedha (Strong Financial system based cities), nchi nyingine ulizozitaja hazina sifa ya nchi hizo mbili. Lakini, thaman ya fedha inategemea na ukubwa na upana katika uzalishaji wake wa bidhaa tofauti ambazo ina-trade na nchi nyingine duniani. Katika muktadha huu:-
1. Nchi ambazo zina uwezo wa kuzalisha sana kiasi cha kutosha na ku-export sana inatarajiwa kuwa fedha yake itakuwa "imara" na thamani yake relatively cheaper. Kinyume chake, ikiwa nchi haizalishi na wala haiuzi sana nje lakini fedha yake ni "relatively cheaper" jua hapo kuna matatizo ya uchumi hivyo yanahitaji maelezo mengine.
2. Nchi ambazo hazina upana wa uzalishaji wa bidhaa tofauti-tofauti na hivyo kutarajia ku-import sana sehemu kubwa ya bidhaa zake (non-reciprocally) inatarajiwa kuwa fedha yake itakuwa juu(bidhaa kuwa ghali sana) kwa kuwa bidhaa zote ni imported (kinyumeche, nchi ina matatizo ya kiuchumi hivyo itahitaji maelezo ya ziada kuelezea). Je kwani Kuwait, Bahrain, Oman, na nyinginezo hazizalishi, si wanazalisha mafuta? Jawabu ni kwamba, mafuta katika uchumi ni bidhaa inayoitwa "inelastic" (less responsive) product, kwamba kubadilika kwake kwa bei kwa kiasi fulani hakubadilishi demand yake. Ndiyo maana wakati nchi zinapigana kushusha thamani ya bidhaa zake ili kuzifanya ziwe rahisi nje, hawa jamaa wana umoja wa kuongeza bei ya bidhaa yao hiyo, na dunia haitaacha kununua isipokuwa kusikitika na kuwaomba wasipandishe bei(which is contrary to normal trading principle). Kwa hiyo katika kanuni za kawaida za kibiashara za kimataifa, zina ushindani mdogo wa 'kucheza na thamani ya fedha"(Devaluation and revaluation) ili kukidhi mahitaji fulani hususan ya kuongeza mauzo yake nje. Hata hivyo, nchi kama Dubai iko tofauti cause pale Dubai kuna "large number of financial markets" hususan kwa bidhaa za mafuta, utalii nk na hata thamani ya fedha yake ni relatively cheaper. Maelezo yooote haya, matumizi yake hayana budi kusimamiwa na kitu kiitwacho "other things remain constant"-(ceteris paribus)